Ibara ya 15:1 na 2


Inakuwaje nchi iliyojaliwa mali asili nyingi na ardhi yenye rutuba na watu wake wanakufa kwa kukosa chakula? Yaani kama hata kujilisha hatuwezi..nini kingine tutakachoweza?
 
Unajua mzee Nyerere alifaa sana kipindi chake hichohicho na alifanya vyema sana kuamua kung'atuka pale alipofikia. Kwa hakika Nyerere angeng'ang'ania madaraka (na kama Mungu angemuweka hai) hadi leo, naamini yangemkuta yaleyale yanayomkuta Mugabe na CCM ingekuwa as unpopular as ZANU-PF. Na hili ni jambo ambalo CCM inabidi wamshukuru Nyerere, hasa kwa kitendo chake cha kushinikiza mabadiliko ya katiba ili kipindi cha urais kiwe na kikomo cha mihula miwili. Hili la ukomo wa urais lime-work for the advantage ya CCM maana imekuwa ikijibadili rangi kama kinyonga kwa kubadili mgombea urais na watu wanaamini wamepata kitu kipya kumbe ni kilekile. Tazama watu walivyopagawa na ujio wa Kikwete hadi kuamini kwamba eti CCM imezaliwa upya na imemjua bwana. Ambacho najiuliza mpaka kesho ni inakuwaje watu wengi namna ile wanaendelea kuingizwa mkenge huu na CCM hadi maprofesa wa political science? Angalia watu walivyopagawa na mkutana wa CCM huko Butiama utafikiri wamelishwa limbwata na CCM!
 

mzee, ukiangalia na wewe uko kundi hilo hilo. Wale ambao walikuwa wanatarajia kitu toka Butiama na wale ambao walikuwa wanapuuzia kilichotokea Butiama wote walikuwa wanazungumzia Butiama na hivyo wote walikuwa kwa namna tofauti wame"pagawa na mkutano wa CCM huko Butiama utafikiri wamelishwa Libwata na CCM". Unaponyosha kidole kuwaelekeza wengine angalia vingine havikueleki wewe.
 
Mimi nilijuwa itakuwa the same 'ol pompous claptrap! Sikutegemea jipya na sitegemei jipya hadi waondoke (CCM) madarakani...
 
i have to give this one to mwanakijiji, jinsi anavyosimamia hoja, av alwayz appreciate mawazo ya Nyerere, yaani ilikuwa ni elimu tosha kumsikiliza ingawa sikuzaliwa enzi za uongozi wake lakini naheshimu jinsi alivyoweza kuongea katika namna ya kuburudisha na kusisimua, alikuwa na authority katika maneno yake, natamani ningekuwa bingwa wa kutoa hoja kama waheshimiwa humu ndani kuhusu hiyo ibara lakini ni wazi ninaelimika sana kama mtu wa kizazi cha sasa, thank you guys.
 

Hakuna anayeweza kubishana na Mwanakijiji kuhusu Nyerere...anayethubutu hutolewa nishai. Mwanakijiji anajua kila neno lililowahi kutamkwa na Nyerere ukuachilia mbali yaliyoandikwa! Ukitaka kubishana naye kuhusu Nyerere...do it at own peril...he will own you. If you don't believe me ask Field Marshall ES...kwikwikwiiiii....

On the other hand....ukitaka kupanguliwa kwa hoja na maneno makali na Field Marshall ES basi mseme vibaya mzee Malecela. Huyu bwana (FMES) anamjua Malecela kama mtu ajuavyo kiganja chake. Hakuna anayemweza ikija kwa Malecela. Hata Mwanakijiji haingizi mguu!! Anayetaka kutolewa nishai na FMES ajaribu kumsema vibaya Mzee Malecela....atakiona mwenyewe....kwikwikwiiiii
 
Mzee kwanza, naomba ujifunze kukubali kukosea na kusahihisha. Umesema huko nyuma "Hajawahi kusema alikosea wapi" nimekuonesha lakini umeshindwa kukiri kuwa ulikosea; ukasema kuwa Nyerere na Jumbe hawakushiriki katika suala la Katiba ya CCM nimekuonesha na ushahidi lakini umeshindwa kukubali kuwa uliongeza chumvi.

Uungwana ni pamoja na kukubali kukosea au kutosema sawasawa. Kuendelea kurukia hoja nyingine kana kwamba yaliyopita si ya maana hatutafika mbali.


Alituletea uhuru on time, na pia alituletea umoja, akaondoa udini na ukabila.

alifanya hivyo kwa misingi gani na ni kitu gani kilimuongoza kushughulikia mambo hayo?



1. Maazimio ya Arusha, yaani viongozi lazima wawe masikini kwa maana kwamba viongozi wote wa upinzani sasa na CCM wote wangetakiwa kuwa un-qualified under mawazo ya Mwalimu, maana sio unaona karibu wote wako sawa kipesa.

Sasa nikikuuliza ni lini Mwalimu alikuwa na fikra kuwa viongozi wawe masikini? Ni wapi na lini Mwalimu aliwahi kusema kuwa viongozi wawe masikini? Hizo siyo fikra za Mwalimu.

2. Mambo ya chama kushika hatamu yamepitwa sana.

Chama chochote kinachoshika madaraka huwa kimeshika hatamu; huwezi kuondokana na hilo. Chama cha Demokrat kimeshika hatamu za Bunge la Marekani wakati chama cha Republican kimeshika hatamu za Urais. Siku chama kimoja kinaposhikilia vyote viwili basi tunasema kimeshika hatamu za uongozi wa Taifa.

Sasa hivi CCM imeshika hatamu za uongozi wa Tanzania. Hili haliepukiki, unless huelewei maana ya kushika hatamu.


3. Wananchi kuogopeshwa kuzumgumza ukweli wa siasa ya taifa lao, yalipitwa hayo.

Yaani hizo zilikuwa ni fikra za Mwalimu? Mwalimu alimkataza nani kuzungumzia siasa za Taifa lao. Tatizo ambalo naamini Mwalimu alikuwa nalo ni kuwa watu waliokuwa wanazungumzia hoja za Taifa walikuwa very shallow na akizipangua hoja zao wanaona anawazima. Huwezi kwenda kumshauri Mwalimu tununue Richmond, Rada, sijui vitu gani ukategemea akasema "ndiyo" kirahisi rahisi kama tunavyowaona hawa ndugu zetu wa leo.

Waulize waliokuwa wanaenda na mapendekezo yao kwa Nyerere alivyokuwa akiwagrill, you had to be very sharp. Kama huamini rejea mjadala kati ya Nyerere na Prof. Ali Mazrui.

4. Wananchi wote kwenye taifa kuwa sawa, au siasa za ujamaa leo ni a big joke hilo limewashinda hata wa-Rusi waanzilishi wa ujamaa wake, haya yamepitwa kabisaaa na time.

Mzee ujamaa bado upo unaishi na unafanya kazi hata Marekani na nchi nyingine. Ujamaa ni itikadi ambayo huwezi kuboreshwa n.k China ni nchi ya kijamaa (kwa mazingira yao), Vietnam ni nchi ya kijamaa, hata huku magharibi nchi kama za Scandinavia baadhi zina mlengo wa kisoshalist zaidi. Hivi majuzi Jose Zapatero toka chama cha Ujamaa cha Wafanyakazi ameshinda tena huko Spain.

Ujamaa haujafa ndugu yangu, bado upo na una nguvu. Leo hii hata Wamarekani wenyewe wanaanza kufuata mambo yenye chembe za kijamaa ingawa hawatoweza kamwe kuuita ujamaa.!

5. Siasa kwenye uchumi, yaani mwenyekiti wa tawi la CCM kiwandani anamtisha meneja, hayo yamepitwa sana.

Hizo siyo fikra za Nyerere, na kama mwenyekiti wa CCM anamtishia Meneja huyo Meneja inabidi atimuliwe!

6. Elimu bure na afya bure, ndio hayo taifa letu linalipia mpaka leo.

Mzee, leo hapa nilipo kuna Kalamazoo Promise ambapo wanafunzi wa HIgh School wa Kalamazoo wameahidiwa kwenda Chuo Kikuu bure! Hivi unajua ni kiasi gani nchi za magharibi zinachangia katika elimu za watu wao? Hivi unajua ni wangapi hapa wanasoma Harvard Bure? Unajua ni wanafunzi wangapi wa shahada za juu ambao wanafanya research bure kabisa? Mwalimu alilijua hilo ndio maana alihakikisha kuwa elimu inapatikana kwa kila anayetaka.

Leo sisi tumewarudisha watoto toka Ukraine ambako walikuwa wanasomea Udaktari, Uhandisi n.k Ili waje kuuza nyanya Dar, halafu tuna ujasiri wa kusema "tuna upungufu wa madaktari"! give me a break kaka.



Mzee mawazo yenye nguvu na fikra sahihi hazina muda asikudanganye mtu. Hili wazo la Demokrasia limetokana na mawazo ya wagiriki wa miaka ileee! Baadhi ya kanuni za uchumi tunazojifunza sasa kwenye classical economy nyingine zimetokana na mawazo ya kina Thomas Aquinas (just price theory), Adam Smith na kina John Stuart Mill, wapo na wengine ambao waliishi miaka ile ya nzige na mawazo yao hadi leo tunayaboresha zaidi na mengine tunakubaliana nayo zaidi.

Mawazo ya kina David Hume, na John Locke yote yalitolewa miaka mia kadhaa iliyopita; Soma maandishi ya Smith ya Wealth of Nations utaona ni jinsi gani nadharia zenye nguvu zinaishi na hazipitwi na muda.


mkuu wangu nitarudi baadaye hii ngoma bado mbichi.....!

well, of course ila uje na hoja zenye nguvu, you are making this too easy!
 
See...this is exactly what I'm talking about....if I were FMES...I would quit this debate....it's becoming a no contest...
 


Ndio maana wengine tunasema Nyerere was ahead of his time! alijua kama mwanadamu ana mipaka gani na yeye mwenyewe alisema kuwa aliyoshindwa kuyafanya kwa miaka 20 hatoweza kuyafanya kwa miaka mingine mitano. Akaamua kuachia ngazi. Huyo anaitwa kiongozi kaka. Laiti wengine wangefuata nyazo zake, tungekuwa mbali.. lakini wanaandelea kuwa ving'ang'anizi. Wanafunzi wazuri wa Mwalimu ni wale walioona alama za nyakati.

Salim
Butiku
Warioba
Msuya

na wengine ambao walijua madhaifu yao ya kibinadamu wakaamua kukaa pembeni, hivi Kingunge angeamua kuachia ngazi wakati ule si tungekuwa mbali..? Majina mengine naogopa hata kuyataja. Mnawajua.

Na hili ni jambo ambalo CCM inabidi wamshukuru Nyerere, hasa kwa kitendo chake cha kushinikiza mabadiliko ya katiba ili kipindi cha urais kiwe na kikomo cha mihula miwili.

Huyo anaitwa kiongozi, kama angetaka kukaa miaka mitano zaidi Nyerere angeweza, you know that, and I know that. Ndio maana hata Mandela baadaye akafuata nyazo hizo hizo. Kwa kuonesha mfano wa kung'atuka sisi sote hatuna budi kushukuru sana siyo CCM peke yake.
 
See...this is exactly what I'm talking about....if I were FMES...I would quit this debate....it's becoming a no contest...


Nyani wewe ndio chief instigator.. naweza kukuona miaka ile ulikuwa unawaweka watu mchanga mkononi na kuwaambia "puta".!! yaani nimecheka kwa chombeza zako hadi sina hamu. Basi naona tumsubiri mzee mwenzangu akirudi.
 
Nyani wewe ndio chief instigator.. naweza kukuona miaka ile ulikuwa unawaweka watu mchanga mkononi na kuwaambia "puta".!! yaani nimecheka kwa chombeza zako hadi sina hamu. Basi naona tumsubiri mzee mwenzangu akirudi.

Sitashangaa akirudi na kugeuza debate kutoka Nyerere na kuwa ya Malecelea ili akugalagaze kama ulivyomgalagaza wewe....kwikwikwiiii
 
Sitashangaa akirudi na kugeuza debate kutoka Nyerere na kuwa ya Malecelea ili akugalagaze kama ulivyomgalagaza wewe....kwikwikwiiii

mzee kwenye hilo nitasalimu amri hata kabla ya kipenga, nilishampa ushindi wa mezani yaani hata kutokea ulingoni sitaki. LOL...
 

Mkuu Ngabu umenivunja mbavu.Yaani ni ukweli ambao umeuandika kiaina "Unaintertain sana"

Mwanakijiji
Ni vizuri umemuuliza suali la wapi Nyerere alitaka viongozi wawe masikini.
Azimio la Arusha nia yake haikuwa kuwafanya viongozi wawe masikini ila ilikuwa kuwazuia wasifanye haya wanayofanya sasa. Kuiba serikalini na kusema zimetoka kwenye biashara yake.Kutumia ofisi za serikali kufanya maamuzi yanayotanguliza maslahi ya Kampuni aliyoko,au aliyonayo na si serikali.
 
..nimesoma waasisi wa CCM wakitambulishwa kuwa ni, Mwalimu Julius Nyerere, na Ndugu Aboud Jumbe.

..kinachonishangaza Watanzania wote tulitambulishwa kama ndugu, halafu Baba wa Taifa hakuitwa ndugu, bali MWALIMU!!

NB:

..Mzee Jumbe,na Mzee Mwinyi,.. walikuwa waalimu pia.
 

Na point yako hasa ni nini? Mbona Seif anaitwa "mwalimu"?

asante.
 
1.
1. Mkuu heshima mbele, sikumbuki hotuba yoyote ya Mwalimu, kwa taifa alipokubali kuwa alikosea, na exactly alikosea nini, hizo interview unazosema, mimi sijawahi kuzisikia na wala sidhani kama kuna wananchi wa vijijini waliwahi kuzisikia, lakini wananchi wote wa Tanzania, walimsikia Mwalimu akimponda Mwinyi kuwa hafai, why? Kwa sababu aliyasema hadharani,

Mara ya kwanza Mwalimu, angalau anagusa tu meble ya hadhara kuwa alikosea, ni pale Kilimanjaro Hotel wakati anamsafishia njia Mkapa, ohterwise sijawahi kusikia hadharani Mwalimu, akisema wazi mbele ya public kuwa mazuri niliyofanya ni 1234, na nilipokosea kama rais wa jamhuri ni 12345, kwa hiyo ninangependa wanaofuata wasirudie makosa niliyoyafanya, never! alichokuwa akifanya ni kuwasakama viongozi aliowaachia, ninarudia tena kuwa Mwalimu, alipaswa kusema wazi tena kwa public, Rais Nixon alipojiuzulu kuukwepa mokondo sheria alisema wazi makosa yake, na viongozi wote wastaarabu hufanya hivyo, sio kwenye interview ambazo waananchi wachache wa taifa lako wana access nazo.

2. Uungwana ni pamoja na kukataa kulazimishwa kukubali uongo wa siasa, haiwezekani kuwa Mwalimu na Jumbe walikaa chini, wote kwa nia njema kabisa, wakakubaliana kuunda muuungano wa vyama vyao vya siasa, halafu baadaye muda hata sio mrefu Jumbe akabadilika na kuyakana mawazo yake mwenyewe juu ya muungano aliokubaliana nao kwa hiari yake mwenyewe, I mean huenda kuna wananchi wanaweza hapa JF ku-buy hiyo, lakini I m sorry sio mimi mkuu. Hii siku zote ndio ilikuwa tabia ya Mwalimu, kuwachezea wananchi akili, ndio maana Binaisa, siku zote anasema kuwa alikuwa ni mkuu wa mkoa sio rais wa Uganda, kwenye makubaliano hayo ya CCM Msekwa, alikuwepo, lakini siku moja alipohojiwa Lusaka, akatakaa kabisa kuwa hakuhusika na uamuzi na kwamba nia ya Mwalimu ya centralization imeshindwa kabisaa, aliporudi tu akaenda kuwa RC Tabora, now we can go on and on, bado ninasimamia hoja yangu ya msingi kwamba Mwalimu, aliandika hizi katiba za CCM peke yake, hawa viongozi wetu wa "Yes Man" aliwatumia tu kama alivyomtumia Marehemu Karume, kuanzisha muungano ambao alikuwa akiujua yeye tu, tena mkuu wangu ni yeye akiwa amestaafu ndiye aliyeamua kuwa cheo cha waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais vitenganishwe, na kwamba makamu wa rais lazima atoke Pemba, nenda kwenye maandishi yako utakuta kama kawaida alishirikiana na viongozi kufanya hayo maaamuzi.

3. Mkuu tunasoma maneno ya kina George Washington, maneno ya kina Churchhill, I mean yalisemwa miaka mingi iliyopita lakini mpaka leo ni applicable na yanaonekana kwenye matendo ya siasa na sheria za hayo mataifa, ni bongo tu maneno ya Mwalimu hayawezekani, kwanza yalimshinda yeye mwenyewe kuya-implemment, sasa sisi tutayaweza wapi? Wananchi wote tutakuwaje sawa wakati hata vidole vya bin-adam tu haviko sawa? Mkapa mr. clean na mwanafunzi wake yalimshinda, sasa who can do it?

I mean no question kuwa unamjua na unampenda sana Mwalimu, na umejifunza all his ideas na kwamba you can alyways make a good argument on his words hata kama practically ni impossible kuyafanyia kazi as our nation has learned tayari, lakini haibadili ukweli kwamba yamepitwa na wakati, ni mazuri tu kuyasoma, lakini practically ni bure,

sasa tuko kwenye ubepari mkuu, na umeanza yeye mwenyewe akiwepo hatuwezi kurudi nyuma tena kama walivyosema Butiama, nonesense, sasa tunaangalia mbele, maneno ya katiba za vyama hatuyahitaji tena tunataka the rule of law, haiwezekani taifa zima li-freeze kwa sababu CCM wanakutana Butiama, ni lini US ili-feeze, eti kwa sababu Democrats au Republicnas wanakutana, never, vikao vya CCM na upinzani vinatakiwa viwe serious na kuzumngumzia sheria za jamhuri, sio maneno ya maadili who needs maadili? Na wanapokutana sisi wananchi na taifa tunaendelea kama kawaida kwa sababu wote tunajua kuwa tuna sheria za jamhuri, hili taifa limedumaa kisiasa na kisheria kwa sababu ya maadili yaliyoshindwa, tumechezewa weee na viongozi wachache wakijitajirisha huku sisi tumeshikilia maadili, sasa eti tuyarudie tena, no way!

Ahsante Mkuu!
 
Mwanakijiji upo? Naona Mzee kajibu mapigo....kazi kwako sasa...
 
Nyerere pamoja na mazuri yote aliyofanya alijishushia hadhi aliposhiriki kuvuruga uchaguzi Zanzibar moja kwa moja kwa kumuweka Salmin wakati Seif alishinda.

Hii hata wazee wa CCM who are worth their names in salt wote wanajua, si siri.

Sijui Mzee aliona kila legacy yake inashindwa iliyobaki ni "Amani" ambayo iko controversial na huo muungano, sasa akaona CUF akichukua Zenj muungano utakuwa bye bye.

Akatupilia mbali principle zote na kusema "over my dead body"

Just showing you how fallible we all are, Nyerere or not.
 
We all know we are fallible...
And no one said Nyerere was infallible...next
 
Sasa nikikuuliza ni lini Mwalimu alikuwa na fikra kuwa viongozi wawe masikini? Ni wapi na lini Mwalimu aliwahi kusema kuwa viongozi wawe masikini? Hizo siyo fikra za Mwalimu.

Viongozi kutokuwa na mali, ilikuwa ndio hasa the heart of Azimio La Arusha, kwenye mkutano wake pale Kilimanjaro Hotel, alisisitiza sana hiyo hoja kuwa viongozi wachague between biashara na uongozi maana haviendi pamoja, na akashauri wengine waache uongozi wakalime mashamba yao,

Alichoshindwa kusema hapa ni kwamba katika uongozi wake wote ameshindwa kusimamia sheria, na kwamba viongozi kuwa matajiri wa kupindukia katika kipindi kifupi cha Mwinyi, ilikuwa ni kwa njia za kuizunguka sheria, na yeye Mwalimu, alipaswa kudai sheria ifuate mkondo kwa wale wote wanoshukiwa na wizi wa mali za serikali na wananchi, lakini wapi kwa sababu nia ilikuwa kumpitisha Mkapa tu, mengine hakujali ambayo ni ya muhimu kwa taifa mradi tu alichotaka kimefanikiwa, lakini he was smart enough kuandika vitabu maneno meeengi, kumbe anachotaka ni kumpitisha mkapa tu, au Mwinyi, against ridhaa ya wa-Tanzania karibu millioni 35, sasa eti tukayarudie tena maneno yake ili as a nation tufanikiwe? No tutaishia kuvaa magunia kama wananchi wa Mtwara, enzi zile!

Yes, Mwalimu alipenda viongozi wawe masikini, ndio maana alipofariki tu, si umeoan mwenywe jinsi kuanzia na mwanafunzi wake mwenyewe Mkapa, mambo aliyoyafanya, na wengine wakimfuatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…