Kuna nafasi hazipaswi kufanyiwa majaribio,mojawapo ni ya Urais.
Kama alivyosema Mwalimu, urais sio nafasi ya mchezo, unapita mitaani na kuona namna wananchi wako walivyo hohehahe, unasoma magazeti na kuona namna watu wanavyoteketea na magonjwa yanayoweza kuzuilika, unaangalia kwenye runinga na kuona namna wananchi wa nchi nyingine zenye nafuu wanavyofaidika na ustawi wa nchi zao. Urais wa nchi masikini ni kazi ya wito ..
Japo bado wapo wabishi sugu wanaoendelea kuamini kuwa JK ni chaguo la Mungu na atapunguza kama sio kumaliza matatizo ya Tanzania, binafsi sioni dalili zozote za kunifanya niamini hivyo. Hakuna udhati kwenye dhamira za JK. Maisha bora kwa kila Mtanzania ..
Pia nilipomsikia JK akitamka bila uoga kuwa anawajua wala rushwa lakini anawapa muda wajirekebishe nikatambua wazi kuwa huyu jamaa hayuko serious na ahadi zake.
Rushwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo, sasa kwa kuwapa muda wala rushwa wajirekebishe inamaanisha kuwapa idhini wamalizie kula rushwa kabla hawajachukuliwa hatua.
Mwaka umepita sasa tangu JK atoe tamko hilo na hajatupa feedback iwapo hao wala rushwa wameshajirekebisha lakini haihitaji certificate ya uchumi kutambua kuwa nchi yetu inatafunwa vibaya mno.
Kasi, ari na nguvu mpya imeshaonekana: kwenye matumizi yanayozidi mapato. Utabiri wangu ni kuwa JK ataamua kutogombea 2010 baada ya kugundua kuwa urais sio jambo la majaribio. Hopefully,and good for him, atayemrithi atakuwa ni chaguo lake la sivyo atakuwa kiongozi wa kwanza TZ kwenda kunyea ndoo Segerea.
Kama Mtume alivyo shushiwa maandiko matakatifu ndivyo pia sisi Watanzania Mungu ametuletea Mtume na Mwokozi wa Watanzania JK au mnasemaje ?
Mlalahoi,
Hilo dua lako naona umekosa pa kulielekeza. Yaani JK aachie hatamu za utamu thubutu! Nakuhakikishia hata 2015 kutakuwa na watu wanapendekeza abadilishe katiba ili aendelee tena.
Ninachoweza kubashiri hapa ni kuwa 2010 atakuja na maneno haya "nipeni tena miaka mitano niweze kumalizia kazi niliyoianzisha"
Wanaoweza kumfanya asigombee ni watoto wake ambao wanafika hapa jambo JF, Tafadhali mwelezeni Pops aitendee haki Tanzania kwa kuachia ngazi 2010. Kama ni hamu ya Urais si imeshaisha?
bajeti ya mwaka ujao wa pesa TRILLION 5.2 ..hiyoo inakuja ,sijui hii deficit ya mwaka huu 1.3 trillion projected till june wamejumlishia huko?
Kuna wengi humu Jambo Forums walishangilia sana JK alipoibuka mshindi Dodoma.
JK alipoanza vibaya sana kwa kutangaza baraza la mawaziri 60, nilitabiri kwamba kabla hajamaliza miaka 2 madarakani, kasi ya mfumuko wa bei itazidi 10% kwa mwaka. Nilitabiri vile kwamba kabla hajamaliza miaka 5 ya kwanza, tutafikia kasi ya mfumuko wa bei ya karibu 20% kwa mwaka.
Takwimu alizotoa Waziri wa Fedha wakati huu ni kwamba kasi ya mfumuko wa bei imeshafikia 7.3% (Ilikuwa 4.5% JK alipochukua nchi). Kasi ya kukua kwa pato la taifa ilikuwa 7.2% JK alipochukua nchi na tayari imeshuka hadi 5.8%. This 1.4% decline in GDP growth rate translates into a decline in the rate of growth of the national wealth by some 56bn/- each year.
Tutasingizia njaa na mafuta mpaka lini?
Augustine Moshi
Viongozi wa dini ni watu wa ajabu sana. Ndio walishawishi waumini wao kuwa JK ni chaguo la mungu! Hawakutaka kungalia sera wala uwezo wa mgombea.Matokeo yake wamewatumbukiza waumini wao katika umaskini wa kutisha.
sasa Rais afanye nini, mimi naona yuko njia panda! Asipoingilia kati watu wata muona hawajali na hatimizi ahadi zake, akiingilia kati wengine watasema anaingilia kazi za watu wengine na anaweza "kususiwa". Sasa kama ungekuwa wewe ndiyo Kikwete ungefanya nini?
Mzee Moshi,
Aliyempa Muuungwana urais kwanza ni rais mwema na mtukufu wa zamani Mkapa, na baadaye sisi wananchi tukampigia kura, baada ya kuambiwa na mtukufu Mkapa kuwa anafaaa, au?
JK akitawala miaka 10, atatuachia uchumi mbaya kuliko hata ule uliokuwepo wakati Mkapa anaingia madarakani.