Tanzania inatafuta Rais bora zaidi ya wote kwa muhula wa 2030-40, Je vyama vyetu vya Siasa vitatupa wagombea tunaowataka sisi au kinyume chake?
====
1. Rais ajae lazima awe ni mtu ambae ukiitazama staili yake ya maisha anayoishi ukihusianisha na hali na umasikini wa nchi yetu utakubaliana na Mimi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030 Watanzania watataka rais wa kupambana na rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya Fedha za umma hili halina ubishi kwa walio wengi.
2. Rais ajae lazima awe Mbabe, Watanzania watataka rais mbabe lakini awe chini kidogo ya Hayati Rais Magufuli na juu kidogo ya Hayati Rais Benjamini Mkapa ili kudhibiti uzembe na ugoigoi wa wafanyakazi wa Serikali na idara zake zote.
3. Rais ajae watanzania wataona sio sahihi rais atoke tena Zanzibari baada ya huyu kutokana na utamaduni wa kuachiana kila baada ya miaka 10 ya Uongozi au kupewa Unaibu wa Rais.
4. Rais ajae zaidi sana watanzania wataona sio sahihi kuwa na rais mwanamke mfululizo kwakuwa bado mfumo dume upo na unanguvu hata kama hauonekani.
5. Rais ajaye hatokuwa chaguo la Rais Samia Suluhu Hassan lakini pia hatokuwa tishio la Mstaafu Samia Suluhu Hassan kama ilivyo kawaida miaka yote na Kwa Marais wote waliotutangulia.
6. Rais ajaye atakuwa ni mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja na kueleweka vema kwa kada ya Gen z hivyo mdahahalo wa wagombea Urais kwa Uchaguzi Mkuu ujao wa 2030 haukwepeki ( inevitable )
7. Rais ajae atakuwa ni mkristu kwa desturi ya kuachiana wakristo na Waisilamu na huenda akatoka Kanisa Catholic kama kawaida kwani ndio taasisi yenye kundi kubwa na lenye ushawishi zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
8. Rais ajae atakuwa ni rais mwenye misimamo ya wastani kwa sababu misimamo ya Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli Rais wa awamu ya Tano pamoja na mazuri yake, bado madhara ya kuwa mtata yatachukua muda kusahaulika kwa wengi.
9. Rais ajae atakuwa mwenye sifa nyingi za Hayati Dkt Benjamini Mkapa Rais wa awamu ya tatu kuliko sifa za wengi waliomtangulia kwani ni Mkapa ndio ameanzisha karibu Kila taasisi unayoifahamu hapa nchini pamoja na mifumo mingi ya kiuongozi na kiutawala.
10. Rais wa Saba ingawa atakuwa na sifa nyingi za Hayati Dkt Benjamini Mkapa lakini atakuwa na sifa za ziada za kukubalika kwa Umma, sifa ambayo Dkt Benjamini Mkapa na Mzee Mwinyi hawakuwa nazo sana kwani walibebwa na chama.
11. Huenda Rais ajae atakuwa ndio rais bora zaidi kuliko wote ikiwa atachanganya tabia za marais wote wa awamu zote sita waliomtangulia bila kuziacha 4R za Samia.
12. Rais ajae kwa Upande wa CCM atatakiwa kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kukabiliana na upinzani kwa hoja, CCM lazima kukumbuka mwaka wa 2030 CHADEMA & ACT wataweka mgombea mmoja na huenda akawa ni Zitto Zuberi Kabwe kwa nguvu atakayojenga bungeni 2025-30 kwani ni muda mrefu wa kubadili chochote ikiwa ni pamoja na kupunguza makovu ya tofauti zao sanjari na CHADEMA kutokuwa na mgombea mwenye uwezo, Umri na kiwango cha Zitto Zuberi Kabwe au Tundu AM Lissu au hata Freeman Mbowe wa sasa.
13. Rais ajae kwa Upande wa Upinzani hasa CHADEMA kwa sasa ukimwondoa Tundu AM Lissu na Freeman Mbowe huoni Kiongozi mwingine mwenye haiba ya kuaminika kwa siasa za kitaifa labda kichama ambazo utamkuta John John Mnyika na John Heche hivyo lazima CHADEMA ama ikope mgombea ama waungane wasimamishe mgombea mmoja.
14. Rais ajae kwa Upande wa CHADEMA, Ukiwaangalia Tundu AM Lissu na Freeman Mbowe utawaona muda wao ukiwatupa mkono Uchaguzi mkuu ujao wa 2030 , CHADEMA itakuwa na changamoto ya Watu wa kuchagulika kwenye siasa za Kitaifa kama hali itasalia kuwa ilivyo kati ya sasa na 2030.
15. Rais ajae ndani ya CHADEMA, tangu mwaka 2005, CHADEMA imekuwa na wanasiasa wanne (4) tu ambao ni Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Tundu AM Lissu na Dkt Wilbroad Slaa hivyo tutegemee zaidi Sifa za watu hawa kuelekea hiyo 2030.
16. Rais ajae ndani ya CHADEMA, Kwa miongo miwili CHADEMA wameshindwa kutengeneza Viongozi wengine wa daraja hilo Haiyumkiniki waweze kuwa na wagombea imara zaidi ya waliopo kwa miaka mitano ijayo kwa lugha nyepesi 2030 wagombea toka CHADEMA ni hawahawa, Alianza kuibuka kidogo Mnyika na Heche lakini wamepoteza mwelekeo kwa karibu miaka saba sasa hivyo wagombea watakuwa ni hawa hawa.
17. Rais ajae ndani ya CHADEMA katika zao hilo la wanasiasa wa CHADEMA hao Wanne toka miaka ya 2000, umri utamruhusu Zitto pekee, ambaye pamoja na umri kumbeba dhidi ya wenzake 2030, Zitto Kabwe ameporomoka mno kisiasa kufuatia vita yake ndefu dhidi ya CHADEMA ambayo kama wataungana atapata nguvu maradufu na atakuwa mshindani wa kweli wa CCM hiyo 2030.
18. Rais ajae Watanzania kuna mambo watataka kuyaona toka kwake akijipambanua lakini pia kuna aina ya rais ajae anaeweza kuaminika kwa jamiii hiyo iliyojaa wasomi wengi mtaani ambao ni critical mass isio na ajira kabisa au isiyo na ajira rasmi.
19. Rais ajae atambue wenye ngazi ya diploma na degree mtaani watakuwa wengi kuliko waliopo kazini serikalini kwa ujumla, hiii ndio critical mass itakayotaka majibu huko 2030 ambayo itataka kiongozi ambae wana hakika nae kwamba anajua na ana uwezo wa kufanya tofauti kwa hakika ya uwezo wake sio porojo Wala maigizo ya hapa na pale.
20. Rais ajae afahamu mwenendo wa siasa za africa na dunia kwa muda sasa tangu miaka ya 2000, watu wamepoteza imani na falsafa au Itikadi za taasisi, Zaidi watu wanaamini mtu. Hivyo uhai na ushindi wa chama chochote umebaki mikononi mwa wagombea na nguvu yao kwa Umma sio Chama.
21. Rais ajae ndani ya CCM sio kuweka mgombea yeyote na kutegemea kushinda hapana, lazima kiweke mgombea wa kukibeba ili kushinda,
[Mkapa na Mwinyi hawakusomeka kwa umma lakini walishinda kwa sababu enzi hizo chama kilikuwa na nguvu ya kumshindisha yeyote ila kwa sasa ni kinyume chake.
22. Rais ajae ndani ya CCM na kumbukumbu za JPM kuonekana bora kuliko wote kwa kazi ndani ya CCM na ushindi alioupata ni jibu la hoja zangu kwa wagombea wa CCM ikumbukwe CCM tangu miaka ya 2005 inateua mgombea wa kukivusha chama sio kuvushwa hivyo CCM italazimika kuwa na mgombea maarufu kuliko CCM yenyewe huku Upinzani ukitegemea zaidi nguvu ya Chama.
23. Rais ajae atalazimika kuwa na Uraia usio na chembe ya shaka kutokana na yanayoendelea duniani lakini pia kwa hatma pana ya Taifa.
24. Rais ajae atalazimika kuwa ni kijana asiyepungua miaka 45 Wala kuzidi miaka 55 kulingana na Tanzania kuwa na wapiga kura wengi vijana kuliko wazee.
Toa pendekezo nani atafaa zaidi ya wote wanaotajwa tajwa au kujitaja.