Huyu mhasibu hakuangalia vizuri zile movie zinazofundisha

Huyu mhasibu hakuangalia vizuri zile movie zinazofundisha

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827


MHASIBU wa Kampuni ya Your Home Choice ya Keko, Dar es Salaam, Deodatus Luhela (35), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na kujeruhiwa na majambazi kisha kuporwa Sh. milioni 60 za mwajiri wake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi (ACP) Jumanne Muliro.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi (ACP) Jumanne Muliro, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa kituo kidogo cha polisi cha Gongo la Mboto na baadaye kufungua jalada katika Kituo cha Polisi Chang’ombe akidai kufanyiwa kitendo hicho.

Muliro alisema Novemba 14, mwaka huu, mtuhumiwa huyo katika taarifa alizotoa polisi, alidai kuwa majambazi walimjeruhi na kumpora Sh. milioni 60 alizokuwa ametumwa na mwajiri wake kuzichukua katika benki ya CRDB tawi la TAZARA.

Alisema Luhela alidai kuwa siku hiyo, saa 3:30 asubuhi, alikamatwa na majambazi wawili waliokuwa na gari jeusi baada ya kumtishia kwa silaha na baadaye akaingizwa kwenye gari.

Kwa mujibu wa Muliro, mtuhumiwa alidai kuwa majambazi hao walimjeruhi mkono wa kushoto na shavuni na hatimaye kumpora fedha zote alizokuwa nazo.


“Alidai kuwa baada ya tukio hilo alitupwa maeneo ya Gongo la Mboto njia panda ya Pugu na Mbezi, akajikongoja hadi kituo cha Polisi ambako alipewa PF. 3 (Fomu namba tatu ya polisi) kwa ajili ya matibabu. Baadaye mtuhumiwa huyo alifungua kesi ya unyang’anyi na kuporwa Sh. milioni 60 katika kituo cha Polisi Chang’ombe,” alisema Muliro.

Baada ya taarifa hizo, Muliro alisema polisi walimhoji kwa kina na kubaini kuwa taarifa hizo zilikuwa za uongo.

Alisema ilipofika Novemba 15, saa 8:00 mchana, mtuhumiwa aliwaongoza askari hadi Chanika Kitunguu, jijini Dar es Salaam, alikokuwa ameficha fedha hizo
 
Huyo muhasibu wakati anaenda bank hakupelekwa na gari ya ofisi yenye dereva wa kampuni.

Hiyo kampuni nayo inafanya mambo kilocal sana
 
Itakuwa bosi wake aliwapandia dau polisi, wafanye wanaloweza, mpaka aeleze alipoficha hela...
Kama hakukalia chupa huyu...
 
Huyo mhasibu apewe mume huko jela nanyi huku uraiani chukueni mkewe hakuna wa kumlea/kumtunza.
Kazi ni kwenu.
 
Huyu mhasibu zuzu sana
Mimi nikisikia MTU kaua ,kalawiti au kubaka kuiba pesa za umma ndio nachukia.........
 
Mwanaume kapata ajali katika utafutaji, ni shujaa.
At least amejaribu kuchukua hizo pesa (japo kwa mbinu za kiboya) na kuona hatma yake kuliko angeishi na majuto ya kutojaribu na kuhisi labda angefanikiwa.
 
Nipo Babu Asprin mimi zaidi, hata sikuoni kule watoto wengi...
Niambie uliko niweke timu 😀😀😀
Mpaka mitihani ya form four iishe tutakoma.

Nipo bhana. Kama usingeniblock ningeshakufuata PM.

Kwanini uliniblock lakini wakati sijawahi kukukosea?
 
Back
Top Bottom