Huyu ndiye mdudu chunusi wa usoni?

Huyu ndiye mdudu chunusi wa usoni?

Me too

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
7,388
Reaction score
9,333
Pitapita zangu mitandaoni nikakutana na hiki kitu kuwa huyu ndiye mdudu anayekuwepo usoni na kusababisha chunusi hizi tuzionazo baada ya balehe👇

FB_IMG_16571397276286010.jpg

Wanasema unapobinya chunusi hutokea weupe ule weupe unakuwa umetoka kwa huyo mdudu yaani umemfinya yeye na damu yake ndo inaachia mabakabaka usoni au eneo husika.

FB_IMG_16572667491736808.jpg
FB_IMG_16572667216515443.jpg

Swali kwa wataalamu je ni kweli?

NB: uzi usipelekwe JF doctors sitafuti tiba, bali mawazo na hoja za watu juu ya hilo swala.
 
Nahisi
swali, kwa nini uyo mdudu anaibuka kipindi cha balehe? Connection kati ya balehe na mdudu inatokea wapi?
Ni mabadiliko ya mwili vinatokea ambavyo avikuwepo ni sawa na kuota ndevu au titi,

Ila kwa usahihi zaidi ngoja waje watueleze wajuvi
 
swali, kwa nini uyo mdudu anaibuka kipindi cha balehe? Connection kati ya balehe na mdudu inatokea wapi?
Ngozi, kinywani na tumboni ndizo sehemu zenye bakteria wengi zaidi mwilini.. mabilioni ya bakteria.. hivyo kama huyo bakteria anaishi ndani ya vishimo vya vinyweleo lazima awemo kwenye mchanganyiko huu wa mafuta,usaha na bakteria uitwao chunusi

Kipindi cha balehe ngozi huzalisha zaidi mafuta ambayo hadi mengine yananasa ndani ya vinyweleo.. yakishanasa inamaana seli zilizokufa hazitolewi zinanasa humo pia bakteria mbalimbali (sio aina moja tu) wa kwenye ngozi nao hunasa humo.. kitendo hiki hufanya kinga ya mwili kujibu kwa kupeleka majeshi ya ulinzi ndani ya vishimo vya vinyweleo(inflamatory mediators ikiwemo seli hai nyeupe za damu unazoona kama usaha ukibinya chunusi) na kusababisha kuvimba na kutokeza kama mapele juu
 
Ngozi Ina mizizi ya vinyweleo na Kuna gland zinazotoa mafuta. Sasa hiyo mizizi ya vinyweleo vikizibwa na mafuta na ngozi iliyokufa basi husababisha chunusi na wakati mwingine hupata maambukizi ya bakteria.

Hii nimejitahidi kuelezea kwa kifupi sana na kiurahisi
Mkuu na vipi muwasho unahisi ninin kinasababisha? ikiwa external skin ikitambaliwa na mdudu washawasha utajikuna na tupele tutatokea sehemu husika je internal skin kuna nin kinaleta muwasho na kujikuna kisha kuleta vipele hivyo?
 
Ngozi, kinywani na tumboni ndizo sehemu zenye bakteria wengi zaidi mwilini.. mabilioni ya bakteria.. hivyo kama huyo bakteria anaishi ndani ya vishimo vya vinyweleo lazima awemo kwenye mchanganyiko huu wa mafuta,usaha na bakteria uitwao chunusi
Elimu nzuri mkuu enheee endelea sasa
 
elimu nzuri mkuu enheee endelea sasa
Kipindi cha balehe ngozi huzalisha zaidi mafuta ambayo hadi mengine yananasa ndani ya vinyweleo.. yakishanasa inamaana seli zilizokufa hazitolewi zinanasa humo pia bakteria mbalimbali (sio aina moja tu) wa kwenye ngozi nao hunasa humo.. kitendo hiki hufanya kinga ya mwili kujibu kwa kupeleka majeshi ya ulinzi ndani ya vishimo vya vinyweleo(inflamatory mediators ikiwemo seli hai nyeupe za damu unazoona kama usaha ukibinya chunusi) na kusababisha kuvimba na kutokeza kama mapele juu
 
Na vipi kuhusu

Huyo mdudu ni kweli yupo usoni?
 
Pitapita zangu mitandaoni nikakutana na hiki kitu kuwa huyu ndie mdudu anaekuwepo usoni na nakusababishia chunusi hizi tuzionazo baada ya balehe[emoji116]

View attachment 2284255

wanasema unapobinya chunusi hutokea weupe ule weupe unakuwa umetoka kwa huyo mdudu yaani umemfinya yeye na damu yake ndo inaachia mabakabaka usoni au eneo husikaView attachment 2284267View attachment 2284268

swali kwa wataalamu je ni kweli?

NB: uzi usipelekwe jf doctors sitafuti tiba, bali mawazo na hoja za watu juu ya hilo swala.
Si kweli Mkuu kwa hoja zifuatazo:-

Chunusi (Acne Vulgaris) ni ugonjwa unaohusisha tezi za kuzalisha mafuta (oil glands) zilizopo chini ya ngozi kwenye sehemu ya vijitundu vya vinyweleo (hair follicles)

Kila kitengo huundwa na kijitundu cha kinyweleo (hair follicle), tezi ya mafuta (sebacious gland) na kinyweleo (hair). Vijitengo hivi vinapatikana sehemu zote za mwili isipokuwa maeneo ya viganja vya mikono, kwenye nyayo, sehemu za juu za miguu na kwenye midomo. Vitengo hivi hupatikana kwa wingi usoni, shingoni na kifuani.

Tezi za mafuta hutoa sebum ambayo huvisaidia ngozi na vinyweleo kutokuwa vikavu.

Mtu anapokuwa kwenye balehe, tezi hizi za mafuta hupanuka na kuwa kubwa na hutoa sebum (aina ya mafuta) kwa wingi zaidi, hali inayochangiwa na kuongezeka kwa homoni za androgens. Baada ya umri wa miaka 20, utengenezaji wa sebum hupungua.

Sasa mdudu huyo mbona sioni alipoelezewa Mkuu?
 
Back
Top Bottom