Hahaha haaaaa, nimeipenda hii post ya huyu dada na imenifurahisa kwa sababu imeleta changamoto kwa vijana wengi maana nadhani waliokamilisha masharti yao ni wachache na pengine hawapo sina hakika.
Naomba nitoe maoni yangu juu ya hili tangazo, anachokihitaji huyu dada nahisi ndo matakwa ya wanawake wengi hasa wa mjini na ambao hawajaolewa na kuna vingine hajavitaja na hii ni moja ya sababu ya vitu ambavyo vinapelekea wanachelewa kuolewa. Kwa sababu anamtengeneza mme kichwani ambaye kwenye mazingira yake yanayomzunguka hayupo ndo maana ameamua kwenda extra mile kumtafuta kwa sababu katika wanamzunguka hayupo, mimi nina slogan moja ambayo huwa ninaiamini kwamba "mpenzi wako yuko pale ulipo" kama hayuko basi una mahusiano na mtu ambaye yuko mbali na wewe(long distance relationships) kama nako hayupo basi yuko hapohapo ulipo, so sioni sababu ya kwenda mbali, mimi ninaona inabidi uwe na potential mara mbili ya izo siga unazozihitaji kwa mwanaume then ndo nayeye atashawishika kukubali kama mke.
Ushauri wangu kwa vijana wa kiume tupokee haya matakwa ya huyu dada kama changamoto especially kwa wale ambao hawajaoa na kwa akina dada ambao hamjaolewa jaribuni kupata ushauri wa wamama wa makao juu wa wanaume wa kuwaoa msibase kwenye fikra zenu za kuwatengeneza wanaume kichwani na za kinadharia, hili swala liko practically. Wa mama wa makamo wanamaono mazuri na uzoefu katika hili jambo, nilivyokuwa mdogo nilikuwa najua ukifika umri flani ukitaka kuoa au kuolewa ni unaoa tu nilikuwa najua mke yupo la hasha!!! Kumbe maisha ni vita nilijua ukitaka mke ni kama unataka unata mtumba then unasema ngoja niende karume nifachukue mzigo. Siyo kazi rahisi.