Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Wakuu kunasiku nilipost humu kuhusu Hydroponic techinology, Ila kama ilivyo kawaida yetu thread kama hizi huwa watu wanapotezea, Ila ukweli ni kwamba hii tekinolojia ni nzuri sana na inaweza kuwa ndo suluhisho pekee mpaka sasa la chakula cha mifugo.

Inaweza kukupunguzia gharama za chakula kwa 50% na kama tunavyo jua kwenye ufugaji hasa Kuku chakula kinabeba hadi asilimia 85 ya gharama zote za uendeshaji wa kuku.


Kanga wakiwa wanakula Hydroponic fodder.

Kuku wakila hydroponic fedder.

HYDROPONIC FODDER inaweza tumika kulishia aina zote za mifugo na hii ni njia rahisi sana na isiyo kuwa na gharama sana.





 
Wakuu Hydroponic si kwamba ni zao, ni sayansi ya kuotesha mazao kwa kutumia maji na nutrients zingine, yaani hutumii udongo kamwe, na unaweza otesha hata Mboga za kula kwa hii sayansi,

Na mara nyingi inatumika kuotesha vyakula vya mifugo, kuotesha, nyanya, mboga za majani, na baadhi ya matunda.

HYDROPONIC FODDER-Ni kulima/kuotesha chakula cha Mifugo kama vile, Kuku, Mbuzi, Cow, kondoo na kazalika, ila kama ni mboga inaweza itwa hydrponic tomatoes na kazalika,

Hapa jamaa kaotesha mboga zake na anaweza uza bila tatizo



majani ya mifugo

Chakula kama hiki wanaweza kula kuku, Ng'ombe, mbuzi na hata kondoo

HYDROPONIC FODDER, Mara nyingi inapendelewa ioteshwe ngano ya bia au Barley hii ndo ina nutrients zote kiasi kwamba utapata energy, protein, vitamini na kazalika, ingawa hata oats inaweza oteshwa ao hata wheat.
 
Kama nikitaka kuanza kulima hayo majani huko ndani ya vibobo/karai ninaweka nini ili mbegu imee.
Na huchukua muda gani kukomaa?
Je maji yanahitaji kubadilishwa au ndio hayo hayo mpaka mavuno.

Mkuu si kila chombo kinafaa kuoteshewa na ni lazima chombo kisicho ruhusu kutu, au bacteria na gangasi ambao ni hatari sana kama wataingia kwenye hayo mazao.

Mkuu inachukua siku 9 kuweza kuwa imekamilika kwa ajili ya kuwapatia NG'OMBE na kwa kuku ni siku tatu inatosha kabisa.

Maji unakuwa unaongeza ila si mengi sana, ila kama unalima mazao ya muda kama nyanya ndo unakuwa unayabadilisha na si kuyabadilisha unaweza fanya resaiko,

HAYO MAJANI UNAYO YAONA HAPO NDO YAMEFIKIA KUTUMIKA SI KWAMBA NI MPAKA IKOMAE IKAUKE NO,
 
Pia mwaweza kufungua youtube,"kilimo biashara"kuna maelezo kuntu.
nimikuwa nikifatilia hiki kilimo... sasa hivi singapore wanahamia katiki 'wertical farming'.... plot ndogo ...wanainua ghorfa za fremu... wanalaza mirija na kufanya kilimo has cha mboga...inapendeza...
 
ila mkuu. Chasha kwenye lile bandiko lako ulisema unaenda kenya kujifunza.
kwasababu mbegu za hayo majani hata wewe hujui
 
Last edited by a moderator:
Japo mkuu ungewaka wazi mtu kama mimi ndiyo leo nasikia nawezaje kufanya hiyo na hatua gani nifuate na material zinapatikanaje?

Mkuu unaweza tumia simple materio ila ni lazima ziwe ambazo haziruhusu kutu au fangasi, kuna mbolea yake inayo itwa hydroponic nutrients, hii ina zile nutrients ambazo zinapatikana kwenye udongo.
 
nimikuwa nikifatilia hiki kilimo... sasa hivi singapore wanahamia katiki 'wertical farming'.... plot ndogo ...wanainua ghorfa za fremu... wanalaza mirija na kufanya kilimo has cha mboga...inapendeza...

Mkuu hii ni kilimo kizuri sana hasa sehemu zenye shida ya maji, ukivuna maji yako ya mvua yanakutosha musimu mzima,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…