Huyu ni mume au mzigo?


Lakini AshaDii, nimesema hivi, anafanya kazi na anapata mshahara, ila mshahara wake anautumia kwa pombe na umalaya au vyoye viwili.... ina maana hata kama amekusomesha na kukutengenezea future jambo ambalo kimsingi ni wajibu wake.......kwa hiyo itakuwa ni halali kwake kutowajibika katika familia na kuelekeza fedha zake katika pombe na umalaya?
 
Kuna msemo huu: "Kazi mbaya kama unayo". Mi nasema, mume mbaya kama unae! Ukiwa na mume, utaimba kila siku kwa mashosti-mara ooh, hajui kazi, mara ooh anahema sana, mara ooh amekuwa bonge siku hizi mara ooh wangu ni mwanaume suruali! Ukiwa unatafuta mume, unaenda hata kwa waganga wakienyeji wakuongezee masaburi ili upendeze na watu wakuoe!! Ndio maisha, hatujui thamani ya kitu mpaka kipotee/kiondoke!
 
Ningemuacha aendelee na maisha yake na mimi ningeendelea na yangu.
 
Kweli shetani wa mtu ni mtu mwenyewe sikatai kuna familia nyingi zinazoishi katika maisha kama haya ila ukweli sifurahishwi na hizi tabia naomba Mungu atuepushe na hii tabia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…