Huyu kijana alinikosanisha na rafiki wa karibu, na ikaonekana ninafuga jini

Huyu kijana alinikosanisha na rafiki wa karibu, na ikaonekana ninafuga jini

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Kuna siku nilitembelewa na rafiki pale nyumbani, basi kama wazee tukaona sio mbaya tukikaa nje pembeni kidogo ya nyuma palikua na mti mkubwa uliofanya kivuli safi kabisa.

Nilimuita yuke kijana wangu mnae mjua, kisha nikamuagiza viti na akaleta viwili pale. Sasa wakati tumekaa na rafikiyangu yule, kisha nikamuona kijana wangu pembezoni mwa nyumba kwa mbaali kama kuna jambo analifikiri hivi, anyway nikjisemea moyoni kwamba ngoja mgeni aondoke then nitaongea na huu mwamba nisikie kulikoni.

Sasa huyu rafiki yangu yeye ni mvutaji mzuri wa sigara, kama kawaida akaitoa na akaishika kwenye mkao wa kuivuta wakati bado hajaiwasha alitaka asimame na asogee pembeni kidogo ndipo aiwashe kuepuka kunikera na moshi. Wakati bado hajanyenyuka, nikamcheki huyu kijana akisogea tulipo kwa tahadhari sana, na kisha akaiwasha sigara ya mgeni wangu pasioo yeye kujua.

Kwakua mimi nilimuona nilijisemea tu ebu ngoja nikae kimya na nione hatma ya hili, then kijana akaondoka kurudi ndani wakati huyu mgeni hajamuona.
Sasa huyu mgeni wangu alipo tamalaki, akaanza kushangaa kwamba sigara imewakaje, na wakatihuo namuona kabisa anashangaa lakini hataki kuniuliza ama kuzungumzia hili, basi akaamua tu aendelee kuivuta palepale pasipo kusogea kando.

Wakati akiendelea kuivuta tena nikanuona kijana akirejea tulipokaa kwa tahadhari tena pasipo mgeni huyu kumuona na kisha akaikata sehem ya mbele ya ile sigara iliokua ikiwaka, na akarudi tena kwa tahadhari huku moyoni nikisema leo huyu mtoto lazima nitamvunja kwa kichapo.

Basi yule mgeni wangu wakati anataka kuendelea kuvuta sigara yake, kidogo alipata mshtuko wa dhahiri kuona tena sigara yake imezimwa. Nilimuona kabisa jinsi mgeni wangu huyu alivyo changanyikiwa na kisha akaanza kuangaza huku na kule hata juu ya mti, na bila kusema neno akaniaga na wakati namsindikiza ikabidi akatae kwamba kwa kunishukuru tu yeye aende....

Sasa kesho yake nikiwa maendeo ya kibaruani nikakuta habari imesambaa kwamba Dahhhh... Kwa mzee Ushimen kuna jini pale nje kwake chini ya mti, na mimi maneno yalipo nifikia ikabidi nikanushe tu kwamba mbona hiyo siku jamaa anayosema alikuja kwangu mimi sikuwepo..??

Basi binadam kama mnavyojua wakamrudishia nduguyangu yule kwamba Mimi nimekana kwamba sikuwepi home, basi naambiwa hapo ndipo jamaa alipo changanyikiwa zaidi kwamba, yawezekana alipokuja kwangu alikaa na jini. Yaani badala ya kukasirika hua nikikumbuka nabaki kujichekea tu....[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu mpk hivi sasa unamajini mangapi..?

Waswahili husema biashara matangazo..
 
Sijawahi faham tafasiriyake mkuu, lakini ni aina ya viumbe visivyo onekana ingawa inasadikika kwamba wanaishi
Kumbe ni maviumbe hayaonekani!

Fanya hivi,mshauri huyo rafiki yako aache kuvuta masigara!

Yanarahisisha kifo
 
Dah.... kwa wale wasiojua majini
kisirani 😂😂😂🤭
Amber+Lulu+%E2%80%93+Jini+Kisirani(0).jpg
 
Back
Top Bottom