Jambo la maana ni kupiga vita ngono.
Kama hakuna ngono za ovyoovyo mimba kamwe hazitaongelewa.
Kupinga kutoa mimba bila kuwa mstari wa mbele kupinga ngono kwa wasio na leseni au mkataba unajumuisha ngono(ndoa) ni ujuha tu.
Mimba inapatikana baada ya watu wawili kuingiliana kimwili. Kwa hiyo kama kutoa mimba ni uuaji kuto pinga ngono waziwazi ni uuaji pia.
Walio mstari wa mbele kutetea uhai katika kila hatua wana mpango gani kabambe wa kuhakikisha mimba hazitungwi?
Kupinga kutoa mimba ni kupinga matokeo ya kitendo kilichofanyika cha kutunga mimba. Kitendo cha kukutana kimwili kinyume na maadili taratibu na kanuni za jamii ni kitendo kisicho kubalika. Kusubiri mpaka watu wawe na mimba ndipo mashairi ngonjela na maandamano yaanze kufanyika kuingilia na kupinga maamuzi binafsi juu ya mimba za watu, ni sawa kabisa na kusubiri mtu aumwe na mbu na kupata malaria ndipo uamuzi wa kumpa dawa uanze kutolewa. Kwa nini nguvu isiwekwe katika kuongeza juhudi za kuzui mazalia ya mbu au kukinga watu wasiumwe na mbu?
Kwa nini juhudi zisielekezwe katika kupinga ngono?
Kwa nini nguvu zinaelekezwa kupinga matokeo badala ya kupinga chanzo?
Watu wanaodai wako pro life wana uchungu na vimbe walioko matumboni mwa wanawake tu. Watu hawa hawana huruma wala simanzi juu ya watoto wazaliwao na kukosa malezi bora kwa sababu wamezaliwa kwa matamanio ya kimwli zaidi, kuliko nia ya kuwa na watoto.
Hakuna mipango wala taratibu zilizo wekwa wazi na wapingao kutoa mimba kuhakikisha kila azaliwaye atalelewa na watetezi hawa wa uhai.
Hapa Marekani, mijitu inayo jita pro life inapinga kwa nguvu zao zote hoja ya kila mtoto kuwa na health Insurance. Watu waovu hawatambuliwi kwa maneno wanayoongea wanatambuliwa kwa vitendo vyao. Huwezi kupinga kwa nguvu zako zote akina mama wasitoe mimba kwa sababu kitendo hicho ni uuaji, halafu wewe pia ukasimama kidete ukapinga kwa nguvu zote kuwapa Health insurance watoto waliozaliwa kutokana na kupinga kwako mimba zisitolewe. Unaweza fanya hivyo tu kama una ubia na Ibilisi wa kuzimu au ni balozi wake wa kudumu hapa duniani.
Mtoto akifa kwa sababu hana Bima ya afya wewe unayejiita Pro life mbona mikelele yako haisikiki kulaani mauaji ya kukusudia?
Akiwa tumboni ulimtetea aiuawe, sasa amezaliwa wewe bado unatetea mimba na kujifanya matatizo ya huyu aliye zaliwa hayakuhusu wala si kazi yako kupinga taratibu mbovu za jamii zitumike kuutoa uhai wake.
Mtoto akizaliwa ni kazi ya mama aliyemzaa kwa sababu ni wake na sheria zote zinamfanya mzazi kuwa msemaji wa mtoto huyo. Lakini akiwa tumboni mwa huyo mama kuna watu wanadai wana haki ya kusema juu ya mtoto huyo, hii inaleta kizunguzungu cha mawazo.
Msukumo wa kutetea uhai unaishia kwenye mimba tu?
Kundi la watu wanaotetea mimba liko mstari wa mbele kutetea mimba zisitolewe tu na kamwe haliko mstari wa mbele kutetea kwa nguvu zao zote watoto wanaolelewa na mzazi mmoja wahakikishiwe malezi bora. Ni kundi jingine kabisa la watu linalojitokeza kuwasaidia watoto wa mitaani na watoto walio na malezi haba kutoka kwa wazazi wasio kuwa tayari kuwa na watoto.
Watoto kwa mamilioni wanakufa kila pembe ya dunia kwa kukosa huduma, huku mijitu inayojiita ni pro life ikilalama kutetea mimba na si kuuunda mipango na utekelezaji wa kuhakikisha mimba walizozitetea miaka iliyopita zinapata huduma zote ili ziendelee kuishi bila shida.
Watu wanaotetea uhai ni lazima waje na plan nzima ya kuhakikisha kwamba kila mimba wanayoitetea mtoto anayezaliwa anawekewa mipango inayotekelezeka ya kuhakikisha anaishi kama mtu na si kivuli katikati ya jamii.
Vinginevyo, Pro life wote ni wasemaji/ wanasiasa wazushi wanao ukataa ukweli kwamba matamshi yao ya kutetea uhai ni propaganda za kuwafanya wajinufaishe kiuchumi na kijamii kwa kisingizio cha kutetea uhai.
Pro life hao hao ni wepesi kuanzisha Vita na kusindilia watu jela kwa sababu zisizokubalika hata kwao wenyewe. Pengine utetezi wao wa kupinga utoaji wa mimba una nia ya kuwa na kundi kubwa la watu ili Jela zisikose watu na vita wanazozianzisha zisikose watu wa kuwapeleka wakafe kwa jambo wasilolijua.
Wanamwingiza Mungu katika jambo hili wakati Mungu wanaye mtaja wanamkana katika matendo yao yote.
Pro life inaishia kwenye mimba tu, kwangu huo ni upuuzi wenye ushenzi ndani.