mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,555
- 6,972
Kuuliza si ujinga, wengine utaalamu wetu ni kwenye kuhesabu pesa counter, Je kitendo cha huyo Traffic kumkaribia Rais namna hiyo sio Security Breach?
Ukiangalia kwa umakini alikaribia mno tena kupita nyuma ya hao Walinzi wenye silaha nje nje, kwa akili zangu za kawaida naona hatari maana kama mtu mbaya na mwenye mafunzo anapita karibu hivyo anaweza kuwapokonya hao akafanya fujo
Lakini pia baada ya kuambiwa huku usipite pita huko akamgusa huyu afisa mmoja kiunoni kwa nyuma kiasi anaweza kugusa silaha iliyofichwa mfukoni.
Na kuonesha kuwa halikuwa jambo la kawaida, amevuta attention ya karibu wana usalama wanne mpaka watano mpaka waliokuwa karibu kabisa na Rais, kiasi wamegeuka na kumtizama kwa sekunde kadhaa wakati anaondoka, hata huyo Kamanda aliyepigiwa saluti hajamuelewa kabisa huyo askari kamuangalia kwa mashaka.
Hiyo haiwezi kuitwa Security Breach au ni kawaida tu