Huyu ndiye Mh. KAGASHEKI

naomba ufafanuzi,
je alisema atajenga hiyo hospitali na uwanja wa ndege
kwa pesa zake za mfukoni au kwa pesa kutoka wapi?
It doesn't matter fedha zitatoka wapi! Issue hapa ni kwamba alitoa ahadi. je alipotoa hiyo ahadi hakujua mambo yote ya kujenga miundo mbinu fedha zinatoka wapi? Kama hakujua basi ni alidanganya wananchi na kama alijua bado alidanganya wananchi. Wanachotaka wananchi ni ahadi zako umezitimiza? Kama hukutumiza ahadi kuna sababu nyingi nzuri tu lakini zote hizo zinaitwa "excuse" na hii haikubaliki. Performanca is required and nothing less than that. You must stay to what you have promised. Anyway lakini "no politician has died by swallowing his own words"
 

Na nyinyi mlimuamini? Hakuna mtu mwenye ubavu wa kujenga hospitali ya rufaa au uwanja wa ndege unaoeleweka Tanzania. Kama mlimpa kura kutokana na ahadi hizi ambazo wazi ni za alinacha basi inabidi mjisikitikie wenyewe. Kama Bukoba mlikojaa wasomi mdanganywa kirahisi hivyo, sehemu nyingine zitakuwaje? Halafu tunashangaa kwa nini bado tuko hapa tulipo!

Amandla.....
 
hizo ni siasa za bongo tisha toto lakini hata panya hatishiki
 

Hii habari imekaa kushoto mno. Inaweza ikawa ni uzushi tu wa kumchafua Kagasheki. Tunaitaka hotuba yote aliyoitoa ili tuweze kuamini!
 

Ukiona mbunge anatumia vitisho ujue MAJI YAMEZIDI UNGA!!!
 

Mkuu jamaa msanii kweli kweli...katikati ya kampeni za 2005, akaleta wazungu wake ...wakapima pima eti ni jinsi gani uwanja utapanuliwa upande ule wa ziwa victoria (kuhamisha ziwa)....ujinga na umasikani upo sehemu zote za Tanzania mkuu..... si Bukoba , Dar, Moshi.... Watu walipoona wazungu wanapima pima wakajua maendeleo ndo hayooooo...ujue ana sifa ya swahida "tumeongelea hilo nyuma"
 
Hii habari imekaa kushoto mno. Inaweza ikawa ni uzushi tu wa kumchafua Kagasheki. Tunaitaka hotuba yote aliyoitoa ili tuweze kuamini!

Ni vigumu kwa mswahili kuamini moja kwa moja. Hapa hakuna cha uzushi, ninaamini nilichokisia na kuna mtu katoa hadi picha za maandamano hayo akidhibitisha hilo.

Na hotuba yake bado inarudiwa kwenye kiji radio chake cha kampeni hizi mgando. Ni kichefuchefu tupu.
 


Tafadhali tuwekeeni hicho kipande cha hotuba yake, tusikie na kuamua wenyewe. Kampeni zimeanza, lolote linaweza kuwekwa popote na kuwekewa jumuisho linalolenga anakotaka mhusika. Tuwekee hotuba yake tumsikie, ndipo tuanze kumjadili ipasavyo.
 
naomba ufafanuzi,
je alisema atajenga hiyo hospitali na uwanja wa ndege
kwa pesa zake za mfukoni au kwa pesa kutoka wapi?
hivi kweli na ujuwaji wao wote watu wa Kagera wanapatikana kwa uwongo wa kitoto kabisa,
 
hii mada nimeipendea kitu kimoja, nimeona majina ya zamani na ya MAGREAT THINKERZ maarufu ambao siku hizi ni nadra sana kuchangia, GUYZ TUWE PAMOJA
 
hii mada nimeipendea kitu kimoja, nimeona majina ya zamani na ya MAGREAT THINKERZ maarufu ambao siku hizi ni nadra sana kuchangia, GUYZ TUWE PAMOJA

Basi tuwe wastaarabu kidogo, tunaanza kutajana majina!!!

Kwa upande wangu siasa za BK sizifahamu, ila siasa najifunzia hapa JF.
 

Picha za maandamano sio hoja hazithibitishi maneno yanayodaiwa kwamba Kagasheki ameyasema.



No! Huu ni uzushi Kagasheki hawezi kusema haya na kama yanatoka kwenye redio yawezekana kabisa kuna hujuma ya aina fulani!
 
Picha za maandamano sio hoja hazithibitishi maneno yanayodaiwa kwamba Kagasheki ameyasema.



No! Huu ni uzushi Kagasheki hawezi kusema haya na kama yanatoka kwenye redio yawezekana kabisa kuna hujuma ya aina fulani!


Boramaisha sikuelewi, sijui ni kipi halielweki hapa. Nilipoanzisha hii mada kuna mchangiaji aliiunga mkono na akajaribu kutoa picha za maandamano, lakini bado unasema haiwezekani na unadiliki kusema "NO" na kusema kama yanatoka radio basi ni hujuma.

Napata tatizo na uwezo wako wa kufuatilia mambo na uchangiaji.

awali nilisema nilimsikia "live" akihutubia mkutano kupitia radi "KASIBANTE" anayomiliki yeye Mh. KAGAESHEKI. Vile vile baada ya muda nilipishana na maandamano yake baada ya mkutano. Zaidi nikasema anayeweza ku access full speach atusaidie hili na nyie mliofungwa na kugandishwa ubongo mpate upeo,

Ushauri wa bure "hata kama hamtaki hali ndio hiyo, haiwezekani vipi?"
 
Kagasheki anajua fika jinsi "alivyoshinda" ubunge wa Bukoba mjini 2005.Ubatili Mtupu! Sasa anaogopa kivuli chake mpaka anaweweseka mpaka anatishia maisha ya mtu toka CCM atakayethubutu kumpinga kwenye kura za maoni. Na wapo. Kama anaogopa joto la jikoni atoke aende sebuleni yaani asubiri kuteuliwa na Rais katika Bunge la 2010.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…