Huyu mwanaume ana makosa?

Dena Amsi

R I P
Joined
Aug 17, 2010
Posts
13,080
Reaction score
4,273
Ni Baba wa watoto wanne wana ndoa nzuri tu. Imetokea shida ndani Mama kachukua mkopo Benki mara ya kwanza bila Mumewe kujua alikopeleka pesa anajua yeye akashindwa kulipa Benki wakaja wakabeba kila kitu mume kurudi kawa mkali kabembelezwa kakubali wakaanza upya, Mama kabadili Benk the same story wakabeba kila kitu, leo ni mara ya tatu wakaja mchana wa leo wamebeba kila kitu km kawaida kumbuka hii nayo ni Bank tofauti mzee kurudi kukuta yale yale ya kusafishiwa nyumba kamtimua mkewe yuko anaomba msaada plus msamaha arudishwe. Mie nauliza huyu Baba ana makosa kwa hili kweli? Kwangu binafsi naona yuko right....

Kwa kweli hata mie naona hivo mara tatu unalaza mumeo chini chochote mie nilikuwa sijawahi ona benk wanavofilisi leo nimeona yaana watu wamehama vile? Inauma bana kha?

Huyo baba kweli anampenda mke wake tena mapenzi ya dhati....

huyo dada hata angekua mdogo wangu ningemkaribisha nyumbani kwa mikono miwili. Hampendi mumewe, hamueshimu, hamshirikishi, hajaona thamani ya huyo mume! vipi anataka kumuua baba wa watu wakati kuna ladies akili zimetulia na wanatafuta waume???

nyumba ukuti wa makunga,tusimuhukumu hatujui ya chini ya zulia.

Well said Baby Gal..

Mwanamke mwenye HEKIMA kweli kweli amejenga nyumba yake,lakini aliye MPUMBAVU huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.(methali 14:1)

Kweli kabisa huyu kaibomoa kwa mikono yake mwenyewe

Dada DA kuna usemi unasema kuwa kutenda kosa sio kosa ila kurudia kosa ndo kosa kwa hiyo yeye a do the needful she must pack and go hampendi mume wake.

Reactions: BAK
Dada DA kuna usemi unasema kuwa kutenda kosa sio kosa ila kurudia kosa ndo kosa kwa hiyo yeye a do the needful she must pack and go hampendi mume wake.

Kabisa unayosema ni kweli kapewa mizigo anatusumbua majirani hapa. Off topic nimekumic wewe ujue

Kabisa unayosema ni kweli kapewa mizigo anatusumbua majirani hapa. Off topic nimekumic wewe ujue
Yaani huyo Mama basi tu ni kama mtu anaekula nakushiba sana mpaka anatapikia sahani uliolia chakula. Nipo dear unajua hichi kijiji kikubwa ndo maana huwa tunapishana humu humu, sore ofu topiki.

Naamini HUYO BABA na yeye ni part ya tatizo,na yaelekea kama hiyo nyumba yao hakuna mawasiliano kati ya baba na mama.Lilipotokea mara ya kwanza huyo baba alitakiwa anajaribu kuwa karibu na huyo mama washauriane, Yawezekana mama ana nia nzuri ila kukosekana msaada wa mawazo wa huyo baba ndo kunachangia kushindwa kurudisha mkopo

Kuna watu wana bahati ya kupata wanaume wazuri jamani....he he he he, sioni kosa la huyo baba,Mungu ampe nguvu manake hayo maumivu ni makubwa kwake....!!!

kitendo cha kufanya kitu bila kumtaarifu mumewe tayari ni kosa, achilia mbali kumfilisi mumewe na familia yake....
hamna mswalie mtume hapo, aende huko alipowekeza....mshxhsh

Hili nalo linawezekana...

kitendo cha kufanya kitu bila kumtaarifu mumewe tayari ni kosa, achilia mbali kumfilisi mumewe na familia yake....

hamna mswalie mtume hapo, aende huko alipowekeza....mshxhsh

Kabisa kwa kweli

Kha! duniani kuna mambo...kosa la kwanza lingesamehewa,la pili ingebidi baba atake action na pia awe muangalifu kwa mkewe...hili la tatu ni red card tu!
lakini pia huyo mzee hr should recheck himself mapungufu yake,huenda anakosa mawasiliano na mkewe ama kuna wajibu hatekelezi.

Hakuna kumtimua mke. Ndo mzigo wenyewe huo na huyo mume aubebe. Kwani alivyokuwa anakubali apizo bila shuruta alidhania the negative side haitakuja? Anyway let me think a bit.....mhh mkopo bank? Dhamana ni household furniture etc? Hiyo bank inayokopesha iko wapi mazee? @DA fuatilia hiyo bank utujulishe! Lol love u JF

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…