Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
YUKO WAPI MWAKYEMBE YULE WA RICHMOND?
Madaraka yana tabia moja mbaya sana hususani kwa Waafrika. Tabia hii mbaya ya madaraka ni kulevya. Madaraka ni kama Pombe tu, wengi wanashindwa kuyanywa kwa ustaarabu, wanajikuta wanakuwa ni walevi wa kupindukia wa madaraka. Viongozi wengi wanasumbuliwa na tatizo la uraibu (addiction) wa madaraka, wanahitaji kupelekwa katika vituo vya tiba (rehabilitation centre).
Nani asiyemkumbuka Mwanasheria Harrison Mwakyembe wakati akiwa nje ya Bunge? Nani asiyekumbuka namna ambavyo Mwanasheria huyu nguli alivyokuwa bega kwa bega na Marehemu Dr. Sengondo Adrian Mvungi (PhD) katika kupigania mageuzi ya Katiba, demokrasia na utawala wa Sheria? Nani ambaye angebisha kuwa hata baada ya Mvungi kuuawa Mwakyembe angevaa viatu vya Sengondo Mvungi na vikamuenea barabara. Nini kimemfika nguli huyu tajika wa Sheria ambaye usomi wake sio wa kutiliwa shaka?
Nani asiyekumbuka Mwakyembe wa Bunge la Mzee wa viwango na kasi Marehemu Spika Samwel Sitta hususani wakati wa sakata la ufisadi wa Richmond? Nani hakumbuki namna Mwakyembe alivyosimama imara na kuungana na Upinzani bila kujali chama wala itikadi kutetea maslahi mapana ya Taifa hili?
Nani alijua kuwa Waziri Mkuu mwenye mizizi na mtandao mpana wenye nguvu ndani na nje ya Bunge Edward Lowassa angeweza kutikiswa na kijana mdogo kabisa Harrison Mwakyembe?? Nani alijua kama Lowassa anaweza kudondoshwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond ambapo Mwenyekiti wa jopo la kuchunguza ufisadi huo alikuwa ni Mwanasheria nguli Harrison Mwakyembe akisaidiana na makamo Mwenyekiti Mhandisi Stella Manyanya? Nini kimemsibu shujaa huyu mtajika ambaye jina lake liliandikwa kwa wino wa dhahabu wakati wa ufisadi wa Richmond.
Yuko wapi Harrison Mwakyembe yule aliyeweza kuwatikisa vigogo wenye mizizi ya chuma katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete? Yuko wapi Mwakyembe yule aliyekuwa anaogopwa na akina Mtemi Andrew Chenge, Ngeleja, Nazir Karamagi, miongoni mwa majitu mengine mazito ndani na nje ya CCM?
Yuko wapi Mwakyembe yule ambaye Taifa bila kujali itikadi wala vyama tulisema anastahili kuwa Rais wa nchi hii au ikishindikana basi awe Waziri Mkuu?
Marehemu Samwel Sitta, Sengondo Mvungi na Deo Filikunjombe akafufuka leo akamuona Mwakyembe akiongea Bungeni amini amin nakuambia kuwa mashujaa wetu hawa wawili watapatwa na mshtuko mkubwa wa moyo na watafariki tena. Hawawezi kuamini kuwa huyu ndiye Mwakyembe wanayemfahamu.
Huyu ndiye Mwakyembe yule ambaye alidaiwa kulishwa sumu baada ya sakata la Richmond ili kumyamazisha kimya milele? Huyu ni Mwakyembe yule yule aliyechungulia kaburi na kurudishiwa uhai kwa muujiza wa Mungu? Nini kimemsibu?
Leo Mwakyembe baada ya kuwa Waziri wa Habari na bahati nzuri sana amewahi kuwa Waziri wa Sheria na Katiba Wabunge na Wananchi wanaulizia ni wapi alipo Mwanahabari nguli Azory Gwanda ambaye amepotea muda mrefu na serikali ipo kimya tu kana kwamba ni kunguru kapotea, Mwakyembe ni anawabeza na kuwapuuza kuwa kuuliza ni wapi alipo Azory ni hoja na kesi DHAIFU sana! Aisee! Mwakyembe anasema aneo ambalo Azory amepotelea ni watu wengi tu wamepotea wakiwa hapo hivyo kuendelea kumuulizia au kumtafuta Mwanahabari Azory Gwanda ni hoja na kesi DHAIFU isiyo na tija. Mwakyembe anatoa wapi hiki kibri wakati anafahamu kuwa Ben-Rabiu Wa Saanane ametoweka na serikali haina majibu, MO DEWJI alitekwa serikali haina majibu, Roma Mkatoliki alitekwa serikali haina majibu!
Leo Mwakyembe ambaye Watanzania walipigania maisha yake kwa kodi zao na maombi yao wakimuombea Mungu amnusuru shujaa huyu ili aishi aendelee kututetea anasema ni kesi DHAIFU kumtafuta binadamu wenzetu. Mwakyembe amefika mahali anaona kuna maisha yenye thamani kuliko maisha ya wengine. Kweli! Ndio maana nauliza Mwakyembe nini kimemsibu?
Hivi ingekuwa aliyepotea ni mwanaye Mwakyembe "George Mwakyembe" au binti yake leo Mwakyembe angesema kumtafuta kijana George Harrison Mwakyembe ni kesi DHAIFU isiyo na tija?
Hivi Mwakyembe anapata walau wasaa wa kutazama picha zake wakati akiwa amebabuka baada ya kulishwa kitu kinachodaiwa kuwa ni sumu wakati wa sakata la ufisadi wa Richmond? Vipi Serikali ingesema tumeshamtibu sana Mwakyembe haponi ni pesa tu inaendelea kupotea hivyo haina tija na ni UDHAIFU kuendelea kumtibu. Ungesikiaje Mwakyembe wewe?
Azory ni Mtoto wa Gwanda kama ambavyo George ni Mtoto wako leo madaraka yamekulevya unaona maisha ya Azory ni kama Mbuzi wa kafara, Ila maisha yako na ya mwanao George ni ya thamani. Kweli taaluma yako ya Sheria ndivyo inavyosema.
Leo Mwakyembe wewe ni Waziri wa Habari tena bahati nzuri ni mwana Sheria, Wabunge wanauliza ni kwa nini gazeti la Tanzanite na Jamvi la Habari linatukana, kudhalilisha, kupotosha, kutweza UTU wa watu na kufanya uchochezi lakini serikali haichukui hatua kwa mujibu wa Sheria wewe kwa kibri na dhihaka unasema ambaye amedhalilishwa na gazeti la Tanzanite au Jamvi la habari aende mahakamani. Kweli!
Hii double standards katika Sheria ni sehemu ya taaluma yako? Mbona Serikali imeyafungia magazeti ya Mwananchi, Mwana Halisi, Tanzania Daima, The Citizen miongoni mwa wengine kwa sababu mlizodai ni upotoshaji, uchochezi, udhalilishaji, nk. Kwa nini serikali haikuenda mahakamani? Kwa kuwa Tanzanite na Jamvi la habari yamejikita kuwatukana na kuwadhalilisha Viongozi wa Upinzani serikali haioni haja ya kusimamia Sheria?
Mwakyembe anaifahamu vizuri historia ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, anafahamu ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 kuwa yalichochewa sana na vyombo vya habari ambavyo serikali zilikaa kimya kwa kuwa wanaochafuliwa ni wapinzani au maadui wao.
Najua madaraka yanalevya Ila nahisi Mwakyembe amevuka kwenye ulevi wa madaraka na sasa amekuwa mraibu (addicted) wa madaraka hii ni kawaida kwa Viongozi wa Afrika.
Nimkumbushe kuwa mara baada ya Sadam Hussein wa Iraq kuangushwa, Waziri wa Habari wa Iraq alilazimika kwenda kujificha kwenye kalavati la maji machafu. Baada Dikteta uchwara Omar El Bashir wa Sudan kuangushwa Waziri wa Habari wa Sudan naye alikimbilia kwenda kujificha kwenye kalavati la maji machafu lakini wote walikamatwa. Madaraka yana mwisho? Yuko wapi Mwakyembe wa Richmond? Nini kimemsibu?
#MwagaPombe2020
I rest my case!
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
Soma