Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Mfanyabiashara maarufu mjini Moshi, Ibrahim Shayo 'ibra Line', ameguswa na mafuriko yaliyosababisha athari kubwa kwa wananchi wa Kata za mji mpya na Msaranga na kuahidi kuwasaidia vifaa mbalimbali ikiwamo mashuka na magodoro.
Usiku wa kuamkia Leo mvua kubwa iliyonyesha imeziacha familia nyingi bila makazi baada ya nyumba zao kuanguka huku mazao na mahitaji mengine ikiwamo mifugo nayo ikisombwa na Maji.
Mfanyabiashara huyo ambaye miongoni mwa wahanga wa mafuriko hayo ni wazazi wake,ameotoa wito kwa wadau wengine kuwasaidia wahanga hao.
Akiwa kwenye kata ya mji mpya ambako ni nyumbani kwa wazazi wake, ametoa wito pia kwa wataalamu kuangalia namna ya kutatua changamoto ya mafuriko hayo ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuleta athari kubwa kwa wananchi ikiwamo uharibifu wa Mali.
Tangu usiku wa manane mfanyabiashara huyo alikuwa Katika hekaheka za kuokoa wahanga wa mafuriko hayo kwenye kata hiyo ambako baadhi ya wanafunzi walikwama kwenda mashuleni kutokana na mvua hizo.
Watu watano wakiwamo watoto watatu wa familia moja wameripotiwa kufariki Dunia baada ya nyumba Yao waliyokuwa wakiishi kuangukiwa na kifusi.
Watoto hao wameripotiwa kufariki Dunia kwenye kata ya Kimochi wikaya ya Moshi Vijijni huku miili ya watu wengine ilkiopolewa maeneo ya Msaranga na mto Rau.
Inadaiwa kuwa Kingo za mto Rau zilishindwa kuhimili nguvu kubwa ya maji Hali iliyopelekea kuvunjika na Maji kujaa kwenye makazi ya watu huku kingo za Daraja la Kwa Otieno Katika kata ya Mji Mpya nazo zikivunjwa na Maji.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi,maiti zote tano zimeopolewa huku timu ya uokoaji ikipambqna kurejesha hali ya utulivu kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo.