Huyu ndiye Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta

Huyu ndiye Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Jina lake halisi lilikuwa Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni Mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyatta lilitokana na mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga . Wagĩkũyũ wanauita kenyaata.
f24f2e2f248a5eeabd84b5b28c2ecdba.jpg

Alisoma katika shule ya kanisa la wamisionari wa Kiskoti .
Baada ya kuhitimu aliajiriwa kama karani na msoma mita wa manispaa ya Nairobi, alioa mke wake wa kwanza ambaye ni Grace Wahu.
Kabila lake lilikuwa ni Mgĩkũyũ. Azma yake ya kutaka kuikomboa ardhi ya Wagĩkũyũ ilimfanya aweze kuwaunganisha, naye akawa katibu wao mwaka 1928.
Mwaka 1930 alizuru Marekani na Uingereza ambako aliishi miaka kumi na mitano na hata kuoa mwalimu wa Kiingereza ambaye aliitwa Edna Kenyatta .
fe29c40498ec618a54206ad0acdcd4d6.jpg

Alirudi Kenya mwaka 1946 na alichaguliwa kuwa rais wa chama cha siasa cha Kenya African Union (KANU). Alihamasisha kukomeshwa ubaguzi wa rangi; kuwa na mwamko kisiasa pamoja na mambo mengine yanayompa Mwafrika heshima na utu .
Aliandika kitabu kiitwacho Facing Mount Kenya kilichohusu ukombozi na historia ya Wagĩkũyũ. Alikuwa pia mwanzilishi na mhariri wa gazeti la kwanza kwa lugha ya Gĩkũyũ ambalo liliitwa
Mũigũithania .
Kutokana na kuhusishwa na harakati za vita vya msituni vya kundi la Mau Mau alihukumiwa miaka
saba jela mwaka 1952 . Huwezi kuzungumza historia ya Kenyatta bila ya kuitaja Maumau.
Baadaye alioa mke wa tatu aliyeitwa Mama Ngina Kenyatta ambaye alikuja kuwa mke wa rais wa kwanza na ambaye ndiye mama yake Uhuru Kenyatta , rais wa sasa.
Licha ya Waingereza kuwa na matumaini ya kuwapa wapinzani Waafrika mamlaka "ya wastani" zaidi, ilikuwa Kenya African National Union (KANU) ya Jomo Kenyatta, mfungwa wa zamani, ambayo iliunda serikali muda mfupi kabla ya Kenya kupata
uhuru tarehe 12 Desemba 1963 .
Tarehe 1 Juni 1963 Kenya ilipata madaraka na Jomo Kenyatta alitawazwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya.
a57d17da542d9258d4a9446496c4e075.jpg

Mwaka mmoja baadaye, Kenyatta akawa rais wa kwanza wa Kenya juu ya uanzishwaji wa jamhuri .
Chama kidogo cha Kenya African Democratic Union (KADU), kilichowakilisha muungano wa makabila madogo ambayo yaliogopa utawala wa makabila makubwa, kilijitoa na kujivunja mwaka wa 1964 na wanachama wake wakajiunga na KANU.
Chama kidogo cha upinzani, Kenya People's Union (KPU), kilianzishwa mwaka 1966 , kiongozi wake akiwa Jaramogi Oginga Odinga aliyewahi kuwa
makamu wa rais Kenyatta. KPU ilipigwa marufuku , na kiongozi kuwekwa kizuizini baada ya chachari za kisiasa zilizohusishwa na ziara za Kenyatta katika
Mkoa wa Nyanza . Hakuna vyama vingine vya upinzani vilivyoanzishwa baada ya 1969 , kupelekea Kenya kuwa mfumo wa chama kimoja chini ya KANU.
Kenyatta alifariki mjini Mombasa tarehe 18 Agosti
1978 na kuzikwa jijini Nairobi kwenye jengo la
bunge .

Chanzo :JamiiForums.com
 
Aisee kumbe upinzani wa kina odinga ni wa kihistoria??
 
Hii habari yako imeruka vipengele vingi,Jomo kenyatta urais wa kenya kwake ulikuwa sawa na magufuli waliokota embe dodo kwenye mchungwa!.
Isingekuwa baba yake raila odinga,kenyatta asingekuwa raisi!.
 
Back
Top Bottom