Tangu nianze kufuatilia kwenye luninga mambo ya michezo Mi naonaga kama hivi vilabu bingwa ya mabara inachezwaga Japan tu? Mwenye kujua anijuze jamani Wanamichezo haswa wa mpira wa miguu wa JF! Ninawasilisha!
Si wangeporomoti kwingine licha ya kwenda taifa kubwa kama lile maana kuna kipindi kampuni ya Toyota nayo ilihusika sana! Hata FIFA Mi naona hata ufisadi umetanda humo. Heri hata wangepeleka India!
Si Japan tu mzee. 2000- Brazil. 2005/6/7/8- Japan. 2009 na 2010- UAE. 2011 yamefanyika Japan na pia 2012 yatafanyika Japan. 2013 na 2014 yatafanyika Africa katika nchi ya Morocco
Mtoa mada yaelekea ni mgeni kwenye mambo ya Soccer sio mbaya kumuweka sawa Manake hata Mimi nilistuka kukuta swali hili Ina maana hata ile fainali waliyocheza TP Mazembe hakujua ilichezewa wapi! na kama angekumbuka Man utd Ilipoenda Brazil na jezi chache babu fergi akagoma wachezaji wake kuchange jezi na timu zingine...