Huyu ndio fundi chuma...

Huyo ndege nadhani ni WOODPECKER.



 
Naomba nipishane na wewe kidogo, hii sifa ni ya ndege wawili tofauti, kuna gotagota na Fundi Chuma, Fundi Chuma hutafuta sehemu nzuri ya mti na kuweka kiota chake ambacho ni kweli huwa imara kwa vile anachanganya na kila chochote anachokiokota na watoto wakikua huondoka na mwisho huwa ni makazi ya nyoka, huyu gotagota yeye ndio hotoboa mti kama picha zinavyoonekana hapo juu
 
Ndege huyu ndio yule anaitwa Woodpecker ama?
 
 
Mwandishi amechanganya sifa za ndege wawili fundi chuma yeye hujenga kiota kwa kutumia tope pamoja na miti hata mifupa ya wanyama waliokufa...yeye hana sifa ya kutoboa miti,bali hujenga kwenye matawi ya miti.Wakati mwingine huitwa "Ndege Mfalme"kwakuwa nyumba yake ni kubwa kama kasri ya Mfalme!
 
Majina labda ndio tofauti, lkn mie naona huyo huyo fundi chuma, kikwenu mnamuita gota gota mkuu..
 
Sijachanganya mkuu fundi chuma anatoboa mti, tobo na kutengeneza kiota chake, akichanganya na udongo, kwenye kiota chake kama nilivyoeleza, utakutana na nywele za binadamu, shanga, hadi baraghashia, na bado anawalinda watoto wake humo ndani ya kiota chake akiwa, ayupo ameenda kuwatafutia chakula, watoto wake hakuna adui atakaeingia humo mlangoni kwenye kiota anatengeneza kufuri la lililochanganywa na tope na majani ya nyasi mkuu.
 
Mwenye kujua sifa zake zaidi, sio mbaya akatuletea zaidi wakuu ..
 
Majina labda ndio tofauti, lkn mie naona huyo huyo fundi chuma, kikwenu mnamuita gota gota mkuu..
Mkuu hawa ndege ni wawili tofauti kabisa angalia hizo picha vizuri halafu kuhusu kabila
natumia lugha ya taifa peke yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…