Huyu Wenger vipi? Atishia kujinyonga angefungwa na Chelsea!

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametishia kujinyonga iwapo kikosi chake kingefungwa na Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu jana Jumatano.
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya mabao 2-2 huku Wenger akisema kwamba iwapo Chelsea wangebebwa tena kwa namna yote ile kisha kuibuka na ushindi angejinyonga hadi kufa.
Wenger alibainisha kwamba uamuzi wa kuipa Chelsea penalti na kupata sare ya 2-2 kwa upande wake anaona jambo hilo halikuwa sahihi.
Mwamuzi wa mchezo huo, Anthony Taylor hakusita kutoa adhabu ya penalti baada ya Eden Hazard kuchezewa vibaya na Hector Bellerin.
Alisema penalti hiyo iliwaathiri kwa kiasi kikubwa kwa sababu kulikuwa na mazingira a kuelekea kupoteza mechi hiyo huku akisema kwa maamuzi ya aina hiyo mwamuzi anaweza kujikuta anagawa hata penalti 10 kwenye mechi moja.
 
huyu Wenger anatufanya mashabiki wa arsenal tuwe wanyonge mbele ya timu za hovyo hovyo kama man u
Kaalikwa na Mchezaji wake wa Zamani WEAH, huenda Mh Rais atamshauri kitu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…