Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,443
- 3,480
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ahudhuria Dua Maalum ya Hitima ya Marehemu Mzee Omary Rashidi Mchengerwa
ZANZIBAR – Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, ameungana na Wazanzibari wengine katika Dua maalum ya hitima kwa ajili ya Alhaji Marehemu Mzee Omary Rashidi Mchengerwa, Baba mzazi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Dua hiyo maalum imefanyika leo, Februari 27, 2025, katika Kiwanja cha Kilimani kwa Msolopa, Zanzibar, na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali ya Visiwa hivyo.
Marehemu Alhaji Mzee Omary Rashidi Mchengerwa alikuwa muumini aliyependelea sana kuswali katika Msikiti wa Kilimani kwa zaidi ya miaka 20, tangu mwaka 1990, na alikuwa akiheshimika kwa mchango wake katika jamii.
Ibada hiyo ya hitima imekuwa ni fursa kwa ndugu, jamaa na marafiki kumuombea dua na kumkumbuka marehemu kwa mema yake, huku viongozi wa serikali na wananchi kwa ujumla wakitoa pole kwa familia ya Mchengerwa.