I got to say it; watawala wana matatizo kichwani!?


Mkuu hayo matumizi nami nimeyafurahia yanaweza yakawa solution kwa matatizo fulani fulani ya Ndoa.
Hili sakata la muro natamani niuushuhudie mwisho wake kwa kauli thabiti kutika kwa viongozi wetu....lakini nahofia mambo yatakuwa kama stori zingine za EPA,Meremeta n.k
 
Nilitegemea wangesema labda risiti sio halali wangeanzia hapo..
Walipoanzisha Duka lao walitegemea wateja wawe nani Polisi na Magereza pekee?
 

MM,
umenichekesha sana Kaka,ila me kwa upande mwingine namuunga mkono huyo mjeda ingawa of cpurse point zako zina mashiko, ni vigumu kwa Raia kujilinda kwa kutumia pingu,haiwezekani kabisa wewe MM ,majambazi wamekuvamia afu ukawatisha na pingu..MM umenisoma!!!!
Ila bunduki,Raia wa kawaida anaweza akaitumia kujilinda nayo,au sio MM..
ila nijuavyo mimi,hakuna kifungu cha sheria kinachosema ni marufuku raia kumiliki pingu, hivyo si kosa kuwa nayo coz sheria iko silence on that..wanasheria watanisaidia katika hili..
Mwisho kabisa et nimesikia fununu kuwa MM Muungwana anataka ugombee ubunge mwaka huu,kakuahid Uminista....Natania MM
 
Taanzania Tanzaniaaa nilukupenda nchi yangu!!!
KUNA MWENZAKO alikosea,penye "Tanzania" akaweka jina la shemeji, na penye "nchi" akaweka mpenzi...weeeeee
hebu jaribu na wewe dada..
Natania Dadaaangu.
Av a gud day
 

we! sikukuambia ufungue macho ukanunue pingu! ila uangalie kuwa swala la Muro la kununua pingu inaonekana ni common kwa baadhi ya raia kwenye lile duka!

ukinunua mimi simo! usiisahau tu kwenye gari! LOL!
 

Naheshimu sana michango yako ambayo imejaa nguvu za hoja... lakini angalia safari hii isije ikawa wewe ndiye mwenye stahili ya kupimwa akili...
Kwanini?
1. Mwenye duka hakusema raia kumiliki pingu ni uvunjivu wa sheria bali amesema raia wa kawaida hawaruhusiwi kununua pingu.
2. Bunduki/risasi za moto vs pingu ni vitu viwili tofauti... na vinatumika kwa kazi mbili tofauti.
AND... Raia wa kawaida hawauziwi pingu kama wasivyouziwa mavazi ya jeshi/polisi..... kwa sababu wanaweza ku-mis-use kazi zake i.. e. wakatumia kwa utapeli kama alivyofanya Muro
 


Hakuna kitu kama "raia wa kawaida".

AND... Raia wa kawaida hawauziwi pingu kama wasivyouziwa mavazi ya jeshi/polisi..... kwa sababu wanaweza ku-mis-use kazi zake i.. e. wakatumia kwa utapeli kama alivyofanya Muro

Muro ameitumia vipi pingu kitapeli? alimfunga nayo nani na wapi?
 
Hakuna kitu kama "raia wa kawaida".



Muro ameitumia vipi pingu kitapeli? alimfunga nayo nani na wapi?


OPSS... ni kweli hakuna kitu kama raia wa kawaida (theoretically) lakini hoja yangu inabaki palepale.... raia...

Hii ya Muro ameitumia vipi... tusubiri tafadhali... kesi iii mahakamani... utajua tu aliitumia vipi...
 

Dinho halafu inaonekana ni very romantic! Mimi baada ya MMKJ kuweka ule ushairi kule basi nikasema wacha tutafute lakini tatizo Mzinga watakuwa wanajishtukia kuuza kwa sasa
 
Hii ya Muro ameitumia vipi... tusubiri tafadhali... kesi iii mahakamani... utajua tu aliitumia vipi...

kwanini tusubiri tena mahakamani wakati tayari umeshahitimisha kuwa aliitumia kitapeli? Umesema hivi:


... sababu wanaweza ku-mis-use kazi zake i.. e. wakatumia kwa utapeli kama alivyofanya Muro

inaonekana hukutaka kusubiri mahakamani kwani tayari umeshajua kuwa Muro ametumia pingu kitapeli? umejuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…