Wananchi unaowangoza wanapoamua kuangalia mpira wa ulaya badala ya kusikiliza hotuba ya kiongozi wao wa nchi hapo ujue kuna walakini wa uongozi na sio chuki binafsi kama unavyodhani. Kiongozi anatakiwa azungumzie mambo yanayowagusa maisha ya wananchi kwa mfano; jinsi serikali inavyosaidia kupambana na ugumu wa maisha badala ya kusifu umahili wa mbwa wapolisi wakati wa sherehe za muungano!!Mkuu, hata kama ungekuwa wewe ungeianzaje hotuba? Embu tupe demo ungetuambia nini!.
kuna points za maana sana aliziongelea jana hasa lile la mafuta. Watu washaanza kugombania mafuta wakati watafiti kwa zaidi ya miaka 56 hawajaona dalili.
Wakati mwingine tupunguze chuki binafsi.
kuna points za maana sana aliziongelea jana hasa lile la mafuta. Watu washaanza kugombania mafuta wakati watafiti kwa zaidi ya miaka 56 hawajaona dalili. Wakati mwingine tupunguze chuki binafsi.
Hata mimi nilipenda sana huu ufafanuzi alioutoa kuhusu mafuta.
Jana nilisikia wimbo wa taifa ukiimba, nikakurupuka kutoka nje nilipokuwa naoga.......
Kufika tu nakuta Mkubwa anaanza kutoa hotuba zake kama kawaida....
NDUGU WANANCHI HIVI PUNDE TUMETOKA KUSHUHUDIA SHEREHE ZA MUUNGANO, KWAKWELI ZILIFANA SANA NA NAMPONGEZA PINDA KWA MAANDALIZI MAZURI, TOFAUTI NA MIAKA MINGINE TULIKUWA NA MAONYESHO YA MBWA, WALIKUWEPO WATU WALIOZALIWA MIAKA 45 ILIYOPITA WAKATI WA UHURU....... MARA SWEETHEART AKAKURUPUKA HUKO ULIKOKUWA "wewe twende tukalale unasikiliza upuuzi gani? Mwanaume badala ya kuongea vitu vya maana kama dhana nzima ya Muungano anasifia sherehe.........." TV IKAZIMWA........ SIKUJUA KILICHOENDELEA MWENYE POINTI/PUMBA ZAIDI anaweza kutuambia nini kiliongelewa????

Sore, lakini mkeo alikuwa na zaidi ya hiyo hotuba kwani kila kitu kina preamble. She was horny! si vingine. Hotuba ilikuwa ya muda mrefu tu na kuna vitu vingi viliongelewa humo na vya maana tu. msimhukumu JK!!
Hata mimi nilipenda sana huu ufafanuzi alioutoa kuhusu mafuta.
I love this forum.... na shime turudi kule 2006/7 na tupekenyue yote aliyosema tulinganishe pumba na mchele
Ni kweli kuna kasoro kadhaa ambazo zimejitikeza katika ungozi wa JK ila nafikiri hayo ni mapungufu ya kawaida ambayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa aidha na baadhi ya watendaji ambao wamekosa umakini au walichelea kutimiza wajibu wao hivyo kusababisha yatokeee hayo yote. Mimi nionavyo Jk bado ni kiongozi anayejitahidi kutimiza majukumu yake ila huenda ana watu ambao hawatimizi majukumu yao sawasawa hivyo kumfanya Rais adhalilike bila sababu za maana:frusty:
Ama kweli huu ni Usanii!
Sasa hawa mawaziri waliotufungia kanyaboya mndio wameisha save au sio. Msabah na umeme bandia alitakiwa kuchukuliwa hatua na sio kuhamishwa wizara. Navyofahamu Wadanganyika wepesi wa kusahahu na kusamehe, kesho utasikia watu wakimlaumu Karamagi.
Mkuu ukitaka kuyapekenyua yote yaliyosemwa unaweza kutokwa na machozi
but let me ask you one thing guys. Hivi mnajua kwamba hata ashuke malaika kutoka mbinguni kuja kuwatawala watanzania bado hali hii ya manung'uniko, ho sijui viongozi ni wabaya na mengineo, haitakwisha? watanzania tuwe serious na maisha especially katika level ya familia na katika jamii inayotuzunguka. Kitu kimoja ambacho mimi ninaamini katika hicho ni kwamba hata wanoongozwa wana asilimia 90 ya kufanya uongozi uwe mbaya na wa kuchosha kwa wale wanaowaongoza. Sasa niulize tena swali jingine ni nani mnayemzania anaweza kuiongoza hii tanzania kuelekea kwenye kilele cha mafanikio? ni wewe au ni yule? mwizi au polisi magereza? mgonjwa au daktari ni sisi sote achane na mambo ya kupoteza wakati na badala yake fanya kazi kwa bidii na pale inapobidi chukuwa hatua ya kuwa wewe kiongozi kuzuia matukio ya kizembe.
mfano mzuri ni huu hapa kikwete na serikali yake ndio huwa ina agiza wauwaji wa wa albino kufanya vitendo vya kishetani? au yeye ndie anaye apanga njama na wote wanafanya ushenzi ushenzi wao na hatimaye wanalalamika maisha magumu kutokana na uongozi mbaya.
Nasema wewe mwananchi tena mkulima na mfanyabiashara iweni waadifuli kwanza ndio viongozi wenu watakuwa waadilifu