Huyu Mbunge wa Kenya Anatrend kwenye mitandao.

Kwa hakika kwenye yale mambo yetu:



Tupiganie reforms kama hizi.

Kwanini watu wasipige kura kwa vitambulisho vya uraia?

Kwanini daftari la mpiga kura ndiyo liwe pekee?

Ubaguzi huu ni kwa niaba ya nani?

Tlaatlaah, Lucas Mwashambwa, Paskali mama na chama mboga mboga wafikiwe kuwataka (si kuwaomba) kuwapa watanzania haki zao, uchaguzi wanazoendelea kuzikalia kidhalimu.

imhotep na wale wengine au nasema uongo?
 
kuanzia mwaka ujao wa fedha tukijaaliwa, utaratibu wa kuandikisha na kuwapatia waTanzania vitambilisho vya Taifa utakua ni pale mtu atakapozaliwa tu na anakabidhiwa na kitambulisho chake cha taifa.

Suala la upigaji kura na vitambilisho vya kupigia kura, lina sifa na vigezo tofauti vya kisheria na kwahivyo ni tofauti kabisa na suala la utaifa na vitambilisho vya Taifa.

hivyo basi haviwezi kwenda sambamba na wala havihusiani πŸ’
 

Vitambulisho vya uraia vinathibitisha uraia, umri na taarifa zote binafsi za mtu ambavyo ndiyo vigezo vya mpiga kura.

Labda ndugu kipi ambacho kinapungua au kuzidi kwenye kitambulisho cha uraia kuathiri matumizi yake kwenye kuwa kuwa pia kupigia kura?
 
zingatia maelezo ya msingi gentleman,
vitambilisho vya kiraia ni maalumu kwa utambulisho wa uraia ukaazi wa kila mTanzania pekee na si vinginevyo.

ukihama makazi ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania huna haja ya kubadili ukaazi wako tofauti na cha mpiga kura Lazima kubadili kituo cha kupigia kura πŸ’
 



Kwenye madai yetu, na hilo la NIDA kuwa ndicho pekee kigezo cha kupigia kura nalo limo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…