KWA FAIDA YA WENGI, MAANA SWALA LA HIVI LIMEKUA TATIZO KUBWA NA WATU WENGI UJIULIZA MASWALI SANAA KUHUSU HILI;
wakuu ni hivi, mtu anaposhinda kesi ya madai kitaalam huitwa DECREE HOLDER, na yule alieshindwa kesi huitwa JUDGEMENT DEBTOR hivyo basi DECREE HOLDER ata takiwa kufungua shauri jingine ktk mahakama ile ile iliyotoa hukumu ili iweze kukaza hukumu hio ambapo kitaalam huitwa Applicatin for Execution of Decree.
Sasa kwa mujibu wa sheria, hatua ya kukaza hukumu inatakiwa ifanyike muda wowote ule lakini usizidi miaka 12 ambapo mtu ukishafungua shauri ilo la kukaza hukumu Mahakama itamuita JUDGMENT DEBTOR (au mdaiwa au aliamuliwa na mahakama kulipa) ili ajieleze ni kwanini hajafanya vile alivyoagizwa na mahakama baada ya kesi kuisha, ni kwa nini amri za kwenye hukumu aliyopatiwa kesi ilivyoisha hajafanya vile? Na hizi favor/amri/mlolongo wa ulipwaji zinakua zimeainishwa kwenye Decree (au statement ya kikaza hukumu).
Sasa baada ya Mahakama kulizika kwamba hakuna Rufaa iliyokatwa kupinga hukumu iliyotolewa au muda wa rufaa ulipita na Judgement Debtor hakukata rufaa basi mahakama itaamuru hukumu itekelezwe mara moja (huku ndio kukaza hukumu). hapa sasa mdaiwa uyo Judgement Debtor atazimishwa kulipa deni analodaiwa... Na hatua hii hawezi kuzingua tena, kwani Mahakama ita waorder madalali wake wataifishe mali za uyo mdaiwa ili kumfilisi.
Kila la kheri.