Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
98.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha
masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata Kanuni zifuatazo:-
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii (isipokuwa yale yanayohusika na
aya ya (b) ya ibara hii ndogo) au masharti yoyote ya
sheria yoyote iliyotajwa katika Orodha ya Kwanza
kwenye Nyongeza ya Pili utaungwa mkono kwa kura
za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili
ya Wabunge wote;
(b) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya Sheria
yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo
yaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya
Pili iliyoko mwishoni wa Katiba hii, utapitishwa tu
iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambao
idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote
kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge
wote kutoka Tanzania Zanzibar.
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo
ya (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii au masharti ya sheria
maana yake ifahamike kuwa ni pamoja na kurekebisha au
kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine
badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti
hayo.
SWALI BADO HALIJAJIBIWA: Ni ibara gani ya Katiba ya sasa inayoruhusu Katiba hii kufutwa na kuandikwa nyingine? Au ni wapi ambapo kuna chombo kilichopewa madaraka ya kuweza kuanzisha mchakato wa kufuta Katiba hii kama Bunge lilivyopewa madaraka ya kubadilisha vipengele na masharti ya katiba ya sasa?
Hiki kinachoitwa Bunge la Katiba kiko wapi kwenye Katiba ya Muungano? Neno lenyewe Bunge la Katiba halipo kwenye Katiba hii.