Nashauri kuwa jukwaa hili tungelilitumia kwa lengo la kuwaelimisha na wengine pia. Nimeshangazwa kwamba 'I Miss You' inawashinda wanajamvi kuipatia tafsiri na badala yake wanaishia kupotosha ulimwengu! Kama hujui jambo si dhambi, jiweke kando wanagenzi watakujuza na wewe utaelimika, au siyo? I MISS YOU kwa tafsiri sisisi ya Kiswahili tunaambiana, "TUMEPOTEZANA"! na unaweza kuongeza vikorombwezo vingine kama "Tumepotezana sana" kumaanisha "I MISS YOU VERY MUCH" au "Tumepotezana, Mpendwa" kumaanisha "I MISS YOU, DEAR"!! n.k n.k n.k...........