Huyu ni Freeman Mbowe yupi? Yule wa bunge la katiba? Au huyu wa sasa kibogoyo asiyeweza kung'ata?

Huyu ni Freeman Mbowe yupi? Yule wa bunge la katiba? Au huyu wa sasa kibogoyo asiyeweza kung'ata?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
HUYU NI MBOWE YUPI?

Huyu MBOWE wa CHADEMA hii ya baada ya kutoka Ikulu kuongea na MAMA kwa siri; sio yule Mbowe wa CHADEMA ya Bunge Maalum la Katiba.

Huyu ni MBOWE mwingine kabisa na wa tofauti; ambaye ameifanya CHADEMA ya sasa iwe Kibogoyo isiyoweza tena kung'ata. Hovyo kabisa!

Yes! Ni MBOWE asiye na kauli ya kuonyesha njia ya kuing'oa CCM kama Kiongozi Mkuu wa Chama.

Maoni na mtazamo wangu binafsi kwa fact bila kupepesa macho,naomba nimkumbushe wazi Freeman Mbowe kwamba; CCM ni wajanja na wanataka kumuingiza chaka, waipoteze CHADEMA kwenye ramani ya vyama vya upinzani vyenye nguvu ya kisiasa na ushawishi hapa barani afrika,

Pengine Freeman Mbowe anataka ale pesa zao halafu awalie timing,hiyo haitafanya kazi, nimdokeze Mbowe kwamba,CCM wanapambana sana ili uwe mgombea Urais CHADEMA 2025 ili baadae wakupe nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali mpya kabisa ya Umoja wa Kitaifa ya JMT itakayoundwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Sasa nikueleze tu Bwana Mbowe kwamba,mgombea sahihi wa Urais ambaye CCM wanamuogopa na ambaye ataivusha nchi hii kwa sasa, kwenye Uchaguzi ujao 2025 ni TUNDU LISSU.

Nishauri pia,

Baada ya wewe kustaafu kuiongoza CHADEMA unaonaje Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa awe Tundu Lissu, Katibu Mkuu awe John Mnyika na Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara awe John Heche?

Asanteni sana, Mwenyezi Mungu awabariki sana!

Kwa nini namtilia wasi wasi Freeman Mbowe?

1.
Kikao hiki kilipaswa kuitishwa siku ile mwili wa ALI KIBAO ulipookotwa na kuwekwa mochwari pale Mwananyamala.

Otherwise kama ingeshindikana, basi Kikao hiki kingeitishwa kule Tanga Mjini.

Sikilizeni, ukiona Kikao cha CHADEMA kinaitishwa kipindi hiki na kufanikiwa kukutana, ujue hakuna hoja yenye madhara kwa dola na lazima dola imeshajua ama kujulishwa kwa siri kinachokwenda kujadiliwa na kutolewa kwa waandishi wa habari.

Haya ndio mojawapo ya madhara ya wenzenu ku-compromise kwa adui kwa siri sana.

Tazama Mkutano wa BAVICHA Mbeya uliokuwa na harufu ya GenZ ambao Serikali liona kama "nia ovu" ulivyodhibitiwa fasta na mchezo ukaisha.

Kwa tension (taharuki) iliyopo hivi sasa ndani ya Taifa hili; kama Kikao/Mkutano huo wa CHAMA na Mabaraza ya Kanda ya Pwani ungekuwa na AGENDA yenye maslahi yenye seriousness kwa CHADEMA; hakika akina Masauni wasingekubali Kikao hicho kifanikiwe.

Hoja sio kuhusu uhalali ama umuhimu wa Kikao hicho, hoja yangu ni hizi technicalities za kishenzi zinazofanyika ndani ya CHADEMA kwa manufaa ya dola ya Mama kisa tu kuna watu kadhaa wanatumikia mgao wake.

Very shame!

Madhara ya DOLA kuwateka watu wenye nguvu za maamuzi kwenye Chama cha Siasa chenye nguvu ni makubwa na usipotuliza akili huwezi kuyaona kwa macho.

Lazima uwe na jicho la 3 ndipo uweze kuyaona madhara husika.

Mojawapo ni MATAMKO ya Chama kutokuwa na nguvu yoyote ile ama kukosa MATOKEO Chama. Hii ndio ile CHADEMA iliyokuwa ikitoa TAMKO Serikali inahaha.

Leo hii Mwana-Chadema anauawawa na mwili wake unapelekwa mochwari; Spika wa Bunge anapost picha za michezo ya Bonanza lake huku anacheka hata hawazi?

Rais wa nchi anatoa statement dhaifu kama ile. How it comes. Hii ndio ile CHADEMA tuliyoijua?

Mtendaji wa Chama anauawawa kikatili halafu M/Kiti wa Chama anazungumza kishikaji tu halafu suala linaishia hapo tunarudi Dar es Salaam kuita Mabaraza ya Chama.

For what?

Jambo la pili ambalo FREEMAN walikubaliana na Mama kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wao wa migao ya zile fedha alizozikataa Lissu ni kuhakikisha Lissu hapati nafasi ya kugombea Urais 2025; labda wabadili gia angani kwa sababu jambo hili limekuwa na kelele nyingi sana kila kona.

Badala yake; Mama wakakubaliana na FREEMAN kwamba; yeye mwenyewe (FREEMAN) agombee Urais ili baada ya Uchaguzi wa 2025; Mama na watu wake wataunda Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na FREEMAN atakuwa Makamu wa Pili wa Rais wa JMT kwa maana uundwe mfumo kama ule Zanzibar kwenye Serikali ya Muungano ili hii nafasi ya Makamu wa Pili iwe inatumika kuwapooza wapinzani kwa lengo la kulinda uhai wa CCM madarakani kama walivyofanikiwa kule Zanzibar.

Kwa hiyo; hivi sasa FREEMAN na genge lake wanatumikia maelekezo ya Mama kwa siri sana kupitia mgao uliotembezwa kwa wale wote waliokubali kuchukua chao.

Wanatekeleza mambo matatu muhimu anayoyataka Mama; nayo ni haya;

1. Malalamiko ya Covid 19 kutaka warudi kwenye Chama yafanyiwe Kazi na makubaliano yalishafanyika kati ya Mama na Freeman, shida ni akina Lissu, Mnyika, Heche, Ngoto, Pambalu na wengine kadhaa hawataki huo ushenzi utokee; bora wao wafe.
2. Freeman ahakikishe Lissu hapati nafasi ya kugombea Urais 2025 na badala yake Mbowe mwenyewe agombee ili baada ya Uchaguzi awe Makamu wa Pili wa Rais wa JMT.
3. FREEMAN ahakikishe anapooza zile Siasa za kukamia mpaka Umoja wa Mataifa ili Mama na watu wake wasinyimwe misaada na ndio maana mnaona wasaidizi wa Mama hata wakisikia mtu wa CHADEMA ameuawa ama ametekwa hata hawajali wala kushtuka maana wanajua mchezo ushaisha.

Tunzeni haya kama rejea za baadae huko mbeleni tuendako.
 
Madhara ya DOLA kuwateka watu wenye nguvu za maamuzi kwenye Chama cha Siasa chenye nguvu ni makubwa na usipotuliza akili huwezi kuyaona kwa macho.

Lazima uwe na jicho la 3 ndipo uweze kuyaona madhara husika.

Mojawapo ni MATAMKO ya Chama kutokuwa na nguvu yoyote ile ama kukosa MATOKEO Chama. Hii ndio ile CHADEMA iliyokuwa ikitoa TAMKO Serikali inahaha.

Leo hii Mwana-Chadema anauawawa na mwili wake unapelekwa mochwari; Spika wa Bunge anapost picha za michezo ya Bonanza lake huku anacheka hata hawazi?

Rais wa nchi anatoa statement dhaifu kama ile. How it comes. Hii ndio ile CHADEMA tuliyoijua?

Mtendaji wa Chama anauawawa kikatili halafu M/Kiti wa Chama anazungumza kishikaji tu halafu suala linaishia hapo tunarudi Dar es Salaam kuita Mabaraza ya Chama.

For what?
 
Kwa tension (taharuki) iliyopo hivi sasa ndani ya Taifa hili; kama Kikao/Mkutano huo wa CHAMA na Mabaraza ya Kanda ya Pwani ungekuwa na AGENDA yenye maslahi yenye seriousness kwa CHADEMA; hakika akina Masauni wasingekubali Kikao hicho kifanikiwe.

Hoja sio kuhusu uhalali ama umuhimu wa Kikao hicho, hoja yangu ni hizi technicalities za kishenzi zinazofanyika ndani ya CHADEMA kwa manufaa ya dola ya Mama kisa tu kuna watu kadhaa wanatumikia mgao wake.

Very shame!
 
Kikao kilichoitishwa kilipaswa kuitishwa siku ile mwili wa ALI KIBAO ulipookotwa na kuwekwa mochwari pale Mwananyamala.

Otherwise kama ingeshindikana, basi Kikao hiki kingeitishwa kule Tanga Mjini.

Sikilizeni, ukiona Kikao cha CHADEMA kinaitishwa kipindi hiki na kufanikiwa kukutana, ujue hakuna hoja yenye madhara kwa dola na lazima dola imeshajua ama kujulishwa kwa siri kinachokwenda kujadiliwa na kutolewa kwa waandishi wa habari.

Haya ndio mojawapo ya madhara ya wenzenu ku-compromise kwa adui kwa siri sana.

Tazama Mkutano wa BAVICHA Mbeya uliokuwa na harufu ya nia ovu ulivyodhibitiwa fasta na mchezo unaisha.
 
Nataka kusema nini kuhusu haya maandamano ya CHADEMA ya tarehe 23 Septemba, 2024?

Kiufupi, binafsi naunga mkono wito wa maandamano haya kwa asilimia zote kwa sababu ni tukio linalokwenda kuakisi mwangwi wa sauti ya haki hususani haki ya msingi sana ya kuishi ambayo ndio haki namba moja kuliko haki zote zilizotajwa kuanzia pale kwenye ibara ya 12 hadi kwenye ile ibara ya 29 ya katiba ya nchi yetu.

Na kwa jicho langu la tatu; nayaona maandamano haya yakienda kupewa baraka zote na Jeshi la Polisi na pengine awamu hii, ile intelejensia ya Jeshi la Polisi; huenda haitaona vile viashilia vya uvunjifu wa amani ya nchi kwa sababu zifuatazo;

1. Jeshi la Polisi watataka kulitumia tukio hili la maandamano ya CHADEMA kama eneo muhimu la ku-mantain hii status ya sintofahamu ya umma dhidi ya hizi kelele za utekaji na mauaji ya watu.

2. Watayaruhusu maandamano haya yafanyike ili kupunguza sumu za watu zilizojaa vifuani na hii ni mojawapo ya mbinu za dola katika kulifanya Taifa liweze kupumua pale mamlaka za kiusalama zinapogundua kwamba, Taifa limevimba.

Yes! Ukisoma vitabu vya masuala ya kiusalama kwenye nchi ama taifa; na mbinu za watawala katika kukwepana na umma wenye jaziba na hasira kali utanielewa namaanisha nini hapa.
 
Back
Top Bottom