Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Nimekuwa nikifuatilia majibizano mbalimbali ndani ya JF ambayo kwa namna moja au nyingine naona hayana tija kwa mustakabali wa taifa letu kutokana na wachangiaji kuishia kurushiana maneno na kutunishiana misuli kwa kushindanisha madhehebu ya dini, lipi zaidi! .Nionavyo mimi hili halikubaliki hata kidogo katika nchi ya Tanzania ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa na hali ya kuvuliana kati ya watu wa imani tofauti!
Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere alikuww mkali katika hili akiweka msisitizo katika kujenga taifa ambalo watu wake wanaheshimiana licha ya kuwepo kwa tofauti za dini, rangi na kabila.Pia nikiangalia uongozi wa awamu ya nne ,Rais Jakaya Kikwete amekuwa mstari wa mbele kukemea mitafaruku ya kidini kwa kutambua athari zake katika kujenga Umoja,amani na mshikamano.
Kwa upande wangu nimekuwa wazi kabisa katika michango yangu kuwa kama ilivyo kwa katiba ya Jamhuri ya Muunganonwa Tanzania ya 1977 kuweka msingi imara katika masuala ya uhuru wa kuabudu na imani ya dini, Katiba inayopendekezwa pia inatoa tiba ya uendeshaji wa shughuli za madhehebu ya dini hasa Uhuru wa Imani ya dini kwa makundi yote,Sura ya Tano, sehemu ya kwanza kwenye Ibara ya 41 imeweka wazi kabisa utendaji wa Serikali kutoingiza masuala ya dini kama inavyosomeka hapo chini,
41.-(3) Shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini itakua nje ya shughuli za Serikali.
Nawaomba watanzania tuungane katika kuchukia hali yoyote inayotakana na baadhi ya watu wachache wanaotaka kutugawa kwa misingi ya dini!
Mungu Ibariki Tanzania!
Naomba kuwasilisha!