And Arabic is the language of Islamic doctrines.
And am not a muslim, neither i will be.
i will chose death between death, living and being islamised.
what do you think ma pipo?
Umenikumbusha kitu kimoja -- iliishia wapi ile kampeni ya kutaka kubadilisha jina la Jiji la Dar na badala yake uitwe Mzizima?
Wengi wa nani? Namna gani?I hate it not because its arabic but because it makes most of us be myopic and narrow minded above all local!
Nunga mkono kabisa unachosema juu ya ubaguzi.Dar es salaam - sikia vile jina la mji lilivyo tamu kutamka na lenye maana bora. Dar es salaam. Dar = mji au bandari , Salaam = Salama. nini zaidi unataka ?.
And Arabic is the language of Islamic doctrines.
And am not a muslim, neither i will be.
i will chose death between death, living and being islamised.
what do you think ma pipo?
Kiswahili ni kiislamu. Ukienda nchi kama Rwanda, Burundi, Uganda, Sudan ya kusini, Malawi ya kaskazini; kiswahili ni lugha inayozungumzwa na waislamu. Na hata hapa nyumbani kilipozaliwa kiswahili, waislamu ndiyo watu wa kwanza kuzungumza kiswahili. Mombasa, Tanga, Unguja na Pemba, Dar-es-salaam, Kilwa, Lindi mpaka Mtwara.; Kigoma na kuvuka mipaka kuingia nchi jirani. Kikaendelea kukomaa na kuusambaza Uislamu na na mpaka leo hii kinazungumzwa na watu wasiojua kilipotokea.
Na hiyo ndiyo historia yetu.
AWAU'ZA WASWAHILI
1
Risala enuka hima, sikae 'kataghafali
N'na jambo 'takutuma, ubalegheshe suali
Nipate jawabu njema, yenye amani na kweli
Nauliza Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
2
Lugha nyingi duniyani, zatamkwa mbalimbali
Na zote ulimwenguni, zina wenyewe mahali
Si Hindi Si Uzunguni, mewaumbia Jalali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?
3
Wakamba wana kikwao, lugha yao ya asili
Na Wazungu piya nao, wana zao mbalimbali
Na Wameru wana yao, wengine ni Wasomali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?
4
Wahindi wana Kihindi, kwa kabila mbalimbali
Na Wanandi ni Kinandi, ndizo zao akuwali
Wengine ni Wakilindi, wana yao ya asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
5
Kuuliza Si ujinga, musinifanye jahili
Nautafuta niuwanga, tuzinduwane akili
Ndipo shairi hatunga, kubaleghesha suali
Nielezwe Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
6
Mara nyingi husikiya, kuwa hichi Kiswahili
Hakina mtu mmoya, ambaye ni chake kweli
Na wengine huteteya, kina wenyewe asili
Ndipo ha'mba Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
7
Masai ana kikwao, lugha ya tangu azali
Na Mahara wana yao, wengine Mashelisheli
Na Waluo lugha zao, Si sawa na Maragoli
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
8
Na jamii wengineo, wana lugha mbalimbali
Na kujuwa ya wenzao, ni kujifunza ya pili
Lakini wana na zao, lugha za tangu asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
9
Sasa ambalo nataka, kwa wenye kujuwa hili
Wa Kenya na Tanganyika, na walo kulla mahali
Nipani ilo hakika, tubalegheshe ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
10
Miye mefikiri mno, kuamuwa jambo hili
Na huona lugha hino, lazima ina asili
Kwa sababu kulla neno, lina mwanzo wa usuli
Ndipo ha'mba Kiswahili, hi lugha ya watu gani?
11
Na iwapo hivi sivyo, niliyyoamuwa hili
Nionyeshani viliyyo, mubainishe ukweli
Nijuwe ambavyo ndivyo, tutowane mushkili
Kifunuke Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
12
Na iwapo atakuja, wa kunijibu suali
Namuomba jambo moja, twambiyane kiakili
Tusionyane miuja, jambo nisilo kubali
N'anambiye Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
13
Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
Ahmadi wa Nasiri, na Bhalo ndilo Ia pili
Mtungaji mashuhuri, mpenda penye ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
By Ahmad Nassir from Malenga wa Mvita
Hapa Mkuu kidogo kuna kasoro, sio lazima ulichoandika ni sahihi, wakati mwengine tunatumia lugha kimkato-mkato kurahisisha mambo ili ueleweke haraka. Ni sawa kusema Kihindi ni lugha lakini kumbuka India kama nchi kuna lugha kibao ambazo sio kihindi, mara nyingi ikitokea lugha kuzungumzwa sehemu/nchi moja pekee basi tunaweza kutumia jina la nchi kama ulivyoandika hapo juu; mfano wako kifaransa/Ufaransa/mfaransa, jee wajua kua kifaransa hakizungumzwi Ufaransa pekee? Ubelgiji na na nchi za jirani zinazungumza hiyo lugha pia. Mfano mwengine utasikia aah huyu anazumgumza ki-Tanga, ukweli hakuna lugha ki-tanga lakini huwa unamaanisha ana lafdhi (accent) ya watu wanaotokea eneo la Tanga. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na watu wa Afrika ya mashariki; kilugha si kosa kuwaita wazungumzaji kiswahili-Waswahili, lakini kwa vile tulivyoisanifu lugha hii ukmwita mwenzio mswahili humaanishi tena kua huyo ana kimanya kiswahili. Kadhalika nauliza nchi gani "Uarabuni"? najua wazi ni wapi wanazungumza kiarabu. Namalizia kwa kukumbusha Australia, Canada na USA wanazungumza kiingereza na si Waingereza?Kichina = Uchina = Mchina
Kihindi = Uhindini = Mhindi
Kitaliana = Italia = Mtaliana
Kifaransa = Ufaransa = Mfaransa
Kiswahili = Wapi? = Mswahili?
And Arabic is the language of Islamic doctrines.
And am not a muslim, neither i will be.
i will chose death between death, living and being islamised.
what do you think ma pipo?
And Arabic is the language of Islamic doctrines.
And am not a muslim, neither i will be.
i will chose death between death, living and being islamised.
what do you think ma pipo?
Jerusalem, Umeumwa na mbu sugu na sasa una malaria sugu