Ibara ya 15:1 na 2


Mimi mkuu ndio maana nikasema huko nyuma na ninarudia tena kwamba, wewe ni kati ya wana CCM wachache kabisa ninaoendelea kuwaheshimu maana mnadiriki kulisimamia taifa hata kama kufanya hivyo mtakisuta chama chenu. Nilianza ku-highlight point nzito zaidi hapo juu nikajikuta zote ni nzito na hivyo nikaacha. Hii ni hoja nzito mkuu wangu, tena naomba ruhusa rasmi nije ninukuu maneno yako haya kwenye moja ya makala zangu kwenye gazeti. Ahsante sana, tuendelee kuelimishana kupitia hii njia mahsusi tuliyoletewa na ndugu yetu Invisible. Kwa hoja zako hizi mimi naenda zangu kunywa Fosters, tuonane kesho.
 
Nyerere pamoja na mazuri yote aliyofanya alijishushia hadhi aliposhiriki kuvuruga uchaguzi Zanzibar moja kwa moja kwa kumuweka Salmin wakati Seif alishinda.


Nafikiri hamna kitu kinachomchafua Nyerere kama hiki. Tena alipanda mbegu mbaya sana maana baada ya hapo aliwapa kiburi wajukuu zake kwamba kunyang'anya ushindi sio jambo baya. Hili kwa kweli litaendelea kumsuta hata huko alipo.
 
Mimi mkuu ndio maana nikasema huko nyuma na ninarudia tena kwamba, wewe ni kati ya wana CCM wachache kabisa ninaoendelea kuwaheshimu maana mnadiriki kulisimamia taifa hata kama kufanya hivyo mtakisuta chama chenu.

Mkuu wangu Kitila,

Heshima mbele mkuu, I am humbled kama wewe Mwalimu wa waalimu, unayeweza hata kufundisha waliposoma kuanzia rais wetu mpaka waziri mkuu wetu, na mawaziri wakuu wengi wa zamani, licha ya mawaziri na viongozi wetu mbali mbali wa taifa, unaweza kuzikubali baadhi ya hoja zangu kuwa ni za msingi kwa maendeleo ya taifa letu, basi mimi ni kusema amina mkuu.

CCM ni chama changu, tena believe me ninakijua nje ndani na hata hizi moves za hapa na pale, lakini I am not happy na tuliyoyafanya Butiama, it was un-necessary kwenda kule, hakukuwa na sababu ya msingi, huenda uamuzi wa kura ya maoni ni a big political word inayoweza kukumbatiwa na yoyote mpenda maendeleo ya taifa na demokrasia, lakini bado CCM wanahitaji kutoa maelezo zaidi, kwamba itafanyikaje iwapo kwenye kupiga kura kumekuwa na kasoro kila wakati, na kwamba wanachi wengi hawana imani tena na uchaguzi wahuko visiwani na CCM, hoja ambayo ndiyo hasa chanzo cha muafaka.

Otherwise, I love Mwalimu, he was the greatest ever, lakini nina tatizo kubwa sana na maneno ya kuanza kurudia maneno yake na kuyasmabaza maandishi yake, mimi ninafikri tunmahitaji fresh ideas of how to move forward, baadhi ya viongozi wa CCM waliohusika kupitisha hili azimio, ni vyema tu wakakubali kuwa hawana uwezo wa kuongoza na kuwaachia wengine wenye uwezo, maana wapo.

Ahsante again kwa kunielewa hoja yangu ya msingi, ila kama ninavyosema kila wakati mimi sio an-intellectual, na ninasema kwamba wa-Tanzania, tujitahidi kuongea lugha za siasa ambazo wananchi mpaka wa chini wanaweeza kuzielewa, ni tatizo moja kubwa sana linawasumbua ndugu zetu wa upinzani Tanzania, sasa hivi, wananchi hawawaelewi vizuri wanachosema, lakini ninaaamini pole pole tutasogea, na taifa lolote hapa duniani ambalo haliwezi kuuheshimu upinzani wake wa ndani kisiasa, basi hilo taifa ni dooomed.

Ahsante Mkuu.
 
Here we go...

1.

1. Mkuu heshima mbele, sikumbuki hotuba yoyote ya Mwalimu, kwa taifa alipokubali kuwa alikosea, na exactly alikosea nini,

Hapa umesema vizuri kuwa "hukumbuki". Sasa wewe kutokukumbuka haiondoi ukweli kuwa alisema. Lakini kwa vile umesema hukukumbuka ni jukumu langu basi kukumbusha kwa moyo mkunjufu na wa furaha.

Mwalimu Nyerere alizungumza kwenye taafrija aliyoandaliwa na Jeshi la Magereza wakati wa kung'atuka kwake mwa 1985. Katika hotuba yake ile alielezea mlolongo wa mafanikio ya utawala wake na mapungufu yake. Alielezea alifanikiwa wapi na wapi alishindwa na kwanini aliamua kung'atuka. Natumaini hilo litakukumbusha.

hizo interview unazosema, mimi sijawahi kuzisikia

Sasa wewe kutozisikia hakuondoi ukweli kuwa alisema. Wewe kutopata mwanga wa jua haina maana jua halimuliki. Sasa kwa vile hukusikia, naomba nipendekeza usome mojawapo HAPA na kama utakuwa na muda unaweza kujisomea interview yake nyingine HAPA. Yote ni katika kukuonesha kuwa mahojiano ya Mwalimu hayako mbali na vidole vyako, with a few clicks unaweza kuaccess a fountain of amazing political thoughts of our time. Just try.


na wala sidhani kama kuna wananchi wa vijijini waliwahi kuzisikia, lakini wananchi wote wa Tanzania, walimsikia Mwalimu akimponda Mwinyi kuwa hafai, why? Kwa sababu aliyasema hadharani,

"Sidhani" sasa kudhani ni kitu ambacho mtu hawezi kukiondoa kwa sababu watu wanadhania vitu vingi na mara nyingine havina msingi wowote ule. Hivyo kama unadhani haitoshi. Lakini inashangaza kwa ujasiri unapodai kuwa "wananchi WOTE wa Tanzania walimsikia Mwalimu akimponda Mwinyi kuwa hafai". Mimi ni mmojawao na sikumsikia akisema hivyo. Hivyo, kwa vile na mimi ni mmoja wa wananchi hao na sikumsikia kwa hiyo chumvi yako ya "wote" inaonekana kuwa si kweli. Na sitoshangaa wapo na wengine hapa ambao walikuwepo nyumbani wakati ule na wao hawakumsikia.

Hivyo aidha umetia chumvi au unaongopa kwa sababu ulijuaje kuwa "wananchi wote" walimsikia?


Wrong again, nimekupa mfano wa hotuba mbele ya Magereza lakini hotuba nyingine ni ile ya Mei Mosi 1995 pale Uwanja wa Sokoine. Katika hotuba ile aliyoiita "Tumetoka wapi, Wapi Tulipo, na Tunataka kwenda wapi" Mwalimu alijikosoa yeye mwenyewe na wakati huo huo kukosoa wale waliomfuatia na pia kutupa angalizi kwa wale watakaokuja.

Katika hotuba hiyo alitoa mifano wazi ya wapi kama Rais alikosoea, na ukichukua muda kuipata hotuba hiyo utashangaa jinsi gani hakusita kujikosoa ukilinganisha na hawa ndugu zetu wa sasa ambao hakuna anaweza kukosea, kwani wao hawakosei, na hawawezi kukosea. Wakiambiwa wamekosea wanalia "bangusilo" au wanawalaumu wasaidizi wao.

Lakini kwa vile ni wazi kuwa hujui mengi aliyoyasema Nyerere hadharani nikukumbushe kuwa mwaka 1971 Mwalimu akiangalia miaka 10 baada ya Uhuru alifanya ukosoaji wa miaka 10 na alianisha kwa vipengele wapi tumefanikiwa na wapi kulikuwa na matatizo.

kwa hiyo ninangependa wanaofuata wasirudie makosa niliyoyafanya, never!

Once againa unadeclare rather boastfully kuwa "never" wakati hukuwahi kusikiliza hotuba ya Mwalimu ya Mei Mosi 1995 Uwanja wa Sokoine. Siku ile Mwalimu alisema makosa ambayo wanaomfuatia wasirudie. Alionesha makosa ya utawala wake, alionesha makosa ya utawala wa Mwinyi, lakini pia alitoa uangalizi kwa utawala wa Mkapa. Nakuhakikishia kama Mkapa angesikiliza hotuba ile asingeombea Nyerere afe mapema ili ajipatie Kiwira!


alichokuwa akifanya ni kuwasakama viongozi aliowaachia, ninarudia tena kuwa Mwalimu, alipaswa kusema wazi tena kwa public,

Nitarudia tena, Nyerere alifanya hivyo hadharani siyo kwenye hiyo interview peke yake. Kwa hotuba yake ya kuliaga Taifa (Pale Magereza) na pia kwenye hotuba yake ya Mei Mosi ambazo zote zilitangazwa moja kwa moja na RTD. Tatizo ni kuwa waliosikia "hawakumbuki" au niseme hawataki kukumbuka!


Rais Nixon alipojiuzulu kuukwepa mokondo sheria alisema wazi makosa yake, na viongozi wote wastaarabu hufanya hivyo, sio kwenye interview ambazo waananchi wachache wa taifa lako wana access nazo.

Nirudie tena Mwalimu alisema makosa yake wazi na mojawapo ni kwenye hiyo interview. NI kiongozi gani mwingine aliyekuwa na ujasiri wa kukiri makosa? Kuna mtu amemuuliza Rais Mwinyi makosa ya uongozi wake? Je kuna wakati wowote mwinyi alisema katika utawala wake yeye alikosea wapi? Vipi kuhusu Mkapa; Hivi Mkapa alikosea mahali popote pale?

Tuwaulize waliokuwa Mawaziri wetu wakuu; Salim alikosea wapi amewahi kuliambia Taifa? Vipi kuhusu Malecela, amewahi kuliambia taifa wapi alikosea kama kiongozi? Vipi kuhusu Warioba (pamoja na kuwanyoshea kidole wengine) ni lini yeye alisema amekosea kitu? Hata mzee Kawawa (aliyesimamia kampeni ya Operesheni vijijini) ni wapi amewahi kusimama na kusema "nikiwa Waziri Mkuu nilikosea hapa au pale"? Vipi kuhusu Sumaye lini amewahi kusema amewahi kukosea au hata kuandika akijikosoa (self criticism)? Vipi kuhusu Lowassa si yeye aliyelia "nimefadhishwa sana na nimefedheheka sana" alikubali kosa lolote?

Hawa wote hakuna hata mmoja aliyewahi kuwa na ujasiri wa kusema alikosea nini na watu wanafanya kana kwamba hawakufanya makosa. Ugonjwa huu sasa umemvaa Kikwete kiasi kwamba yeye naye hakosei na hana muda wa kuangalia wapi alikosea. Hadi hivi sasa ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania ambaye alikuwa na ujasiri wa kujiangalia, kujichunguza, kujikosoa na kusahahihisha makosa yake.

JokaKuu hapo juu amesema kuhusu Zanzibar, namkubalia lakini si Nyerere aliyekaa na kuzungumza na Seif? Si Nyerere aliyezungumza na Mrema? Si Mwalimu aliyetoa wazo la kurudisha serikali ya Mseto; Je yawezekana alitambua makosa yake? I bet he did; na hivyo ndiyvo viongozi wazuri hufanya, hawaogopi kujikosoa.


Mzee, usichagua mada sikuwa nazungumzia suala la jumbe tu, nazungumzia madai yako ambayo unayoyatoa with "sweeping statements" kuwa "Mwalimu "Never" did this or that" wakati nimekuonesha kuwa alifanya hivyo.

Na kuhusu suala la Jumbe mzee, haikuwa kuhusu CCM; kutofautiana kwake na Nyerere hakukutokana na Muungano wa ASP na TANU. Naweza kukufunza kidogo suala la Zanzibar lakini wapo mabingwa hapa toka visiwani na bara ambao wanaweza kukuambia ni nini hasa waligongana mawazo kati ya Nyerere na Aboud Jumbe. Haikuwa kuhusu Muungano wa Vyama, hapana mzee hilo si kweli.

Mzee Jumbe si yuko Mji Mwema hapo Kigamboni kaka, nenda umuulize kama mgongano wao ulikuwa kuhusu CCM? Ulikuwa ni mgongano wa fikra ambao Watanzania wanapaswa kuusoma na kuulewa.


I mean huenda kuna wananchi wanaweza hapa JF ku-buy hiyo, lakini I m sorry sio mimi mkuu.

Mzee hapa hatulazimishi mtu kukubali kitu lakini ni jukumu la mtu mwenye dhamira safi kuukubali ukweli hata kama utapindua kila hoja aliyokuwa anasimamia. Ni rahisi kung'ang'ania kubisha ili mtu aonekane mbishi, lakini ukiweka facts na siyo mawazo ya juu ambayo hayana msingi wa ukweli basi ni jukumu la mtu kuchagua ukweli.

A haste generalization and a mediocre attempt to tarnish Nyerere's legacy and in a way demonize his principles will prove to be futile. Any mind that is clear, fair, and balanced will look at the evidence presented and on the merit of the evidence alone will make a decision kama Nyerere aliwahi kukubali makosa au la; aliwahi kusahihisha makosa yake au la


Hii siku zote ndio ilikuwa tabia ya Mwalimu, kuwachezea wananchi akili,

Hapana Mkuu wangu, mwalimu hakuwa anachezea watu akili "siku zote". Yaani, mtu mmoja alichezee akili taifa zima basi Taifa hilo halistahili hata kuwepo!

now we can go on and on, bado ninasimamia hoja yangu ya msingi kwamba Mwalimu, aliandika hizi katiba za CCM peke yake,

Mzee unaweza kusimamia hoja yako kwa sababu unaamini ni kweli licha ya ushahidi kuonesha vinginevyo. Kama Mwalimu aliandika Azimio la Arusha peke yake, aliandika Katiba ya CCM peke yake, aliandika Mwongozo wa CCM peke yake na nyaraka mbalimbal zote yeye mwenyewe, basi unanifanya niamini kabisa kuwa alikuwa ni mtu mwenye kipaji kikubwa kiasi kwamba hawa wengine wote walishindwa kushindana nacho.

Na inawezekana kuwa ni kweli, kwani tangia Mwalimu aondoke sijasikia kiongozi mwingine yoyote wa CCM aliyeweza kuarticulate mawazo yake na nadharia zake kama Mwalimu. Hakuna.


3. Mkuu tunasoma maneno ya kina George Washington, maneno ya kina Churchhill, I mean yalisemwa miaka mingi iliyopita lakini mpaka leo ni applicable na yanaonekana kwenye matendo ya siasa na sheria za hayo mataifa,


Mzee yawezekana unahusudu maneno ya wazungu zaidi lakini yakisemwa na mwanakijiji toka Butiama basi hayafai. Si Wamarekani waliosema "Binadamu wote ni sawa" (Angalia "we hold these truths to be self evident, that all men are created equal") Na Mwalimu anaporudia kama mwangwi maneno hayo na kusema "Binadamu wote ni sawa" unayaona "hayawezekani Tanzania.


ni bongo tu maneno ya Mwalimu hayawezekani, kwanza yalimshinda yeye mwenyewe kuya-implemment, sasa sisi tutayaweza wapi?

Mzee, kutowezekana kwa mawazo au fikra fulani haina maana ni fikra za uongo. Labda tatizo haliko kwa aliyetoa mawazo hayo bali kwa watekelezaji. Lakini pia naweza kuona nuru kigodo ya kwanini tunapata shida kwa sababu tuna watu ambao wanaamini kuwa kuna "vitu haviwezekani" Tanzania na hivyo tukubali tu yanayoendelea.


Wananchi wote tutakuwaje sawa wakati hata vidole vya bin-adam tu haviko sawa? Mkapa mr. clean na mwanafunzi wake yalimshinda, sasa who can do it?

Yaani, kama ulielewa Mwalimu alikuwa ana maana ya "usawa wa kimo" au vitu ambavyo ni vya maumbile basi mzee nitakuwa na kazi kubwa sana. Na kwenye hiyo mada niliyofungua nitatumia muda kuonesha kuwa Mwalimu hakuwa anazungumzia mambo ya fedha, urefu, elimu n.k alipokuwa anazungumzia "usawa wa binadamu".


I mean no question kuwa unamjua na unampenda sana Mwalimu, na umejifunza all his ideas na kwamba you can alyways make a good argument

Mzee, simpendi Mwalimu kwa sababu ni Mwalimu, mapenzi yangu yanatokana na mvuto wa fikra zake ambazo mtu yeyote atachukua muda kuzisoma ataelewa utajiri wa kina, na upana wa hoja zake kiasi kwamba zinatosha kumbadilisha kifikra mtu na kumfanya siyo tu alipende Taifa lake bali pia awe tayari kulitumikia na kulisimamia kwa moyo wake wote.

Wale ambao wanaziogopa fikra za Mwalimu wanaziogopa kama vile mtoto anavyoogopa kiboko cha Mwalimu shuleni. Wanazihofia fikra hizi kujulikana na kusambazwa kwa sababu zitafungua mawazo ya watu na kuwapa uhuru na mapenzi kwa Taifa lao.

Fikra hizi kwa wengi zinaendelea kubakia kama hazina iliyofichika, ambayo wale wanaoipata hufurahia. Fikra za kian Plato na Socrates, Aristotle na wengine waliotutangulia bado ni lulu. Na nikuhakikishie kuwa CCM wasifanya makosa ya kutafsiri na kusambaza Mawazo ya Mawazo ya Mwalimu kama walivyoamua kufanya Butiama.
on his words hata kama practically ni impossible kuyafanyia kazi as our nation has learned tayari, lakini haibadili ukweli kwamba yamepitwa na wakati, ni mazuri tu kuyasoma, lakini practically ni bure,

Mzee hatujayafanyia kazi mawazo ya mwalimu, ni kama kilele ambacho tumekwepa kukifikia kwa sababu ni kigumu. Tumeamua kutafuta njia ya mkato.

sasa tuko kwenye ubepari mkuu, na umeanza yeye mwenyewe akiwepo hatuwezi kurudi nyuma tena kama walivyosema Butiama,

Once again, unaonesha ni jinsi gani umeyamiss mawazo ya Nyerere. Hakuna aliyesema tumeingia kwenye Ubepari. Hawa waliopo sasa wenyewe wanaogopa kusema tuko kwenye Ubepari. Kwa nini? Mawazo ya Mwalimu hayapingani na Ubepari. Bali yanaupa Ubepari sura yake ya kibinadamu. Na leo hii nchi nyingi za Kibepari zenyewe bila kujua au zikijua zimekuwa zikichota leo katika mawazo ya kuufanya Ubepari uwe na sura ya kibinadamu.

Wale tuliosoma Political Economy kama wewe mzee utakumbua ile maxim ya zamani ya Ubepari kuwa "everybody for himself but God for us all". Ubepari wa zamani ulikuwa hauna room kwa serikali kuingilia kati maisha ya watu na kuwa na sura ya huruma.

leo hii kina Bush wamekuja na "Compassionate conservatism" na kina Obama na Hillary wote wanajaribu kuifanya Marekani iwe inajali. Hata Bepari kama Bush leo hii anakuja na vitu vya "No Child Left Behind" na leo wameamua kusaidia watu waliokopa na wenye madeni (kama mimi).

Ndugu yangu serikali ya Marekani leo hii imepitisha sheria ya kutoa fedha za rebate kati ya dola 600 na 1200 kwa kila mlipa kodi kuwasaidia, kaka huo ni ujamaa!! Nenda Ulaya huko uone kama kuna mtu anafuata pure capitalism ambapo individual and profit is the only and ultimate goal of an economic activity.

Hata wao hawaamini tena kwani wangeendelea kufanya hivyo Karl Max na Engel wangeendelea kuonekana kuwa kweli kwani classical capitalism creates its own seeds of destruction. Bila watu kama Mwalimu Ubepari usingekuwa na sura uliyonayo sasa.

Watu wengi hawajui lakini siku moja watajua, Mwalimu na taasisi kama Oxfarm na Jubilee 2000 walisaidia sana kujenga huu Ubepari tunaouona sasa.


Duh, imebidi nirudie maneno hayo mara kadhaa kuhakikisha kuwa ni wewe umeyaandika. Kaka Sheria za nchi zinatokana na vyama vya kisiasa. Chama kilichoko madarakani ndivyo chenye kuunda sheria kufuatana na ilani yake. Ndio maana usishangae wakiingia kina Obama au Hillary baadhi ya Sheria zilizopitishwa na Bush zitafutwa! Ndio Demokrasia.

Na hata Tanzania wakiingia CUF (wakishika Urais na Bunge) usitarajie baadhi ya sheria kuendelea kuwepo. Huwezi kujadili sheria za Jamhuri bila kuangalia vyama vya siasa. Ndio maana wengine tunafuatilia sana hawa wanasiasa wanasema nini na kufanya nini kwa sababu maamuzi yao yanagusana moja kwa moja na sheria zetu.

Kama uhusiano wa vyama vya siasa na uundaji wa sheria hauuoni itabidi nitoe somo la "Siasa 101"

sio maneno ya maadili who needs maadili?

Mzee tumia muda kidogo kufikiri badala ya kutoa maneno ya namna hii.. yaani "who need maadili"?!! I will not even try to answer this one.


Somebody please choke meee! Naomba mtu mwingine anisaidie kuhusu umuhimu wa maadili katika Taifa maana nikianza naweza kuvunja hii keyboard.

Ahsante Mkuu!

Asante na wewe mzee, ila unajitahidi sana and I really appreciate your zeal. Na usikubali haya ya kuamua kuachia ngazi kama wanavyomtaka Hillary, you better fight to the bitter end. Ndio uungwana huo.
 
mwanakijiji if anything that CHARLAYNE HUNTER-GAULT: interview you linked reinforces the idea kuwa Nyerere hakukubali kuwa alikosea


Haambiliki


Hapa kaona aibu kusema hakuna alichokosea


So the record shows, he admitted his mistakes.
 
mwanakijiji if anything that CHARLAYNE HUNTER-GAULT: interview you linked reinforces the idea kuwa Nyerere hakukubali kuwa alikosea

mzee umeangalia swali swali la Charlayne jinsi alivyomchomekea Mwalimu? Halafu angalia swali aliloulizwa na huyo mwandishi mwingine. Kimsingi Hunter-Gault aliuliza swali akiwa anassume kuwa nyerere alisema Ujamaa was "miserable" failure and hence jibu la Nyerere

JULIUS NYERERE: Where did you get the idea that I thought "Ujamaa" was a miserable failure?

lilikuwa ni jukumu la Ms. Hunter-Gault kusema nilisoma, nilikusikia ukisema hivi au vile. Angalia utetezi wake. Alichokisoma sicho alichomuuliza Nyerere.
 

Maneno ya CCM ni sahihi siku zote na wananchama wote wa CCM nilazima waweke mbele mambo ya CCM kwanza ndiyo waitumikie nchi.

Shame on you Mtanzania kwa kujaribu kutaka kupindisha maneno ndani ya katiba ya chama chako mwenyewe.
Tena naomba ulegee na unyong'onyee kabisa mbele ya wana CCM wenzako.
Shame on you.
 


Vikao vya kuhudhuriwa na wanywa kahawa na kashata huku wakisubiri Per DM na muda wa kupiga makofi na kuimba CCM CCM CCM?
Usahihi wa katiba ya chama chochote Tanzania ni muhimu kwa maendeleo ya Kila mTanzania. tatizo la kikatiba lililoko Chadema ni vema lishughulikiwe leo kwani siku wakishika madaraka itakuwa too late.
Matatizo ya katiba ya CCM ni lazima yasemwe, yajadiliwe na kupembuliwa kama njugu. Uamuzi wa kubadili katiba ni wao CCM, hatuwalazimishi wabadili katiba.
Tukiwa watanzania na waathiriwa wa moja kwa moja wa maamuzi ya siasa za CCM tuna haki ya kujadiri katiba ya CCM.
Kama watu huru katika nchi huru ,pia tuna haki ya kujadiri katiba ya CCM kwa kina, kwa upana na kwa uwazi bila kuhofu vimaneno kutoka kwa the so called wanachama damu kijani.

Zaidi ya nusu ya kura zilizo muweka MH Kikwete madarakani zilipigwa na watu wasio wanachama wa CCM.

Kama kuna ngendembwe na ngebe za kuwatosa wasio wanachama wa CCM kujiingiza kwa wanaCCM basi ziletwe kwanza zile za watu wasio wanachama wa CCM kumpigia kura mwana chama wa CCM, hapo mtaeleweka.
 

Mkuu Pundit,

Ahsante mkuu, this is very interesting.
 

Hotuba yako kama kweli, aliitoa kwenye magereza, sasa alipomponda Mwinyi, kuwa hafai alisema mbele ya waandishi katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja na media zetu, na isitoshe akaandika na kitabu kabisa, sasa ni wewe peke yako ambaye hukuisikia hiii hotuba ya Mwalimu, plae Kilimanjaro Hotel akimkashifu Mwinyi, sasa labda ukisema kuwa hiyo hotuba ya magereza ilitangazwa moja kwa moja kwa taifa, sikumbuki hilo,

Halafu by the way, huko alikosema kuwa alikosea, exactly alisema alikosea nini au wapi?
 

Mkuu this is great, sasa vipi ukiiweka hiyo hotuba hapa wote tukaisoma ili tujue ni wapi alikubali kukosea, maana ndipo hasa tunaweza kujirekebisha as a nation kwa kufuatilia makosa ya foundation, mkuu iweke hapa tuichambue!
 


Naomba niulize humu ni Watanzania wangapi walimsikia Nyerere akimkashifu Mwinyi pale Kilimanjaro Hotel? Yawezekana labda ni mimi tu. Na hiyo hotuba ya magereza ilitolewa na kutangazwa.

Halafu by the way, huko alikosema kuwa alikosea, exactly alisema alikosea nini au wapi?

Nimeshatoa jibu na Pundit kalirudia, rudi kurasa mbili nyuma mkuu.
 
Mkuu this is great, sasa vipi ukiiweka hiyo hotuba hapa wote tukaisoma ili tujue ni wapi alikubali kukosea, maana ndipo hasa tunaweza kujirekebisha as a nation kwa kufuatilia makosa ya foundation, mkuu iweke hapa tuichambue!


Mzee sasa hiyo itakuwa ni mimi kuwatafunia watu na kuwamezea. Uliza tu wakuu (ninajua una connection) wakupatie mkanda wa video ya hotuba ya Mei Mosi 1995. Inapatikana kiurahisi tu. Unaweza kwenda pale dula la Vitabu vya Serikali karibu St. Joseph unaweza kupata.
 
Hiyo hotuba kule Mbeya kwenye Mei mosi, ilikuwa ni moja ya kampeni zake kumuweka Mkapa, kinyemela, nakumbuka jinsi alivyouchambua utawala wa Mwinyi, ambaye at the time alikuwa ndio kwanza anarudi toka ziara ya Mozambique, na akamjibu Mwalimu, kuwa kama utawala wake Mwinyi ulikuwa mbya iweje hakuwahi hata kupata jkaribio moja la kupinduliwa, as opposed na Mwalimu, aliyepata majaribio chungu nzima huku yeye anadai utawala wake ulikuwa bomba, okay hiyo sasa ninaikumbuka.
 
Na hiyo hotuba ya magereza ilitolewa na kutangazwa.

Hii sijawahi kuisikia wala kuisoma mahali, lakini nitashukuru sana mkuu ukiiweka hapa, wote tukaichambua si unazo zote mkuu.
 
Mwanakijiji, to what degree, if any, was Nyerere's involvement in the purpoted manipulation of the 1995 Zanzibar presidential vote. Because if he did influence it then that and that alone tarnishes his whole persona of a man of high intergrity.

I ask because I don't think you have adequately addressed this issue like you have the other issues concerning him. So I was just wondering what was your take on it...and I'm not clowning around...I'm being serious..
 

Hii ni moja tu ya analysis kuhusu Mwalimu na siasa zake, halafu unaona hapo chini yeye alimchagua Mwinyi, lakini huko wanasema alichaguliwa constitutionally!
 
Mwanakijiji, to what degree, if any, was Nyerere's involvement in the purpoted manipulation of the 1995 Zanzibar presidential vote. Because if he did influence it then that and that alone tarnishes his whole persona of a man of high intergrity.

Swali zuri sana mkuu, sasa ngoja tupate majibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…