Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye katika eneo la Kiwalala katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, amefunga mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoani Lindi na kuwataka Wananchi wajitokeze kwa wingi kesho kupiga kura huku akionesha kuchukizwa na manenomaneno ya ugomvi ndani ya CCM.