ninampa pole kwasababu anaweza kukaa ndani kwa kitambo kirefu akisubiria upelelezi, hadi jalada lipelelezwe na kufikishwa kwa RCO aliandikie liende kwa state attorney atakayeamua kama kesi iendelee kwa murder, au manslaughter au apigwe nolle prosequi (aachiwe kabisa), inaweza kuchukua muda. mtafute kibatara wa pale dsm aliyemsimamia Lulu. kuna defence of alibi hapo, pamoja na kwamba hatujui ilikuwaje story yenyewe hadi kifo kutokea.
wakati mwingine mtu anaweza kupanga mauaji wakafanya wengine yeye akiwa ameondoka makusudi eneo la tukio ili aje aseme hakuwepo kwenye eneo la tukio wakati wa mauaji mf.alikuwa musoma siku ile marehemu alipouawa mtwara etc. hii inaitwa defence of alibi, na ili iwe successiful, ni lazima mshitakiwa/mtuhumiwa ai raise mapema kabisa kabla ya prosecution hawajafunga ushahidi, ili prosecution wapate nafasi ya kwenda kufanya inquiry whether kweli huyo mtu hakuwepo eneo la tukio. hapo mtuhumiwa lazima alete vielelezo vya ticket, alikuwa na nani kule, alilala wapi na maenezo mengine mengi ambayo kusema kweli kama mtu atakuwa ametunga tu, anaweza kuja kujigonga kwenye cross examination. siwezi kusema lolote kuhusiana na kesi hii mpaka niwe nimesoma maelezo ya mashahidi na jalada kwa ujumla, ila kama ni kweli hakuwepo eneo la tukio na hakushiriki kwa namna yeyote ile kupanga mauaji etc, ninaamini atafanikiwa tu Mungu yupo. poleni.