Ibara hizi za Rasimu zinahitaji maboresho, maboresho yafuatayo.

Ibara hizi za Rasimu zinahitaji maboresho, maboresho yafuatayo.

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,112
Reaction score
4,540
Kadiri ya nilivyosoma mpaka Sura ya Nane, nimeona kuna Ibara kadhaa zinapaswa kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha utekelezaji bora wa Katiba, na mustakabali bora kwa Watanzania.

20.Utekelezaji wa masharti ya maadili.
(2)Masharti yaliyoainishwa katika Sehemu hii ya Sura ya Tatu yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki..
Ili kurahisisha utekelezaji ulio bora na ambao ni muhimu sana, inapaswa kuelezwa bayana "kufanyiwa marekebisho stahiki", je marekebisho hayo stahiki yatafanywa na nani? Inapaswa kuelezwa bayana kama marekebisho hayo stahiki yatafanywa na Bunge, Mahakama , au Serikali.

51. Ulinzi wa mali ya umma .
52. - (1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
Kwa kuataja "kila raia", ibara hii ndogo haiwabani wageni waliopo nchini, ambao si raia kwa mujibu wa Katiba, kutekeleza masharti yake. Hivyo, inapaswa kuandikwa 52. - (1) Kila mtu anao wajibu wa kulinda .......
52. Haki na wajibu muhimu.
52. -(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki za msingi za binabamu, na matokeo ya kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilivyofafanuliwa katika Katiba hii.
(2) Kila raia wa katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.

Ibara zote ndogo mbili zinawatenga wageni walio ndani ya Jamhuri ya Muungano, ambao siyo raia kadiri ya Katiba, kupata haki sawa au hifadhi chini ya sheria.
Hivyo, ibara zote ndogo mbili zinapaswa kuanza hivi: 52. (1)
Kila mtu katika Jamhuri..... 52. (2) Kila mtu katika Jamhuri ...... Hiyo itaondoa utata katika utekelezaji na baina ya ibara nyingine ndogo (3, 4, na 5) za ibata hii ya 52.

81. Malalamiko kuhusu uhalali wa Uchaguzi wa Rais
4. Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (3). Mahakama ya Juu inaweza kutoa uamuzi bila kutoa sababu za uamuzi na sababu hizo zikatolewa ndani ya kipindi kisichozidi siku thelethini tangu siku ya kutoa uamuzi.

Ibara hii ndogo inapaswa kuilazimisha Mahakama ya Juu kutoa uamuzi na sababu za uamuzi huo kwa pamoja. Kuruhusu Mahakama ya Juu itoe uamuzi bila ya sababu kunaweza kuzidisha jazba/hasira kwa wafuasi pinzani dhidi ya mgombea aliyetangazwa.
Mahakama inapaswa kutoa uamuzi na sababu za uamuzi wake ndani ya sikuu kadhaa ili mgombea aliyelalamika aweze kuwatuliza wafuasi wake, kadiri ya sababu zilizotolewa.

82. Kiapo cha Rais na muda wa kushika madaraka.
82.-(1) Rais Mteule ataapishwa na Jaji Mkuu na atashika nafasi ya madaraka ya Rais iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote, hatashika madaraka kabla ya kupita siku thelathini kutoka siku matokeo ya Uchaguzi wa Rais yalipotangazwa na Tume Huri ya Uchaguzi au siku ya kuthibitishwa na Mahakama ya Juu.

Utekezaji wa ibara hii utaleta utata mkubwa sana. Haitafaa kwa Rais kutangazwa, na hapo hapo kuapishwa, na asishike madaraka. Inapaswa Rais akitangazwa ya kwamba amechaguliwa, Mahakama ya Juu ipewe siku kadhaa ili kama kuna malalamiko juu ya Uchaguzi, kisha kushughulikia malalamiko kama yatawasilishwa, ndipo Rais Mteule aapishwe na kushika madaraka.
Tuepushe yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya, 2006. Tuige Katiba ya Zimbabwe ilivyotekelezwa kufikia kuapishwa na kushika madaraka kwa Rais Mugabe, 2013.

87. Kinga ya mashtaka dhidi ya Rais.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana kutokana na kuondolewa madarakani na Bunge, haitakuwa halali kwa mtu kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la madai dhidi ya mtu aliyekuwa Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo alilofanya wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
Hakuna mtu aliye juu sheria! Rais hawezi kuruhusiwa kirahisi rahisi kuwa juu ya sheria. Bunge, kama ilvyo katika ibara ya 88, liwezeshwe kuondoa kinga ya kutoshtakiwa baada ya kukoma kuwa Rasi ili apaje kujibu mahakamani makosa ya jinai au madai aliyoyafanya akiwa madarakani, hususani ukikwaji wa Katiba.
Jamhuri ya Muungano inapaswa kuwa kama Zambia, Misri, Ufaransa, ...

Hayo ni maoni na mawazo yangu. Unaweza kongeza uchambuzi wako wa Rasimu ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba, ili kupata Katiba bora.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom