Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Askari Polisi wa Kike kutoka Tanzania Waelekea Dafur Kulinda Amani
Kamanda Munisi akikabidhi bendera ya Taifa askari hao kwa Mkuu wa msafara huo Mrakibu wa Polisi Hawa Luzy.
--------------
Na Mohammed Mhina na Charles Tupa wa Jeshi la Polisi.
Kundi la kwanza la Polisi wanawake linaondoka nchini kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya kuongeza nguvu katika maswala ya kulinda amani katika eneo la Darfur nchini humo.
Akizungumza wakati akiwakabidhi bendera ya Taifa askari hao kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema,Mkuu wa Utawala Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Zuhura Munisi,amewaasa askari hao kwenda kuzingatia maadili ya kiutendaji ili kuleta heshima ya taifa letu mbele ya sura ya Umoja wa Mataifa.
Kamanda Munisi amesema kuteuliwa kwa askari wanawake kwenda kulinda amani nchini sudani kunatokana na ukweli kwamba wengi wa wahanga walioko katika maeneo yanayokumbwa na migogoro nchini sudani ni wanawake na watoto.

Kamanda Munisi amewakabidhi bendera ya Taifa askari hao kwa Mkuu wa msafara huo Mrakibu wa Polisi Hawa Luzy.
Naye Mkuu wa Mahusiano ya Kimataifa wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Geofrey Kamwela amesema kuwa kundi hilo linakwenda kuungana na askari kutoka nchi mbalimbali duniani zinazolinda amani nchini sudani.
Kamanda Kamwela amewataka Askari hao kwenda kudumisha nidhamu na kuzingatia maadili na tamaduni za raia wa Sudan ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Wengine waliohudhuria katika hafla ya kuwaaga askari hao ni Makamanda ACP Adolfina Chialo na Afisa Mnadhimu wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi SSP Hassan Mbezi.

My Take
Sasa..kipaumbele ni kipi.. kupokea mipira, baskeli na viatu au kuwaaga mabinti na dada zetu wanaoenda mbali wakiitikia wito wa taifa lao? Yaani hata Waziri hayupo wa kuwapa bendera..? I'm sorry.. I couldn't resist..
Nevertheless, I'm so proud of these daughters of our nation serving in the tradion of many so other women who have served our nation with distinction. You go girls!! Salute!