Huyu makamba vipi, eti SIM Card Tax ihamishiwe kwenye kodi ya wamiliki wa nyumba za kupangisha

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Imeandikwa na Asha Bani, TanzaniaDaima -- NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amesema badala ya kuwatoza wananchi kwenye laini za simu serikali ihamishie kodi hiyo kwa wamiliki wa nyumba wanaopangisha bila kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Makamba alisema kuwa malalamiko ya wananchi yalikuwa ya kweli na ya msingi hivyo basi serikali iweke mbadala wa tozo hizo kwa wenye nyumba za kupangisha.

Naibu waziri huyo aliongeza kuwa aliwahi kulizungumza hilo na kutoa ushauri kwa serikali na hata kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na suala hilo la kutaka wenye nyumba kulipa kodi ili ziweze​

kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kodi kwenye tozo za simu wananchi walikuwa na hoja lakini aliwaita wabunge kuwa ni wanafiki kwa kuwa walipitisha wenyewe wakiwa kwenye kamati ya bajeti lakini akashangaa kuanza kulalama bila sababu kwa kile alichokiita ni kutaka sifa kwa wananchi.

“Kwa sasa tayari vikao vitatu vimefanyika lakini pia kuna haja ya kuangalia endapo hii itatolewa kutakuwa na mbadala gani wa kufidia hicho kiasi cha sh bilioni 178 kinachohitajika ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi vijijini,” alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kikubwa ni kuganga yajayo na kuacha kukumbuka ya nyuma, kwamba wananchi wamelalamika na wamesikika na sasa maagizo aliyotoa rais wameanza kuyatekeleza.

Akijibu swali kuhusu kuongezeka kwa makato katika miamara ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu za mikononi, Makamba alisema hana uhakika nalo, lakini ni wajibu wao kuliangalia upya suala hilo.​

Source: SIM Card Tax ihamishiwe kwenye kodi ya wamiliki wa nyumba za kupangisha- - wavuti.com
 
hivi hajui kuwa watakaumia ni wapangaji na siyo mwenye nyumba!!!
 
Sawa!Safi kabisa?na shirika la nyumba la taifa nalo linahusika{NHC}.TRA Njooni mwezi ujao mchukue bukubuku kwa vyumba kumi nilivyopangisha pale uwanja wa fisi.
 
Ni majuzi tu manyumba karibia mengi yamelipiwa pesa ambazo serikali wanaziita kodi ya nyumba. Nyumba za udogo zimelipiwa tsh 2000 na zile za matofali ya saruji au ya kuchoma zimelipiwa tsh 10000..
 
hivi hajui kuwa watakaumia ni wapangaji na siyo mwenye nyumba!!!
Umoja wa wapangaji Tanzania{UWAWATA} na wao pia wataandamana kudai wenye nyumba wamepandsha kodi kwa 50% hivyo serikali iinglie kati swala hilo.Heee! Tz kazi kwelikweli?likitokahili linaingia hili,lile tunasahau tunafuata hili1
MUNGU Ibariki TANGANYIKA
 
"Kwa sasa tayari vikao vitatu vimefanyika lakini pia kuna haja ya kuangalia endapo hii itatolewa kutakuwa na mbadala gani wa kufidia hicho kiasi cha sh bilioni 178 kinachohitajika ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi vijijini," alisema.
Vijijini....
Vijijini...
Kwa jinsi serikali inavosingizia "vijiji"
Ukifika huko vijijini wanakosema deile kwenye bajeti zao, utafikiri ndo mwaka huu wameanza kutajwa.
Hizo Bil 178 ni za mtu tu na washkaji zake.

Kazi ya kusimamia makampuni ya sim kuwa na kiwango kimoja ktk kupiga sim imemshinda na ndio ipo chini ya wizara yake. Huu upumbafu mwingne sijui anautoa wp?
 
mi nafikiri ni kwasababu hawajapitia maisha ya chini, nina uhakika hawajawahi kupanga ndo maana, unajua akina makamba na watoto wao hawajawahi kuishi uswazi wakaona shida ya nyumba ilivyo.

Hajui kuwa hao hao waliogomea kodi ya simu ndo hao hao watakaoumia kwa kupanda kwa kodi ya nyumba
 
Kweli hawa wenye nyumba hawakatwi hata kodi,pango zao juu kila mwana na dalali anataka chake,n bora na wao waanze kulichangia taifa hili sasa kwa pesa wanazopata!!bravo makamba.
 
Duuu mi naona waanze kuwakata kodi mateja wote barabarani,
 
Huyu jamaa nae dizaini bendera fuata upepo..
 
Kweli hawa wenye nyumba hawakatwi hata kodi,pango zao juu kila mwana na dalali anataka chake,n bora na wao waanze kulichangia taifa hili sasa kwa pesa wanazopata!!bravo makamba.

mkuu una uhakika wenye nyumba ndo watalipa hiyo kodi?
 
kabla ya kuanza kufikiria kuanzisha kodi hizo kwanza atueleze kwanini mpaka sasa hivi hakuna chombo au mtambo unaohakiki mapato ya kampuni za simu kwa kifupi jamaa anatafuta cheap popurality
 
Ni majuzi tu manyumba karibia mengi yamelipiwa pesa ambazo serikali wanaziita kodi ya nyumba. Nyumba za udogo zimelipiwa tsh 2000 na zile za matofali ya saruji au ya kuchoma zimelipiwa tsh 10000..
Kodi anayosema Makamba ni kodi ya upangishaji/ukodishaji sio hiyo kodi inayolipwa manispaa kila mwaka kwa Kiwanja au Nyumba. Hapo unapoish kama umepanga inabidi mwenye nyumba apeleke 18% ya kodi uliyolipa kwenda TRA na electroniki risiti akupe, lol .
 
Serikali corrupt haikusanyi kodi, inakimbizana na vibiashara vya barabarani.....Mwalimu Nyerere
 
sasa wewe ulitakaje kwani na wao wwenye nyumba ni muhimu walipe tax kwani na wao wanafanya biashara ya upangishaji
Imeandikwa na Asha Bani, TanzaniaDaima -- NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amesema badala ya kuwatoza wananchi kwenye laini za simu serikali ihamishie kodi hiyo kwa wamiliki wa nyumba wanaopangisha bila kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Makamba alisema kuwa malalamiko ya wananchi yalikuwa ya kweli na ya msingi hivyo basi serikali iweke mbadala wa tozo hizo kwa wenye nyumba za kupangisha.

Naibu waziri huyo aliongeza kuwa aliwahi kulizungumza hilo na kutoa ushauri kwa serikali na hata kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na suala hilo la kutaka wenye nyumba kulipa kodi ili ziweze​

kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kodi kwenye tozo za simu wananchi walikuwa na hoja lakini aliwaita wabunge kuwa ni wanafiki kwa kuwa walipitisha wenyewe wakiwa kwenye kamati ya bajeti lakini akashangaa kuanza kulalama bila sababu kwa kile alichokiita ni kutaka sifa kwa wananchi.

"Kwa sasa tayari vikao vitatu vimefanyika lakini pia kuna haja ya kuangalia endapo hii itatolewa kutakuwa na mbadala gani wa kufidia hicho kiasi cha sh bilioni 178 kinachohitajika ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi vijijini," alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kikubwa ni kuganga yajayo na kuacha kukumbuka ya nyuma, kwamba wananchi wamelalamika na wamesikika na sasa maagizo aliyotoa rais wameanza kuyatekeleza.

Akijibu swali kuhusu kuongezeka kwa makato katika miamara ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu za mikononi, Makamba alisema hana uhakika nalo, lakini ni wajibu wao kuliangalia upya suala hilo.​

Source: SIM Card Tax ihamishiwe kwenye kodi ya wamiliki wa nyumba za kupangisha- - wavuti.com
 
sasa wewe ulitakaje kwani na wao wwenye nyumba ni muhimu walipe tax kwani na wao wanafanya biashara ya upangishaji

ladyfurahia unajua impact ya kuwatoza kodi wamiliki wa nyumba za kupangisha?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom