BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameurudisha bungeni muswada wa sheria ya sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini humo. Msemaji wa Rais, Bw.Sandor Walusimbi amesema, Rais Museveni amependekeza marekebisho ya adhabu kwenye muswada huo kabla hajausaini.
Kwa sasa muswada huo unatoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Mapendekezo ya Museveni ni kuwepo na "uwanda mpana" wa adhabu kulingana na ukubwa wa tatizo. Wale walio tayari kubadilika na kuachana na vitendo hivyo wapewe adhabu ya kifungo hadi miaka 30 jela na wakitoka wawe chini ya uangalizi maalumu, huku wengine wakifungwa hadi kifungo cha maisha. Wanaume watakaolawiti watoto, au mashoga na wanawake watakaowarubuni watoto wawaingilie kinyume na maumbile watanyongwa hadi kufa.
Kuhusu haki za binadamu Museveni amesema "Mungu aliwaumba binadamu lakini waliposhiriki ngono za jinsia moja (Sodoma na Gomora) aliwachoma moto na kuwateketeza. Leo watu wanataka kumfundisha Mungu kuhusu haki za binadamu aliowaumba mwenyewe? Inachekesha. Hivi kuna mtu mwenye kujua haki za binadamu kuliko yeye aliyewaumba? Kama yeye aliwachoma moto, mimi kuwafunga jela bila shaka nimewachagulia adhabu nafuu zaidi"
Marekebisho mengine kwenye muswada huo yanahusu ngono za mdomo (oral sex). Museveni amesema litakua kosa la jinai kwa mtu yeyote kufanya ngono kinyume na njia ya asili (against the order of nature). "Mungu aliumba mdomo kwa ajili ya kula na kuongea, sio kufanya ngono. Ndio maana mdomo upo hadharani na sehemu ya kufanya ngono ipo faragha" amesema Museveni.!