tatizo ni sera mbofu mbofu za CCM ambazo hazitoi unafuu kwa mwananchi.
Mkuu Kibs, fikiria mtu kalima mahindi na amevuna ya kutosha [ana ziada ya kuuza], ukifika msimu wa kuuza, anaambiwa hakuna kuuza nje, wakati ndani ya nchi hakuna soko la kueleweka na bei ni ya chini ukilinganisha na kuuza nje.
Juzi, Boss wako JK kapita Sumbawanga na Tunduma (Mby) watu wanalalamika hakuna soko la mahindi. Rais wako akawadanganya kwamba ataongeza hela za SGR ambazo hazipo. Rukwa sasa hivi ina ziada ya tani 900,000 za mahindi. SGR ina fedha za kununua tani 400,000 kutoka Sumbawanga, yaani kwa maneno mengine kila mkoa unao zalisha mahindi umewekewa kiwango cha kuuza mahindi SGR. Sasa kama hakuna mnunuzi, kwanini serikali izuwie wasiuze nje?
Mkuu wa Mkoa wa Sumbawanga anasema kwamba ili kuwasaidia wakulima wa Sumbawanga kuondokana na umasikini inabidi serikali iwaruhusu wauze mahindi nje ya nchi. Huyo anayependekeza hivyo siyo mpinzani ni m-CCM mwenzenu na anajionea hali halisi iliyo mkoani kwake.
Hilo haliishii kwenye mahindi tu, nenda kwenye korosho, kahawa, pamba, tumbaku na mazao mengine ama soko ni holela kiasi kwamba wakulima wanaishia kupunjwa au ufisadi wa wanunuzi ambao wanalindwa na serikali na wanajifanyia wanachoweza.
Matokeo yake ndio hayo ya akina mama kuingia mtaani kuganga njaa kwa kuuza mito, sijui anauza mito mingapi kwa siku? Halafu serikali yako ya CCM kupitia kwa fisadi Kapuya inatangaza kwamba wame-create ajira kwa huyo mama! Bado mwenzetu huoni kwamba kuna tatizo ... kaazi kweli kweli. Anyway, ni madhara ya Jembe na Nyundo!