Baada ya kupata taarifa kwamba Simba wanamleta straika kutoka Senegal aitwaye PAPA NIANG (mdogo wake Mamadou Niang), nilimwangalia kwenye Youtube na kugundua kwamba ni mkali. Jamaa anapiga mashuti makali kwa kutumia miguu yote miwili, na pia ni msumbufu kwa mabeki kama alivyokuwa Emmanuel Okwi. kama kweli Simba watampata straika huyu, watakuwa wamelamba dume. Tatizo ni kwamba viongozi wa Simba huwa wepesi ku-spot wachezaji wazuri halafu baadaye hawawapati sababu ya ubahili.
Mkali ka serunkuma?
hueNDA NI KIPANDE ALICHOCHEZA VIZURIHata ukimuangalia serunkuma kwenye you tube utamuona mzuri kumbe ana llt
wachezaji wote wanaohusishwa kusajiliwa na mikia tunaambiwa ni hatari halafu baadaye wanaishia kukatwa tu
....mrundi ndyaisenga ameshakatwa tiyari sasa hivi anakunywa kahawa ya bujumbura,,,inaelezwa jamaa amekataa pesa ya mboga mliyotaka kumpa akasepa zake,,hamis kiiza hajiamin amin na yeye mda wowote anaweza katwa kama maguli
sijalielewa vizuri suala la Kiiza
Kuhusu kiiza ninauhakika simba imeingia mkenge,huwezi kusajili mchezaji aliyekaa idle bila kucheza mechi za ushindani msimu mzima ukatarajia matunda....hata hivyo pia kiwango chake kilikuwa kimekwisha tangu akiwa na yanga
"anayejua anajua tu" - wahenga
Ok basi wamchukue huyu,anajua
Huyu si kashastaafu Mkuu? Sisi tunasajili wanaojua ambao mpaka sasa wanasakata gozi la ng'ombe.
Hata kiiza alikiwa amestaafu,kwani mmemtoa tim gani mkuu
Sasa kwanini unabishana na wanaojua..Sikumbuki Mkuu.. Ngoja nifuatiliie, nitakuja na jibu mda si mrefu.