khamis kilo
JF-Expert Member
- May 23, 2016
- 1,137
- 1,380
Rafael Caro Quintero 2
Enrique Camarena Salazar"Kiki" alikuwa askari kwenye kitengo cha kuzuia mihadarati "Drug Enforcement Agent" kwenye upelelezi wake akafanikiwa kufahamu mahala shamba hilo lilipo na baada ya kuripoti askari wakavamia na kuteketeza shamba lote na mzigo zaidi ya tani elfu kumi ulichomwa!!! Jambo hilo likapelekea Rafa pamoja na member wengine wa kundi hilo kutaka kulipa kisasi!!! February 7 1985 Enrique Camarena akiwa na rubani wake Alfredo Zavala walitekwa huko Guadalajara wakapata mateso makali na kisha kuuwawa. Baadae March 9 1985 Rafa akaamua kuondoka Mexico na kuelekea Costa Rica ukimbizini.
Tarehe 4 mwezi wa 4 1985 bwana Rafa akakamatwa huko Costa Rica kwenye mjengo wake akiwa amelala na kurudishwa Mexico ambapo alishtakiwa makosa mbalimbali ikiwemo na mauaji ya Camarena. Japokuwa jumla ya makosa yake yote alitakiwa kutumikia miaka 199 jela lakini akahukumiwa miaka 40 tu kwa kuwa sheria ya Mexico ilikuwa hairuhusu mtu kukaa jela kwa zaidi ya miaka 40.
Lakini alitumikia jela miaka 28 tu na August 9 2013 Rafa aliachiwa huru baada ya mahakama kudai amekuwa akionyesha mwenendo mzuri gerezani!! Lakini kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya "Drugs Enforcement Administration" mpaka leo kimemuweka kwenye list ya Most Wanted. Na pia serikali ya Marekani bado inamtamani Rafa kwa kuamini kuwa alikuwa akiendeleza uhalifu wake ingali akiwa gerezani, ambapo imeweka mezani dola millioni 20 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake.
Baada ya kukamatwa kwa Rafa kundi la Guadalajara lilisambaratika huku member wengine wakijiunga na makundi mengine kama Tijuana Cartel, Juarez Cartel, na wengine waliobaki wakaamua kurudi Sinaloa na kuanzisha kundi la Sinaloa Cartel akiwemo na Bwana Joaquin Guzman al maarufu kama "El Chapo". Tangu kuachiwa kwake Rafael Caro Quinteto hajawahi kuonekana hadharani, huku wengi wakiamini kuwa atakuwa amejificha huko kwao Sinaloa. Mwezi March mwaka jana jeshi la Mexico lilituma helicopter, drones na baadhi ya wanajeshi huko Sinolia kwenye vijiji vya La Noria, Las Juntas, Babunica na Bamopa ili kumsaka lakini kazi yao haikuzaa matunda kwani hawakufanikiwa kumpata, acha niishie hapa tu
•
MWISHO