Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Hahahaha Nyani Ngabu, sijazisahau comment zako,
Kwenye ile sred moja jamaa alileta hapa "Nani kama Baba vs Nani kama Mama"
Post zako zilinifanya nitafakari mara ya pili kama na mimi nampenda mwanangu kama wewe, niliona kama unanifunika!
Ila kwa hii naona nimetoa droo.........!
Mbona wengi mnammwagia sifa kama vile yeye ndiye anayemlea mwanaye au mimi sielewi maana ya kulea. Mimi nilivyomuelewa ni kuwa anampenda sana mwanaye (Hapa anastahili hongera zake za kumwaga) lakini amesema wazi kuwa mwanaye analelewa na mama yake kwa kushirikiana na dada yake (ambao ni bibi na shangazi wa mtoto respectively).
Kuna wanaume (single parents) wanaolea kwa maana ya kuwabadilisha watoto nepi na kuwalisha. Na nimesema hivyo baada ya kuona sifa kibao zenye kuashiria kuwa jamaa ni single parent kwa hiyo anakaa na mtoto na ndiye mwenye kudili na ishu zote za mtoto on the contrary kumbe mwenye kuhangaika na mtoto ni bibi. Halafu kama kulea kunazungumzwa kwa maana ya kutafuta msosi hicho ni kitu cha kawaida sana kwa baba hapa Bongo na duniani kwa ujumla au we unaishi sayari gani???Kulea kuna maana gani?!Yeye anashinda kazini kumtafutia chakula nduguze wanashinda nae kumpa chakula alichompa!!Nini tena unataka ili aonekane kweli kalea?!
Kuna wanaume (single parents) wanaolea kwa maana ya kuwabadilisha watoto nepi na kuwalisha. Na nimesema hivyo baada ya kuona sifa kibao zenye kuashiria kuwa jamaa ni single parent kwa hiyo anakaa na mtoto na ndiye mwenye kudili na ishu zote za mtoto on the contrary kumbe mwenye kuhangaika na mtoto ni bibi. Halafu kama kulea kunazungumzwa kwa maana ya kutafuta msosi hicho ni kitu cha kawaida sana kwa baba hapa Bongo na duniani kwa ujumla au we unaishi sayari gani???
Mbona wengi mnammwagia sifa kama vile yeye ndiye anayemlea mwanaye au mimi sielewi maana ya kulea. Mimi nilivyomuelewa ni kuwa anampenda sana mwanaye (Hapa anastahili hongera zake za kumwaga) lakini amesema wazi kuwa mwanaye analelewa na mama yake kwa kushirikiana na dada yake (ambao ni bibi na shangazi wa mtoto respectively).
Unajuaje hua habadilishi?!Unachoweza kugundua kwenye maelezo yake ni kwamba tu nduguze wako na mtoto muda mwingi na sio kwamba yeye hahusiki kwenye malezi moja kwa moja!!!Acha mwenzio apate sifa maana hata kama sio yeye anaebadilusha nepi kitendo cha kumpokea...kumpenda na kuhakikisha anakua na maisha mazuri kadri ya uwezo wake kinatosha kabisa kumtofautisha na wengi wenu!!
Jamani Rose!
Hapo kwenye red, sio kweli kabisa hata kidogo.
Huyo mwanamke ni pasua kichwa mbaya, mtata yaani havumiliki, ndio hatukuweza ku-work out our thing!
Ahsante sana,
Sherehe ni hapo hom tu na Bibi yake na mashosti zake, pia nitampeleka kupiga picha Mayfair.
Karibu sana 1980
Hii wala sio nzuri nilikuwa najaribu kuifanya iwe fupi sana,
Ili nisimkere Lizzy, matokeo yake nimeacha vitu vingi sana!
Anyway, ahsante sana kama umeipenda na kwa kunitia moyo.
Huyu Malaika yupo hapa, ni mzuri sana jamani zaidi ya Mamake,
Ninaraha sana mwenzio.
Karibu leo jioni kwa kuchezea nae keki!
Kwa uweza wa Mungu, nitafika naye mbali..
Ndo Life bro, single parenting ni kitu cha kawaida this day, join the club! and to your mum umpe shukrani sana, kwa vile ndo anaelplay role kubwa ya kumlea baby girl wako.
To your angel, I wish her a HAPPY Birhtday on this special day and pray that she grows up fearing God :A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose:May she grow to blow thousand candles!
Hapo nimekusoma bibie, ukweli ni kwamba siwezi kujua kama anafanya hayo au hafanyi. Nimetoa maoni kulingana na jinsi nilivyomuelewa mtoa mada. Hapo kwenye bluu If I may ask wewe umejuaje kuwa ni wengi wetu?? (Of coz naweza kuwa mmoja wa wasiojali, lakini unajuaje kuwa ni wengi wetu?)Unajuaje hua habadilishi?!Unachoweza kugundua kwenye maelezo yake ni kwamba tu nduguze wako na mtoto muda mwingi na sio kwamba yeye hahusiki kwenye malezi moja kwa moja!!!Acha mwenzio apate sifa maana hata kama sio yeye anaebadilusha nepi kitendo cha kumpokea...kumpenda na kuhakikisha anakua na maisha mazuri kadri ya uwezo wake kinatosha kabisa kumtofautisha na wengi wenu!!
No need of being sarcastic. My response is based on what you wrote Sir.Da Womanizer!
Thanks kwa post yako na uelewa wako "zaidi" ya wengine.
Leo ni siku ya kuzaliwa binti yangu wa pekee (mpaka sasa) mpendwa sana!
Kwa mpaka sasa katika maisha yangu, huyu kiumbe ndio kitu kikubwa sana cha mafanikio yangu, na ndio sababu pekee inayonifanya napambana na ndio msingi wa furaha na mafanikio mengine.
Anatimiza miaka mitatu (3), nipo mimi na yeye tu!
Ilianza hivi.....!
Miaka minne iliyopita.
Kuna maeneo hapa mjini dar, unaweza kupata muono wa bahari ya hindi vizuri sana, hapo ndio utatambua utamu na uzuri wa bahari hiyo vilevile maisha.
Golden Tulip Hotel ni miongoni mwa maeneo hayo, najua yapo mengi na wewe unayajua!
Ilikuwa ni ratiba ya mimi na vijana wenzangu wa uswazi, kwamba kila mwisho wa mwezi tunachagua kiwanja kimoja ambapo tunaenda kubadili mandhari (kusafisha macho)
Wakati tupo hapa, eneo la "Maasai pub" stori za hapa na pale huku tuk-enjoy mawimbi yanavyopiga.... haikuchukua mda mwingi kabla sijajua kuwa huo muonekano wa bahari ya hindi na uzuri wake havikuwa na maana tena mbele ya huyu binti aliyepita hapa mbele yetu mda si mrefu.
Ni cashier. Toka nilivyomuona, akili ikawa ishanihama wala sikutaka kupoteza tena muda na kushangaa uzuri wa-view ya bahari ya hindi.
Wakati tunaondoka, nilimpitia pale counter nikamuuliza kama anaujua wimbo wa "All 4 One" unaitwa "As beatiful as You"
Akasema anaujua! Nikamwambia walimtungia yeye...... akacheka, nikachukua namba yake ya simu, mahusiano yakaanza.
Nyuma ya msichana mzuri sana, kuna tabia usiyoitarajia na itakushangaza (nzuri au mbaya)
Ilichukua miezi miwili nikawa nje ya Dar, then akawa ana mimba ya "Malaika"
Kwa bahati mbaya sana, mahusiano hayakudumu (stori nyingine) ila tulichoumba kilidumu.
Akajifungua "Baby girl".... Kabinti kangu ka kike my first born, raha sana!
Sababu sikuwa dar, hivyo baada ya kumuona tu nilirudi huko na mawasiliano ya mara kwa mara pia nilimuunganisha na familia yangu.
Baada ya miezi 6 ya umri wa mtoto, sikuamini nilivyomkuta mwanangu.... mtoto kama katoka Somalia ati ndio "kabemendwa" hivyo. Na alikuwa kishamuachisha ziwa.
Basi bibi yake hapa (Mama yangu) akasema inabidi mtoto abaki naye ili amshughurikie LISHE.
Inaonekana hiyo ndio ilikuwa ahueni ya huyo "shosti" maana toka siku hiyo binti (Mama mtoto) hadi leo hii wala hajatia pua yake hapa! Kamuacha mtoto.
Leo anatimiza miaka 3.
Mtoto lazima awe na mtu wa kumuita Mama, kadiri anavyokuwa shangazi yake mkubwa (dada yangu) ndio amemchagua kama Mama yake.
Tumeamua kumuacha tu aendelee hivyo sababu kwake aunt ndio anaziba pengo la Mama kimalezi, japo anachanganya na sisi tunavyomuita Bibi yake (Mama yetu) Mama, so na yeye anamwitaga Mama kwa kukosea.
Kiukweli sitamani Mama yake arudi kwa mda huu sababu nadhani itamchangnya zaidi mwanangu.
Nachukua wasaha huu kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa, Mungu ambariki sana na amzidishie hekima, akili na azidi kuwa mtoto mzuri.
Sanasana Mungu awabariki wakina Baba wote. (Kwa niaba yangu binafsi)
Pia awabariki wakina Mama wote (kwa niaba ya bibi yake na shangazi zake)
Mungu awabriki watoto wote wa Tanzania
Lizzy, heshima zako nyingi sana!
Kule kwenye uzi wa "Asha D"
Nimekuita mnoko lakini kwa kumanisha kuwa unaquality zote za uongozi.
Nadhani kitengo cha kusimamia nidhamu kinakufaa sana mtu wangu.
Naona hapa unamuweka sawa "Mwanajamii" mwenzetu
Nakukubali sana Lizzy.
Kuna wanaume (single parents) wanaolea kwa maana ya kuwabadilisha watoto nepi na kuwalisha. Na nimesema hivyo baada ya kuona sifa kibao zenye kuashiria kuwa jamaa ni single parent kwa hiyo anakaa na mtoto na ndiye mwenye kudili na ishu zote za mtoto on the contrary kumbe mwenye kuhangaika na mtoto ni bibi. Halafu kama kulea kunazungumzwa kwa maana ya kutafuta msosi hicho ni kitu cha kawaida sana kwa baba hapa Bongo na duniani kwa ujumla au we unaishi sayari gani???
Hapo nimekusoma bibie, ukweli ni kwamba siwezi kujua kama anafanya hayo au hafanyi. Nimetoa maoni kulingana na jinsi nilivyomuelewa mtoa mada. Hapo kwenye bluu If I may ask wewe umejuaje kuwa ni wengi wetu?? (Of coz naweza kuwa mmoja wa wasiojali, lakini unajuaje kuwa ni wengi wetu?)
Wow...asante sana JG...!
Kumbe unoko sio sifa mbaya afterall!!
Huku sioni kitufe cha "like" wala "thanks"
Nahisi zimeniishia hadi.
Viongozi wazuri wote lazima waitwe wanoko.
JeyKey sio mnoko ndio maana goma linamshinda......