Huyu ndiye bwana Heri bin Juma aliyepigana vita na Wajerumani maeneo ya Saadani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Mtawala wa Saadani, Alitawala chini ya Sultani wa Zanzibar kama mkubwa wake lakini akafaulu kutetea nafasi yake kama sultani aliejitegemea.

Mwaka 1882 aliweza kushinda jeshi la Sultani Sayyid Bargash aliyetaka kutawala Saadani moja kwa moja.

Saadani kama miji mingine ya pwani ilifaidika na biashara ya Wazungu walioleta bidhaa na kulipa ushuru. Alielewana vema nao.
Kuja kwa Wajerumani

Mwaka 1886 Sultani Sayyid Khalifa wa Zanzibar alikodisha eneo lake katika Tanganyika bara kwa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki . Bwana Heri pamoja na viongozi wengine aliona amesalitiwa na Sultani hakuwa tayari kukubali utawala wa Wajerumani.

1888 Vita ya Abushiri
Bwana Heri aliungwa mkono na upinzani wa Abushiri dhidi ya Wajerumani akipata usaidizi wa makabila wa eneo lake hasa Wazigua.

Alishambuliwa na kiongozi Mjerumani Hermann von Wissmann aliyekuwa na silaha za kisasa akapaswa kuacha kambi yake Saadani tarehe 6 Juni 1889. Aliendela na vita ya msituni .

Baada ya kushambuliwa tena na jeshi la Wajerumani katika Januari na Machi 1890 uwezo wake ulikwisha. Sayyid Khalifa aliwasiliana naye na Wissmann akatayarisha kujisalimisha kwake tarehe 6 Aprili 1890. Wissmann aliyemheshimu Bwana Heri hakumwua kama Abushiri bali akamwambia kujenga Saadani upya.

Upinzani wa wenyeji ulishindwa lakini ulisababisha mwisho wa utawala wa kampuni iliyoshindwa kukandamiza uasi wa Waafrika. Serikali ya Ujerumani iliona haja ya kuingilia kati na kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mikononi mwake kama koloni la serikali ya Ujerumani.

Mwisho wake
Mwaka 1894 alijaribu tena kupambana na Wajerumani lakini alishindwa kwa mara ya pili. Akaondoka bara kwenda Zanzibar alipokufa baadaye.
 
Mtawala wa Saadani
Alitawala chini ya Sultani wa Zanzibar kama mkubwa wake lakini akafaulu kutetea nafasi yake kama sultani aliejitegemea.
Mwaka 1882 aliweza kushinda jeshi la Sultani Sayyid Bargash aliyetaka kutawala Saadani moja kwa moja.
Saadani kama miji mingine ya pwani ilifaidika na biashara ya Wazungu walioleta bidhaa na kulipa ushuru. Alielewana vema nao.
Kuja kwa Wajerumani
Mwaka 1886 Sultani Sayyid Khalifa wa Zanzibar alikodisha eneo lake katika Tanganyika bara kwa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki . Bwana Heri pamoja na viongozi wengine aliona amesalitiwa na Sultani hakuwa tayari kukubali utawala wa Wajerumani. 1888
Vita ya Abushiri
Bwana Heri aliungwa mkono na upinzani wa Abushiri dhidi ya Wajerumani akipata usaidizi wa makabila wa eneo lake hasa Wazigua.
Alishambuliwa na kiongozi Mjerumani
Hermann von Wissmann aliyekuwa na
silaha za kisasa akapaswa kuacha kambi yake Saadani tarehe 6 Juni
1889. Aliendela na vita ya msituni .
Baada ya kushambuliwa tena na jeshi la Wajerumani katika Januari na Machi
1890 uwezo wake ulikwisha. Sayyid Khalifa aliwasiliana naye na Wissmann akatayarisha kujisalimisha kwake tarehe 6 Aprili 1890. Wissmann aliyemheshimu Bwana Heri hakumwua kama Abushiri bali akamwambia kujenga Saadani upya.
Upinzani wa wenyeji ulishindwa lakini ulisababisha mwisho wa utawala wa kampuni iliyoshindwa kukandamiza uasi wa Waafrika. Serikali ya
Ujerumani iliona haja ya kuingilia kati na kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mikononi mwake kama koloni la serikali ya Ujerumani.
Mwisho wake
Mwaka 1894 alijaribu tena kupambana na Wajerumani lakini alishindwa kwa mara ya pili. Akaondoka bara kwenda Zanzibar alipokufa baadaye.
Mjukuu wa Chifu,
Ahsante sana.
In Shaa Allah naingia Maktaba nikipata picha nitaiweka hapa.
 
Donnie,
Niwie radhi nilisahau.
Nitatafuta samahani sana.
Bwana Heri huyo.
Siku nyingine ikiwa unatafuta kitu ingia Google.
Kuna mengi utapata.

Screenshot_20200528-083248.jpg
 
Mbirwa,
Sikuulizi hilo.
Nachotaka kujua ni zipo athari za Bwana Heri hapo Saadan?
Siwezi kujibu kwa uhakika hali ya kimaisha Kiuchumi na Kijamii Saadan zimeathiriwa na Bwana Heri. Swali lako linaweza kujibiwa kwa kufanyika Ethnographic Research kuja na ushahidi wa hili.

Saadan inafanana na jamii nyingine za Pwani, kama Bagamoyo, Lindi na Tanga tofauti kubwa kuzungukwa na hifadhi kumeiadhiri na Sheria za Uhifadhi na kupunguza mwingiliano wa shughuli za kiuchumi.

Utakumbuka Saadan walikuwa wazalishaji wa chumvi inayosafirisha hadi Afrika ya kati, lakini kwa sasa uzalishaji umepungua.

Sina uhakika kama nitakuwa nimejaribu kukujibu Mzee Mohamed Said .
 
... watu wa Pwani kwa kujiona mashujaa dhidi ya ukoloni hawawezekaniki! Mara Bwana Heri, mara Abushiri, mara sijui nani utadhani majenerali fulani kumbe midebwedo tu. Vichwa maji walikuwa huko bara akina Mkwawa, Mirambo, Songea, na dizaini hizo. Hawa kweli walikuwa majenerali wa nyakati zao! Sio hao "wala urojo" kila mara kukimbilia hapo Zanzibar kuomba hifadhi kwa Sultan.
 
Wape sifa zao hata kama unadhani walikuwa "midebwedo" bado waliweza kujitoa kupambania watu wao.
 
... watu wa Pwani kwa kujiona mashujaa dhidi ya ukoloni hawawezekaniki! Mara Bwana Heri, mara Abushiri, mara sijui nani utadhani majenerali fulani kumbe midebwedo tu. Vichwa maji walikuwa huko bara akina Mkwawa, Mirambo, Songea, na dizaini hizo. Hawa kweli walikuwa majenerali wa nyakati zao! Sio hao "wala urojo" kila mara kukimbilia hapo Zanzibar kuomba hifadhi kwa Sultan.
Mwana kulitafuta, mwana kulipata.
 
Siwezi kujibu kwa uhakika hali ya kimaisha Kiuchumi na Kijamii Saadan zimeathiriwa na Bwana Heri. Swali lako linaweza kujibiwa kwa kufanyika Ethnographic Research kuja na ushahidi wa hili.

Saadan inafanana na jamii nyingine za Pwani, kama Bagamoyo, Lindi na Tanga tofauti kubwa kuzungukwa na hifadhi kumeiadhiri na Sheria za Uhifadhi na kupunguza mwingiliano wa shughuli za kiuchumi.

Utakumbuka Saadan walikuwa wazalishaji wa chumvi inayosafirisha hadi Afrika ya kati, lakini kwa sasa uzalishaji umepungua.

Sina uhakika kama nitakuwa nimejaribu kukujibu Mzee Mohamed Said .
Mbiirwa,
Ahsante inatosha ingawa ningependa kufahamu kama wako watu wa ukoo utokanao na Bwana Heri.
 
Mwana kulitafuta, mwana kulipata.
Kawoli,
Mkwawa jina lake lingine ni Abdallah lakini hili halivumi.

Songea na yeye jina lake lingine ni Abdulrauf.

Majina haya yote yanatoka kwenye sifa (attributes)99 katika majina ya Allah.

Mkwawa alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mohamed bin Khalfan bin Khamis Al Barwani kwa jina lingine Rumaliza kutoka Zanzibar na ukifika Kalenga kwenye kumbukumbu ya Mkwawa utakuta barua zake alizokuwa akiandikiana na washirika zake waliokuwa Zanzibar zilizokuwa zimeandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Mmoja wa majemadari wake alikuwa nduguye jina lake Yusuf.
 
... watu wa Pwani kwa kujiona mashujaa dhidi ya ukoloni hawawezekaniki! Mara Bwana Heri, mara Abushiri, mara sijui nani utadhani majenerali fulani kumbe midebwedo tu. Vichwa maji walikuwa huko bara akina Mkwawa, Mirambo, Songea, na dizaini hizo. Hawa kweli walikuwa majenerali wa nyakati zao! Sio hao "wala urojo" kila mara kukimbilia hapo Zanzibar kuomba hifadhi kwa Sultan.
Umemsahau Hassab Ibn Omary Makunganya wa Kilwa Kivinje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawoli,
Mkwawa jina lake lingine ni Abdallah lakini hili halivumi.

Songea na yeye jina lake lingine ni Abdulrauf.

Majina haya yote yanatoka kwenye sifa (attributes)99 katika majina ya Allah.

Mkwawa alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mohamed bin Khalfan bin Khamis Al Barwani kwa jina lingine Rumaliza kutoka Zanzibar na ukifika Kalenga kwenye kumbukumbu ya Mkwawa utakuta barua zake alizokuwa akiandikiana na washirika zake waliokuwa Zanzibar zilizokuwa zimeandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Mmoja wa majemadari wake alikuwa nduguye jina lake Yusuf.
Naaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom