Mkuu ninaomba usipatwe na mawazo sana. Wanasema maisha in safari ndefu hivyo hivi ni mojawapo ya vikwazo tu tunavyokutana navyo njiani ila vina mwisho wake.
Kikubwa ni kumtanguliza Mungu akuongoze usiingiwe na imani ya kukufuru na kukata tamaa huyo ni shetani anacheza na wewe kutaka kukuondoa kwenye safari yako.
Usijali japo ni vigumu kidogo ila piga moyo konde ndugu ni la muda tu unaweza ukaamka kesho ukajiuliza hv jana nililala na hali ile kumbe. Mungu akutangulie...