Huyu mkaka mbona simuelewi??? nisaidieni mawazo wanajf

Hadithi yako ni nzuri sana...ila hapo mwishoni kwenye kuhudumia ndio umeharibu!
 
Duh,

Kama wake watarajiwa wenyewe ndio hawa tutaoa kweli?

Unguja tabia hii ya mwanamke kukujua tu mara anataka kukufanya ATM inaitwa "Hashuo la Mkunguzuo"

Kama wanawake wenyewe ndo wamebaki wa aina hii, basi mi hata huo mpango wenyewe wa kuoa mi basi nimighairi somo.
 
Unguja tabia hii ya mwanamke kukujua tu mara anataka kukufanya ATM inaitwa "Hashuo la Mkunguzuo"

Duh! Hili zaidi ya la Mkunguzuo. Yaani mtu anapima mapenzi kwa huduma kiasi gani amepata kabla hata hawajajuana?!
 
Sawa we si kiwete lakini kwa nini unatanguliza pesa kuliko mapenzi ya kweli? Usiweke pesa mbele, kama nia yako ni kusoma mueleze hilo swala uone atakusaidiaje!

mimi si kiwete nashkuru ila nilimueleza historia ya maisha yangu na zaidi nahitaji kusoma tangu afariki baba nimekosa msaada wa kifamilia ila ukweli baada ya kumuona nilimpenda kweli lakini sasa ananirudisha nyuma
 
Amina usipime upendo kwa pesa!
Ni bora ukakaaa na shida zako kuliko kudanganywa, angalia sana ukute naye ana kupima!



naisi hamnielewi kabsaaaaa!!! usiku mwema wapendwa
 
kwa maelezo yako, wewe pamoja na huyo kijana wote matatizo. Na wewe ndiyo ndiyo mwenye matatizo makubwa sana! Na kwa response yako kwa huyo kijana mama yako ahesabu hasara kwako.
 
Huyo mzinguaji njoo kwangu nikuhudumie ipasavyo. Mi ndo nakupenda kweli alafu nna hela. Nielekeze kwenu nije kuongea na mama yako.
 
Kwa haraka zako hizo usitudanganye, ange kuja na gia ya pesa ange kuonja mapema sana.

Ushukuru umekuja jamvi lisilo kosa cha kushauri na jua umejifunza na utabana na hauta harakisha kama ulivyo kuwa umepanga.

Kama una shida si umwambie saa nyingine mtu ana ogopa kutoa pesa kwa kuhofia we unaweza ukadhani amekuja na gia hiyo kumbe ana kupenda.

Tafakari.

 
Amina mi nimekuelewa,nahisi sana sasa nisikilize.
Mapenzi hayana kanuni ama njia flan sahihi ktk kuyafikia.Mtu aweza onana na mwenza wake mahala popote na katika mazingira yeyote,kinachoangaliwa ni je huyo unayeonana nae anakidhi haja ya moyo wako(ktk mapenzi) na pia ana mtazamo chanya katika kutimiza ukitakacho?(iwe ndoa ama kuishi tu kama mke na mume ama vyovyote).Usiangalie wala usisikilize polojo za watu upande wa tatu katika kuamua.Ukipata mume bora ni wewe na familia yako ndo itanufaika na kinyume chake.
Note:
Inabidi uishughulishe sana akili yako ktk kumpima na kupata majibu yatakayoridhisha chemistry yenu.
 
asanteni kwa mchango wenu, naamini sitofanya tena makosa mwenzenu sijakomaa katika masuala ya mapenzi huu ndio mwanzo wangu kuamua kuwa na uhusiano, hata hivyo nawashkuru nitajifunza kutokana na makosa
 
Hebu tuwe serious kidogo,unawezaje kumkaribisha nyumbani mtu ambaye hamjawahi kuonana,pili unawezaje kumpa simu mama yako mzazi aongee na mtu usie na mahusiano nae?Pia huyo jamaa anatangazaje ndoa wakati hajajua msimamo wako?Na wewe unaonekana una tamaa sana,unataka visenti vya vocha mapema yote hii.Kuwa serious unapotaka kuwa kwenye mahusiano ambayo baadae yatazaa ndoa.
 
aisee, haka kambinu ka wrong number ni kama ka kihuni kihuni vile but surprisingly kumbe unaweza ukakatumia kujipatia binti wa kumega kiulaini kama siyo wa 'kuwowa'
 
Ngoja leo niishie kucheka tu......................LOL
 
asanteni kwa mchango wenu, naamini sitofanya tena makosa mwenzenu sijakomaa katika masuala ya mapenzi huu ndio mwanzo wangu kuamua kuwa na uhusiano, hata hivyo nawashkuru nitajifunza kutokana na makosa

Sitaki kuamini kuwa ulikuwa 'serious'..
Kama kweli ulikuwa siriaz basi umejifunza..
I bet this story is fictious!
 
Mie nimemuelewa sana uyu binti...ila nadhani wachache sana wamemuelewa.
 
Sasa ngoja nikufunze we dada pamoja na wasichana wenzako, Wanaume kwa sasa tupo kwenye mgomo wa kuoa mpaka pale mtakapo jirekebisha hiyo tabia yenu ya kuWa OMBAOMBA, mtu unakazi ya kukuingizia kipato, hicho kidogo ukipatacho kitumie vizuri kutatua shida zako na sio kumtegemea mwanaume. KWANI KABLA SIJAJUANA NA WEWE ULIKUWA HAUNA SHIDA? KWANINI BAADA YA KUANZA UHUSIANO WETU NDO SHIDA ZINAKUANDAMA? BASI PENGINE MIMI NINAKULETEA NUKSI KTK MAISHA YAKO, HIVYO NI BORA TUACHANE ILI SHIDA ZAKO ZIISHE.

NYIE WASICHANA MMEJIJENGEA KASUMBA KWAMBA MTU AKISHAZALIWA MWANAUME BASI PESA ANAZALIWANAZO HIVYO MNAMGEUZA ATM.

NDO MAANA KWA KULIGUNDUA HILO WANAUME TUMEGOMA KUOA BADALA YAKE TUNAWAMEGA NA KUWAACHA.
 
mapenzi ya kweli yanapimwa mnapokuwa ndani ya uhusiano huwezi kupima mapenzi ya kweli ukiwa nje ya uhusiano,na kuhusu kukupa vijisenti unaonekana ww ndo huna mapenzi ya kweli kwan unaonekana bila vijisent hakuna mapenzi....kuhusu huyo jamaa inaonekana alikuwa anakufaham hapo kabla na alivutiwa na wewe ila tatizo ilikuwa atakupataje, baada ya kupata namba zako ikabidi afanye kweli kwan kwa akili ya kawaida n vigumu mtu hakufaham anakuja kujitambulisha kwenu na kutangaza ndoa ......mfikirie huyo ni wa ukweli.....ni ushauri tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…