Huyu Malaika anayetenganisha Dunia ya Uhai na Dunia ya Wafu (Kuzimu)

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
Wasaalaam

Kipindi kile tungali wadogo ,tuliishi kwa ngano na hekaya za kutisha kutoka kwa wazee wetu , hadithi kedekede katika mjumuiko mmoja wa wajukuu na watoto kadha wa kadha, wakimsikiliza mzee mmoja aidha awe na sharafa zenye mchanganyiko wa Weusi na weupe unaoleta ukamilifu wa Rangi ya Kijivu , huku kichwani akijawa na utitiri wa nywele nyeupe , wote tukitegesha maskio kwa visasili vyake na hadithi za mizuka , vibwengo majini na misyuka yenye kuogofya.

Kwa bahati mbaya katika zama hizi za kizazi cha Sasa hilo halipo tena , mtoto asikilize hadithi kutoka kwa nani ,huyu mama yake anayefanya kazi Benki au Pale hospitali akibishana na wamama wanaojifungua, na mara nyingi mama huyu akirudi amechoka hana Hali anahitaji Mapumziko, kutokana na uchovu na Mifadhahiko ya kazi , Wale wazee wetu wenye hadithi za kale wengi wao hatunao tena. na wengine wako kule vijijini , mjukuu kumtembelea Babu yake ni nadra sana , pengine ni miaka miwili. mpaka mitatu tena watakaa wiki tatu tu na kurejea mjini .kumuona tena majaliwa ya mungu Au pengine ni siku za mazishi kabisa.

Pengine muda mwingi mtoto huyu anakuwa nyumbani ,na Dada wa kazi lakini dada huyu hana muda, muda mwingi yuko katika shuguli za ndani , ili kasoro isiwepo pale mwajiri wake atakaporejea, ...na hata akipata wasaa wa kupumzika ....atakimbilia Runinga akawatazame wakina Mkojani na Wema sepetu, angefanya nini tena,?? huwezi mlaumu hata kule kijijini alikotoka hakukuweko vitu vya namna hiyo.

Mtoto huyu wa zama hizi anakosa zile hekaya na hadithi za kale za babu zake wa kale na asili yake. ....atakuwa bize na Schooling akirudi atashika Game Padi , Maisha yanakwenda hivyo.

Ngoja nisiuzamishe ubongo katika manyanyaso ya kutafakari utangulizi wangu.

Tuje kwenye uwanja wa nyuzi yetu

Screenshot_20210610-072929.png

Charon ni moja ya histori kubwa sana Uigiriki,
Nilipata kuandika mengi yanayosisimua sana kuhusu ,Medusa, Athena ,Zeus,Pandora na Wengineo wanaofana nao.

Kama ilivyo kwa hao waliotajwa hapo juu basi Charon huyu amekuwa kama mungu mdogo au wengine wanamterm kama demon miongoni mwa malaika mademons.

Drama ya mwamba huyu inaanzia mto wa wafu , Au tuseme huko kuzimu ,ili kuwaletea afiki ya kuelewa nini tunajaribu kuzungumzia.

CHARON MWANA WA NYX

Charon
naye ni mungu wa kuzimu katika hadithi hizi za Uigiriki.

Charon alikuwa mtoto wa miungu wawili ya zamani sana huko Ugiriki ambao ni, Nyx (Usiku) na Erebus (Giza). Nyx na Erebus walikuwa miungu ya asili wa zamani sana wa Ugiriki huko.

Nyx na Erebus walikuwa na watoto wengi, na kwa hivyo huyu mungu wa kuzimu Charon alikuwa na ndugu na miungu wengi wa "giza" hapa kwa wale wapitiao hadithi zao za Uigiriki nadhani tutakuwa tunakwenda Pamoja, mfano miungu kama Nemesis (wa kisasi), Thanatos (wa kifo) na Geras (wa uzee)

Screenshot_20210610-072854.png

Kama ilivyo kwa watoto wengi wa Miungu Nyx na Erebus, Charon ilisemekana alikuwa akikaa kuzimu , na jukumu lake la umilele ni kubeba Roho za wafu ambao wameshaagana na Dunia kuzisafirisha kuelekea kwenye maisha yao ya Milele.

Inaelezwa kuwa Psychopomp (huyu ni malaika anaesafirisha Roho za wafu) angemsindikiza marehemu aliyekufa kwenye kingo za Mto Acheron, Mto wa Maumivu.

Hapa mhudumu wa eneo hili ambaye ni Charon angeichukua roho marehemu na kuvusha katika mto, ili kuuvuka mto huu unaotenganisha ,upande wa wafu na Kuzimu. Pia, ili kusafirisha ilitakiwa kulipa nauli.

Nauli ya Charon ilisemekana kuwa ni sarafu, Hakuna anayefahamu ni kiasi gani kilihitajika ila ili maiti yako isafirishwe basi lazima maiti wangewekwa sarafu kinywani mwa marehemu.

Wale maiti ambao hawangeweza kulipa Nauli kwa Charon wangerandaranda ovyo kwenye kingo za mto Acheron kwa miaka 100, na roho zao zingekuwa kama mizuka juu ya dunia zikiwatesha ndugu zao ambao walishindwa kuwafanyia Ibada hiyo ya mazishi ndugu zao.

Wale ambao wangeweza kumlipa , basi wafu, wangesafirishwa salama kwenye Acheron hadi eneo salama la ufalme huko kuzimu.
Huko Marehemu angeweza kusimama mbele ya Majaji wa Wafu, ambao wangehukumu jinsi alivyoishi. na huko maisha ya Milele.

Screenshot_20210610-073014.png

Mara nyingi husimuliwa kuwa Charon alikuwa msafiri wa kuvuka Mto Styx, ingawa hii ilikuja kubadilishwa na pia mto huo maarufu zaidi uliopatikana katika ulimwengu wa chini (kuzimu) wa Uigiriki.

Screenshot_20210610-072837.png

Mara nyingi pia Charon huwa juu ya mashua yake, ambayo anaitumia kusafirisha miili ya wafu. Hakukuwa na kitu dhaifu juu ya Charon ila inaelezwa alikuwa amejawa na nguvu nyingi sana, na kwa nguvu hizo pia alikuwa na silaha mkononi, ambayo angehakikisha kuwa hakuna mtu ambaye anamletea ujinga na hilba za namna yoyote ile.

Underworld ni kweli kweli makazi haswa ya wafu, lakini kuvuka kupitia Acheron pia ilikuwa njia kuu ambayo walio hai waliweza
kuingia katika eneo la hilo la wafu (hadesi).

Hali yoyote ya Uhai bila shaka haukupaswa kuwa katika Underworld, na Charon hakupaswa kuwasaidia, lakini kuna orodha ya Miungu na viongozi wengi waliokimbilia huko kujificha na kukwepa adhabu baada ya kuleta shida katika dunia ya kawaida hapa walimlipa Charon na kukimbilia huko kujihifadhi na wengine wenye mamlaka walivuka pasi na Malipo

Waandishi baadaye, haswa katika kipindi cha Kirumi wanapata kusema kuwa Charon aliadhibiwa kila wakati alipowaruhusu walio hai kwenda Underworld, Pia Charon alisema angeadhibiwa kwa mwaka kwa minyororo. Ikiwa marehemu katika kipindi hiki alisubiri tu kwenye kingo za Acheron.

Screenshot_20210610-072959.png

NB: Hadithi hizi hazipo kwa wale wanaomini katika Mungu mmoja so take that and Ask yourself.

SHUQRAAN🙏

DaVinci XV

View attachment 1823696

Charon ni moja ya histori kubwa sana Uigiriki,
Nilipata kuandika mengi yanayosisimua sana kuhusu ,Medusa, Athena ,Zeus,Pandora na Wengineo wanaofana nao.

Kama ilivyo kwa hao waliotajwa hapo juu basi Charon huyu amekuwa kama mungu mdogo au wengine wanamterm kama demon miongoni mwa malaika mademons.

Drama ya mwamba huyu inaanzia mto wa wafu , Au tuseme huko kuzimu ,ili kuwaletea afiki ya kuelewa nini tunajaribu kuzungumzia.

CHARON MWANA WA NYX

Charon
naye ni mungu wa kuzimu katika hadithi hizi za Uigiriki.

Charon alikuwa mtoto wa miungu wawili ya zamani sana huko Ugiriki ambao ni, Nyx (Usiku) na Erebus (Giza). Nyx na Erebus walikuwa miungu ya asili wa zamani sana wa Ugiriki huko.

Nyx na Erebus walikuwa na watoto wengi, na kwa hivyo huyu mungu wa kuzimu Charon alikuwa na ndugu na miungu wengi wa "giza" hapa kwa wale wapitiao hadithi zao za Uigiriki nadhani tutakuwa tunakwenda Pamoja, mfano miungu kama Nemesis (wa kisasi), Thanatos (wa kifo) na Geras (wa uzee)

View attachment 1823698

Kama ilivyo kwa watoto wengi wa Miungu Nyx na Erebus, Charon ilisemekana alikuwa akikaa kuzimu , na jukumu lake la umilele ni kubeba Roho za wafu ambao wameshaagana na Dunia kuzisafirisha kuelekea kwenye maisha yao ya Milele.

Inaelezwa kuwa Psychopomp (huyu ni malaika anaesafirisha Roho za wafu) angemsindikiza marehemu aliyekufa kwenye kingo za Mto Acheron, Mto wa Maumivu.

Hapa mhudumu wa eneo hili ambaye ni Charon angeichukua roho marehemu na kuvusha katika mto, ili kuuvuka mto huu unaotenganisha ,upande wa wafu na Kuzimu. Pia, ili kusafirisha ilitakiwa kulipa nauli.

Nauli ya Charon ilisemekana kuwa ni sarafu, Hakuna anayefahamu ni kiasi gani kilihitajika ila ili maiti yako isafirishwe basi lazima maiti wangewekwa sarafu kinywani mwa marehemu.

Wale maiti ambao hawangeweza kulipa Nauli kwa Charon wangerandaranda ovyo kwenye kingo za mto Acheron kwa miaka 100, na roho zao zingekuwa kama mizuka juu ya dunia zikiwatesha ndugu zao ambao walishindwa kuwafanyia Ibada hiyo ya mazishi ndugu zao.

Wale ambao wangeweza kumlipa , basi wafu, wangesafirishwa salama kwenye Acheron hadi eneo salama la ufalme huko kuzimu.
Huko Marehemu angeweza kusimama mbele ya Majaji wa Wafu, ambao wangehukumu jinsi alivyoishi. na huko maisha ya Milele.

View attachment 1823700
Mara nyingi husimuliwa kuwa Charon alikuwa msafiri wa kuvuka Mto Styx, ingawa hii ilikuja kubadilishwa na pia mto huo maarufu zaidi uliopatikana katika ulimwengu wa chini (kuzimu) wa Uigiriki.

View attachment 1823701

Mara nyingi pia Charon huwa juu ya mashua yake, ambayo anaitumia kusafirisha miili ya wafu. Hakukuwa na kitu dhaifu juu ya Charon ila inaelezwa alikuwa amejawa na nguvu nyingi sana, na kwa nguvu hizo pia alikuwa na silaha mkononi, ambayo angehakikisha kuwa hakuna mtu ambaye anamletea ujinga na hilba za namna yoyote ile.

Underworld ni kweli kweli makazi haswa ya wafu, lakini kuvuka kupitia Acheron pia ilikuwa njia kuu ambayo walio hai waliweza
kuingia katika eneo la hilo la wafu (hadesi).

Hali yoyote ya Uhai bila shaka haukupaswa kuwa katika Underworld, na Charon hakupaswa kuwasaidia, lakini kuna orodha ya Miungu na viongozi wengi waliokimbilia huko kujificha na kukwepa adhabu baada ya kuleta shida katika dunia ya kawaida hapa walimlipa Charon na kukimbilia huko kujihifadhi na wengine wenye mamlaka walivuka pasi na Malipo

Waandishi baadaye, haswa katika kipindi cha Kirumi wanapata kusema kuwa Charon aliadhibiwa kila wakati alipowaruhusu walio hai kwenda Underworld, Pia Charon alisema angeadhibiwa kwa mwaka kwa minyororo. Ikiwa marehemu katika kipindi hiki alisubiri tu kwenye kingo za Acheron.

View attachment 1823704

NB: Hadithi hizi hazipo kwa wale wanaomini katika Mungu mmoja so take that and Ask yourself.

SHUQRAAN[emoji120]

DaVinci XV

Hades ni mungu wa Kigiriki anayetawala underworld
 
Nime icheki kwenye movie ya clash of Titans ndo imeelezea kuhusu hii kitu.
 
haya mahadithi nadhani ndio yanafanya wazungu wengi kupunguza mwamko na hizi dini/imani

ukiyasoma yana ingia akilini kuliko vitabu vya dini,vyenyewe vinaacha mswali mengi sana.

mfano hii ya kusema shetani ni Mungu wa giza,hizi hadithi zimeenda mbali zaidi na kusema huyu kiasili ni ndugu(sibling) wa Mungu zeus ambaye ndiye wa anga tunayemwabudu,ndio maana labda alishindwa kumwadhibu mapema au kumdhibiti maana labda wanatoshana nguvu au wanapishan kidogo tu.
 
Hayo ma demon tusiyataje taje huwa yapo na huleta mikosi mbalimbali katika maisha kwa mfano chronos na kadhalika
 
Back
Top Bottom