Huyu ndiye muasisi wa Jina Tanzania

Huyu ndiye muasisi wa Jina Tanzania

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Anaitwa Mohamed Iqbal Dar ni mtanzania anayeishi wingereza
Mzee Mohamed Said shikamoo tunaomba mchango wako kwa hili
 

Attachments

  • Screenshot 2024-07-21 080728.png
    Screenshot 2024-07-21 080728.png
    229.6 KB · Views: 6
Adm naomba mada hii ihamisheni kule kwenye habari na hoja mchanganyiko maana wasomaji wengi vijana wetu wajue historia ya Tanzania kisha mtairudisha mahali pake
 
Huu uzi wakiuona Mohamed Said na FaizaFoxy tumekwisha
Bora hata ya Mzee Mohamed japo yupo biased kwenye story zake hasa likija swala la Uislam ila ana uwezo wa ku back up story zake na ushahidi.

Tatizo la Bi Nyakomba, yeye anabwatuka na mikebehi mixer dharau.

Nikisoma comments za Faiza navuta picha ujana wake na kuona picha ya Giggy Money.
 
Wakristo punguzeni chuki dhidi ya waislam, nchi yetu sote hii.
Kwanza wazee wenu walikua machakani tu huko, wala walikua hawajui kama huku mjini kuna harakati za kudai uhuru.
Kwahiyo punguzeni chuki dhidi ya watu waliowafanya muwe huru.
 
Nashangaaga wa Tanganyika kuitwa watanzania , wanzanzibar kuitwa wanzanzibar ikiwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili!?, Ndo kusema tumeuziwa mbuzi kwenye kiroba!??🤔
 
Nimsubiri Mzee wetu Mohamed Said au Faiza Foxy nikaona niingilie kati someni chini sasa

Watu wengi wanajua tu kuwa Tanzania ni nchi iliyopo katika Africa Mashariki.Lakini ni wachache wanaojua muasisi wa jina hilo ni nani.

Wakati ule raisi wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere na raisi wa Zanzibar Abeid Amani Karume wanajulikana kwa kuziunganisha nchi zao na kuleta kitu kinachoitwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, lakini ni wachache wanaojua kuwa kati ya marais hao wawili hakuna hata mmoja kati yao aliyeshiriki kutengeneza jina Tanzania.

Basi ni hivii “TAN” inasimama kutokana na herufu tatu za kwanza TANganyika, na “ZAN” inasimama kutokana na herufu tatu za kwanza za ZANzibar. Baada ya hapo zikaongezewa herufu mbili za mwisho – “IA” ndio jina “TANZANIA.” Likapatikana hata hivyo aliyeasisi jina hili alikuwa muumini wa kiislam dhehebu la Ismailia inasemekana vile alikuwa mcha mungu wa dini yake aweke herufu za mwisho za IsmaiIA wengi walifikiri inatokana na hivyo laini haikuwa hivyo ila aliona sababu nchi nyingi zinaishia na IA
Mfano Ethiopia,Nigeria,Liberia,Yugoslavia,Tunisia,Somalia,Mauritania,Mesopotamia,Mongolia,Australia,Tasmania,Bolivia,Bulgaria, nk ngoja aongee hiyo IA mwishoni.

Ulikuwa ni ubunifu wa wakati huo wa kijana mdogo mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyekuwa anasoma kidato cha nne shule ya secondary Mzumbe Morogoro akiwa na umri wa miaka 18 mwaka 1964 aliyeitwa Mohamed Igbal Dar.

Ubunifu wake ulipatikana kwa kuunganisha maneno kutoka nchi hizi mbili “Tanganyika na Zanzibar.”

Jina “Tanganyika” linatokana na maneno mawili ya Kiswahili yaani tanga(sail) yaani mfano kutanga tanga na neno nyika (“uwanda maporini ambapo hakuna mtu anaishi).Yaani kutanga tanga nyikani kusiko na watu.

Neno Zanzibar linatokana na neno “zenji”, yaani watu wa asili yaani watu Weusi na kukaongezwa neno la kiarabu bar maana yake pwani kwa hiyo ukiunganisha maana yake nchi ya watu Weusi wanaoshi pwani”

Mohamed Iqbal Dar kiusanii aliunda neno Tanzania baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutoa tangazo kwenye gazeti la The Nationalist kwa sasa, Daily News,jina la nchi mpya itavyoitwa baada ya kungana kati ya Tanganyika ifikapo hapo 26th April 1964.

Mohamed Iqbal Dar alizawadiwa shillingi 200 na kwa kutambua mchango wake huo,Idrisa Abdul Wakili ambaye wakati huo alikuwa ndio waziri wa mambo ya ndani ambapo baadae akawa raisi wa Zanzibar alimpa cheque ya shillingi 200 na zawadi ya ngao.

Historia inaonyesha kuwa washiriki walikuwa raia 80 kwenye shindano hilo na Mohamed Iqbal Dar ndio akatangazwa mshindi.

Mohammed Iqbal Dar alizaliwa Tabora mwaka 1944 kwa sasa ni mzee yuko Birmigham Wingereza na ana umri wa miaka 78.

Baba yake alikuwa daktari huko Tanga enzi za ukoloni

Mungu amtunze mzee huyu
 

Attachments

  • Mohamed.png
    Mohamed.png
    930.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom