Huyu ni Brother Peter wa Shirika la Mtakatifu Fransisko,Katoliki ambaye ameshinda tuzo ya dunia ya Mwalimu Bora.

lukubuzo Samsis

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2014
Posts
2,920
Reaction score
3,388
Huyu ni Brother Peter wa Shirika la Mtakatifu Fransisko,Katoliki ambaye ameshinda tuzo ya dunia ya Mwalimu Bora.

Brother Peter ni MWALIMU wa sayansi kutoka moja ya vijiji nchini Kenya, ambaye hutoa sehemu kubwa ya mshahara wake kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi masikini zaidi, ameshinda tuzo la dola milioni moja ($1m ) kwa kuwa mwalimu bora zaidi duniani.

Brother Peter Tabichi, anayetoka katika Shirika la Mtakatifu Fransisco,Katoliki ameshinda tuzo ya dunia ya mwaka 2019 ya mwalimu bora.
Brother Peter amesifiwa kwa mafanikio yake katika shule yenye madarasa yenye watoto wengi pamoja na vitabu vichache.

Anataka kuwaona watoto wa shule kuiona "sayansi kama njia ya kufuata " kwa ajili ya siku zao zijazo.
Tuzo hiyo ilitangazwa katika sherehe iliyofanyika mjini Dubai, ambapo alitambuliwa kama mwalimu aliyejitolea kufanya kazi "isiyo za kawaida "kwa watoto katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la bonde la ufa nchini Kenya.
Brother Peter Hutoa 80% ya mshahara wake kuwasaidia watoto, katika shule ya kutwa ya sekondari ya wasichana na wavulana ya Keriko iliyopo katika kijiji cha Pwani Village, kaunti ya Nakuru, ambao vinginevyo wasingeweza kupata sare za shule na vitabu. (Chanzo: BBC)

www.radiomaria.co.tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwenye roho mbaya hii tunzo siwezi kuipata.🀣🀣


Ndukiiiii πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Hongera sana mtanzania mwenzetu.

Wakenya msije na povu.

Huyo ni kama mlima Kilimanjaro tu mkiwa Kenya mnaouona... Na sisi Tanzania huyo mwalimu tunamuona pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwalimu ni mwito. Amehojiwa na bbc na amesema atatumia fedha kuboresha shule na kugharamia miradi midogo midogo ya Jamii majirani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…