Hydroponics Techinology inavyoweza kubadili maisha ya wabongo na kupunguza tatizo la Ajira

Hydroponics Techinology inavyoweza kubadili maisha ya wabongo na kupunguza tatizo la Ajira

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Kuna hili swala la Hydroponics Techinology ambapo ni uoteshaji wa mazao bila kutumia udongo na kinacho takiwa ni maji tu na sehemu ya udongo huwekwa virutubisho fulani.

Hii techonolojia inaweza kuwa ni ngeni kwetu ila kwa wenzetu si ngeni make ilikuwepo miaka ya 1929 na William Frederick Gericke wa University of California

Hii techinolojia inaweza tumika kuzalisha

1. Chakula cha kulishia mifugo na hata binadamu
Kwenye eneo la eneo la futi 20 kwa 10 mkulima anaweza zalisha nyasi zaidi ya kilogram 50 kilograms

Hii Techinolojia ni nzuri sana kwa watu wenye eneo dogo hasa wa Mijini kwa sababu eneo la 140 meta lina weza tosha kuweka tray zaidi ya 1800 ambazo zinaweza toa tani 1.2 za majani ya mifugo kwa kutumia maji lita 700-900

FAIDA ZA HII TECHINOLOJIA

  • Hakuna udongo unaoa hitajika
  • Maji yanayo tumika hapa ynaweza tena tumika kwa ishu zingine
  • Ni rahisi kuzibit viine lishe
  • Iko stable na inatoa virutubisho vingi sana
  • Rahisi kuvuna
  • Mimea inakuwa vizuri sana
  • Ni nzuri kwa biashara

vifaa hivyo na hiyo nyumba vilivowekwa ni bei juu kuliko ardhi yetu, ambayo huuzwa elfu 10 kwa heka. hiyo ni ya ulaya.
 
vifaa hivyo na hiyo nyumba vilivowekwa ni bei juu kuliko ardhi yetu, ambayo huuzwa elfu 10 kwa heka. hiyo ni ya ulaya.

hata mabeseni ya maji yanafaa kutumika si lazima hivi vifaa vya kutoka nje,
 
Elimu nzuri sana uliyotupa,ubarikiwe.naiweka kwenye data bank yangu kwa ajili ya baadaye.
 
nataka nirudi dar nikafuge na nachohofia ni majani ya mifugo.
mkuu nirushie namba yako nipate maelezo kwa kina
 
nataka nirudi dar nikafuge na nachohofia ni majani ya mifugo.
mkuu nirushie namba yako nipate maelezo kwa kina

Mkuu na mimi nilipata hii elimu juujuu ila nina mpango wa kwenda Kenya kupata mafunzo zaidi, kwa kweli ni techinolojia nzuri sana kwa sababu ukiwa na eneo dogo kabisa unaweza fuga ng'ombe wako na usiwe na shida ya majani.
 
ni jambo zuri sana mana unatakiwa kwenda na wakat pamoja na teknolojia
 
Mkuu na mimi nilipata hii elimu juujuu ila nina mpango wa kwenda Kenya kupata mafunzo zaidi, kwa kweli ni techinolojia nzuri sana kwa sababu ukiwa na eneo dogo kabisa unaweza fuga ng'ombe wako na usiwe na shida ya majani.

Kama uko fb ingia page moja inaitwa MKULIMA YOUNG, huko huwa tunabadilishana mawazo ya shamba, karibu mkuu.
 
vifaa hivyo na hiyo nyumba vilivowekwa ni bei juu kuliko ardhi yetu, ambayo huuzwa elfu 10 kwa heka. hiyo ni ya ulaya.

Hii ni maalum kwa wale wanaolima karibu na mjini (soko), na hivyo vifaa unaweza kutengeneza hata wewe kwa kuokota makopo ya bure kabisa.
 
Back
Top Bottom