Huyu ndiye James Kotei

njundelekajo

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
310
Reaction score
227
HUYU NDIYE JAMES AGYEKUM KOTEI

Wakati anasajiliwa Simba mwaka 2016 alipewa mkataba wa "mashaka mashaka" wa mwaka mmoja kwa majaribio ,baada ya timu hiyo kunogewa na huduma yake ikafunga nae ndoa nyingine kwa kumpa mkataba mnono wa miaka miwili.

Huyu ndiye mtu pekee aliyetishia utawala wa Jonasi Mkude ndani ya Simba kipindi cha Joseph Omog kabla ya Masoud Djuma kuamua kuwachezesha wote wawili.

Anaitwa James Agyekum Kotei raia wa Ghana na mume halali wa mrembo Matilda Kwakye.Binadamu aliyezaliwa miaka 26 iliyopita haonekani kutajwa tajwa sana na mashibiki wa Soka hapa nchini licha ya shughuli nzito anayoifanya uwanjani.

Uwepo wake ndani ya kikosi cha Simba umeimarisha sana safu ya ulinzi wa timu hiyo iliyofungwa magoli 4tu dhidi ya 15 uliyofunga kwenye mechi tano za mashindano ya Klabu bingwa hadi sasa.

Urefu wake wa futi 5.8 umekua na faida katika kunyang'anya mipira kwa adui kama ilivyokua kwa Patric Viera wa Arsenal,Yahya Toure na wengine.

Simba imekua ikipata wakati mgumu sana kupata matokeo anapokosekana,lakini uwepo wake kikosini umekua ukiwapunguzia sana majukumu ya ukabaji Pascal Wawa,Jonasi Mkude na Erasto Nyoni hivyo kupata muda wa kusaidia mashambulizi.

Ndio maana haishangazi sasa kumuona Mkude akifunga,kupiga mashuti na Pascal Wawa akihusika kwenye baadhi ya magoli ya Simba.

Tangu afunge dhidi ya Kakamega kwa penalt mwaka 2018 mkude hajawahi kufunga goli lolote mpka alipoifunga Nkana hivi karibuni.Na anaonekan atafunga mengine .

Kwenye goli la kwanza Simba ilipocheza dhidi ya Mbabane Swallows,na Mechi iliyochezwa juzi dhidi ya J.SSoura Pascal Wawa amekua mtu wa pili kuugusa mpira kabla ya mfungaji(Second Assist)

Lakini pia mashambulizi
mengi ya Simba hivi karibuni yanaanzia kwake.Katika maisha yake ya soka tangu Asec Mimosa,Azam,El Merrekh Wawa hajawahi fanya hivi.

Ubora wa huu wa sasa wa Mkude na Pascal Wawa katika kufunga na kuanzisha mashambulizi unachangiwa sana na kazi anayoifanya James Kotei,ndio maana hakuna aliyeliona pengo la Erasto Nyoni siku Simba ilipocheza na J.S.Ssoura.

KWA NINI HATAJWI TAJWI KAMA WACHEZAJI WENGINE?

Katika kipindi cha miaka 21 (1997-2018) tuzo ya mcheza bora ya Ballon D'or imewahi kuchukuliwa mara moja tu na mchezaji asiye na asili ya kushambulia na asiyefunga (Fabio Cannavaro mwaka 2006).

Mabadiliko haya ya kimtazamo wa soka la kisasa kuhusisha uchezaji bora na ufungaji umewaathiri wacheza ji wengi duniani akiwepo na Kotei mwenye goli moja.

Katika mtazamo wa sasa juu ya mchezaji bora ni yupi ni rahis kwa Eliud Ambokile wa Mbeya City kuwa mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania kuliko Kelvin Yondani wa Yanga kama ulivyo ugumu kwa David Degea mbele ya Harry Keane.

Siku hizi uchezaji bora ni kufunga na kuhusika katika magoli ndio maana ni rahisi kueleweka kuwa mchezaji bora kwenye mechi kati ya Simba dhidi ya J.S.Ssoura ni Emanuel Okwi ,ingelikua zile George Apong Weah anacheza soka,James Kotei ndiye angepaswa kuwa.

Noel Nguzo.R.

15/1/2019
 
Attachments

  • KoteiJamesSimba.jpg
    7 KB · Views: 88
[Is a good midfielder,deep frezer,wakati timu pinzani inaposhambulia yeye huwa anatuliza moto wa mpinzani kwa staili ya deep freezer inavyopooza vitu vya moto,ana pasi nzuri,kwa kifupi anabalance team inapoenda kushambulia au inapoenda kushambuliwa......mapungu yake ni machache tu,kupiga buti ya kucheza rafu na muda mwingine hupiga pasi zisoizofika....otherwise he is a classic midfielderQUOTE="njundelekajo, post: 30024227, member: 116038"]HUYU NDIYE JAMES AGYEKUM KOTEI

Wakati anasajiliwa Simba mwaka 2016 alipewa mkataba wa "mashaka mashaka" wa mwaka mmoja kwa majaribio ,baada ya timu hiyo kunogewa na huduma yake ikafunga nae ndoa nyingine kwa kumpa mkataba mnono wa miaka miwili.

Huyu ndiye mtu pekee aliyetishia utawala wa Jonasi Mkude ndani ya Simba kipindi cha Joseph Omog kabla ya Masoud Djuma kuamua kuwachezesha wote wawili.

Anaitwa James Agyekum Kotei raia wa Ghana na mume halali wa mrembo Matilda Kwakye.Binadamu aliyezaliwa miaka 26 iliyopita haonekani kutajwa tajwa sana na mashibiki wa Soka hapa nchini licha ya shughuli nzito anayoifanya uwanjani.

Uwepo wake ndani ya kikosi cha Simba umeimarisha sana safu ya ulinzi wa timu hiyo iliyofungwa magoli 4tu dhidi ya 15 uliyofunga kwenye mechi tano za mashindano ya Klabu bingwa hadi sasa.

Urefu wake wa futi 5.8 umekua na faida katika kunyang'anya mipira kwa adui kama ilivyokua kwa Patric Viera wa Arsenal,Yahya Toure na wengine.

Simba imekua ikipata wakati mgumu sana kupata matokeo anapokosekana,lakini uwepo wake kikosini umekua ukiwapunguzia sana majukumu ya ukabaji Pascal Wawa,Jonasi Mkude na Erasto Nyoni hivyo kupata muda wa kusaidia mashambulizi.

Ndio maana haishangazi sasa kumuona Mkude akifunga,kupiga mashuti na Pascal Wawa akihusika kwenye baadhi ya magoli ya Simba.

Tangu afunge dhidi ya Kakamega kwa penalt mwaka 2018 mkude hajawahi kufunga goli lolote mpka alipoifunga Nkana hivi karibuni.Na anaonekan atafunga mengine .

Kwenye goli la kwanza Simba ilipocheza dhidi ya Mbabane Swallows,na Mechi iliyochezwa juzi dhidi ya J.SSoura Pascal Wawa amekua mtu wa pili kuugusa mpira kabla ya mfungaji(Second Assist)

Lakini pia mashambulizi
mengi ya Simba hivi karibuni yanaanzia kwake.Katika maisha yake ya soka tangu Asec Mimosa,Azam,El Merrekh Wawa hajawahi fanya hivi.

Ubora wa huu wa sasa wa Mkude na Pascal Wawa katika kufunga na kuanzisha mashambulizi unachangiwa sana na kazi anayoifanya James Kotei,ndio maana hakuna aliyeliona pengo la Erasto Nyoni siku Simba ilipocheza na J.S.Ssoura.

KWA NINI HATAJWI TAJWI KAMA WACHEZAJI WENGINE?

Katika kipindi cha miaka 21 (1997-2018) tuzo ya mcheza bora ya Ballon D'or imewahi kuchukuliwa mara moja tu na mchezaji asiye na asili ya kushambulia na asiyefunga (Fabio Cannavaro mwaka 2006).

Mabadiliko haya ya kimtazamo wa soka la kisasa kuhusisha uchezaji bora na ufungaji umewaathiri wacheza ji wengi duniani akiwepo na Kotei mwenye goli moja.

Katika mtazamo wa sasa juu ya mchezaji bora ni yupi ni rahis kwa Eliud Ambokile wa Mbeya City kuwa mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania kuliko Kelvin Yondani wa Yanga kama ulivyo ugumu kwa David Degea mbele ya Harry Keane.

Siku hizi uchezaji bora ni kufunga na kuhusika katika magoli ndio maana ni rahisi kueleweka kuwa mchezaji bora kwenye mechi kati ya Simba dhidi ya J.S.Ssoura ni Emanuel Okwi ,ingelikua zile George Apong Weah anacheza soka,James Kotei ndiye angepaswa kuwa.

Noel Nguzo.R.

15/1/2019[/QUOTE]
 
Wakati anafika sikumuona kua ni muhimu ila kwa sasa nampa credit zote

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi ingawa ni mshabiki wa Yanga huwa namkubali sana huyu jamaa. Ni kiungo mtulivu sana awapo uwanjani, achilia tu kuwa alimfanyia rafu mbaya Gadiel Michael. Hata hivyo mimi binafsi namuombea msamaha kwa hilo. Big up James Kotei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…