Tutaendelea kulaumu miaka nenda rudi iwapo mfumo wa utawala hautabadilika. Mfumo wa sasa Rais ni kila kitu. Wakuu wa Mikoa na Wilaya na pia Mameya(wenyeviti wa council) na Wakurugenzi hawana kazi zinazotokana na initiative zao. Kila siku wanapokea maelekzo kutoka Dar es Salaam.
Ni lazima tufikie wakati destiny ya maisha ya watu iwe kwa watu wenyewe. Serikali iweke sera, sheria nzuri na kuhakikishiwa ulinzi na usalama.
Tuwe na mfumo mpya wa utawala utakaotoa uhuru kwa mikoa kujipangia maendeleo kwa kuzingatia sera za kitaifa, malengo ya kitaifa na kulingana na rasilimali zilizopo katika mikoa hiyo. Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji ziwe huru pia kufanya mambo yanaihusu.
Tukifanya hilo tabia ya kumtegemea Rais kufanya kila kitu itakwisha.