I and the FATHER are one!

I and the FATHER are one!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam. Shalom!

Ujio wa mtu huyu duniani aliyetokea Mbinguni Kisha kuuvaa mwili wa mwanadamu, akaingia ndani ya tumbo la mwanamke Mariam bikra Kisha akazaliwa, umeendelea kuwa utata na sintofahamu Kwa wengi.

Wayahudi waliokota mawe na kutaka kumrushia baada ya Kutoa kauli hii tata kwamba:

(Yohana 10:30).
Mimi na BABA ni umoja. Hii ni maana kuwa Mungu ni MMOJA tu, NAFSI Moja.

Wapo wanaodai kuwa mwanzo wa mtu huyu ni pale alipozaliwa na Mariam,

Hii pia Si Kweli, maana Yesu mwenyewe anasema kuwa,

(Yohana 8:58)

Yesu anawaambia, Amin, Amin nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako Bado, MIMI NIKO"

Jina Hilo Mimi NIKO alilotumia kujitambulisha Yesu, ndilo Mungu alilitumia kujitambulisha Kwa Musa katika kijiti kiwakacho moto na hakiteketei. "NIKO AMBAYE NIKO". (Kutoka 3:14)

Huyu Ibrahimu YESU anayemuongelea alikuwapo kabla Yesu kuvaa mwili wa mwanadamu na Kuzaliwa, ndiye baba wa waarabu chini ya Ishmael na wayahudi chini ya Isaka na ndiye baba wa wakristo wote Kwa kumwamini Yesu. Sasa YESU ajitambulisha kuwa Yeye alikuwapo kabla Ibrahim hajakuwepo, Yesu Hana baba wala mama, ndiye huyo huyo Baba, mwana na Neno, Roho mtakatifu.

Kwa maandiko hayo, itoshe kuwafumbua macho na kuwatoa tongotongo kuwa, Yesu ndiye huyo huyo Mungu Mmoja.

Ndiye Mungu BABA.

Ndiye Mungu mwana.

Ndiye Mungu Roho mtakatifu.

Ikiwa hujamwamini Yesu fuatisha Sala hii:

BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN
 
Kama Yeau ndio huyu huyu, alipotundikwa msalabani alilia kuwa “ Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha

huyu alomuacha ni nani?
 
Kama Yeau ndio huyu huyu, alipotundikwa msalabani alilia kuwa “ Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha

huyu alomuacha ni nani?
(Yohana 10:17-18)

Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, Bali Mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uwezo wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena.

...... mwisho wa kunukuu....

Ndipo ujue hata Malaika mtoa Roho hakuweza kupita na Roho ya Yesu, maana Yesu ndiye huyo huyo Mungu Mmoja.

Aliutoa uhai katika mwili wa mwanadamu Kisha kuurejesha tena.

Kulia, kuhuzunuka ni mwili wa nyama na hisia za kimwili maana alivaa mwili na kuwa kama mwanadamu Ili kuuokoa Ulimwengu, lakini KATIKA Roho, alikuwa huyo huyo Mungu Mmoja.

Amen
 
(Yeremia 22:5)
Naapa Kwa NAFSI Yangu, Asema BWANA Mungu.

Mungu ni MMOJA tu, NAFSI Moja.

Islam na Dini zote mlijue hili.
 
Baba wa
Huyu Ibrahimu YESU anayemuongelea alikuwapo kabla Yesu kuvaa mwili wa mwanadamu na Kuzaliwa, ndiye baba wa waarabu chini ya Ishmael na wayahudi chini ya Isaka na ndiye baba wa wakristo wote Kwa kumwamini Yesu. Sasa YESU ajitambulisha kuwa Yeye alikuwapo kabla Ibrahim hajakuwepo,
waafrika ni nani???
Mungu wenu ni nani???
😳😳😳😳
 
Baba wa

waafrika ni nani???
Mungu wenu ni nani???
😳😳😳😳
NENO ndiye Yesu, ndiye NIKO AMBAYE NIKO,

Ndiye muumba wa Mbingu na Nchi.

Waafrika waliumbwa na huyo, ndiye Mungu wa Afrika na Dunia na Ulimwengu wote.

NB: Asiyeamwamini Yesu Kristo amekwisha hukumiwa,ni mfu anayetembea/ msukule,
 
Back
Top Bottom